Friday, July 5, 2013

Sumaye azindua ziara Dsj

 Posted on 5jully 2013
Waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Fredrick Sumaye amezindua safari ya kuelekea nchini Kenya ya wanafunziwa chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam (DSJ).na kuwataka kutumia fursa hiyo kuitangaza zaidi Tanzania

Sumaye amezindua safari hiyo chuoni hapo na kuwataka wanafunzi kwenda kujifunza utalii na jinsi ya kumudu maisha pasipo kutegemea kuajiriwa na serikali bali kujiajiri wenyewe kwa elimu waliyoipata.

Pia aliwataka wanafunzi hao kujifunza mazingira ya Kenya jinsi yalivyo tofauti na ya hapa kwetu Tanzania na hata watalii wengi huvutiwa   kutembelea  nchi hiyo na  kuwaongezea pato lao la taifa.

Alisema kuwa nchi ya Kenya iko juu kiuchumi tofauti na Tanzania  hivyo  basi    mnavyokwenda ni vizuri mkajijifunze kutoka kwa wenzetu na kuja kuyafanyia kazi kwa ufasaha zaidi ili kuleta maendeleo  kwa taifa Letu.

Sumaye aliendelea kusema wafanyakazi wa Kenya ni wafanyakazi waamifu  na wachapa kazi sana tofauti na Tanzania hivyo basi nasi  tukajifunze vitu hivyo katika ziara hii ili tuweze kulijenga taifa letu.

Kwa upande wa biashara alisema Kenya wanauwezo mkubwa wa kufanya biashara za nje tofauti na Tanzania hivyo nasi tukaifunze mbinu hizo za kibiashara kutoka kwao ili tuje kuwa mabalozi hapa nchini..

Ziara hiyo inatarajiwa kuwa ya siku tano kuanzia taehe 9 mwezi wa saba hadi tarehe 14 ambapo malengo ya ziara hiyo ni kujifunza utamadunui wa nje pamoja na kujifunza elimu yao ilivyo tofauti na Tanzania.

Tuesday, July 2, 2013

Simba yamuacha Kaseja

Suala hapa sio kuachwa kwa Kaseja bali Simba walipaswa kuendelea kumuamini  kwani bado ana mchango kwa simba na Taifa stars kutokana na mchango wake ambao amekuwa akiutoa ndani na nje ya uwanja

Kimsingi mchezaji akimaliza mkataba wake huwa anakuwa huru kutafuta klabu yoyote endapo klabu yake haitokuwa na nia ya kumwongezea mkataba mpya

Ikumbukwe kua Kaseja ameidakia Simba kwa miaka kumi yenye mafanikio makubwa  na kuiwezesha kubeba mataji mengi ya ligi kuu bara pamoja na kuiwakilisha vizuri katika michuano ya vilabu barani Afrika

Kwani mnamo mwaka 2003 alifanikiwa kuingoza simba kuwandoa mabingwa wa vilabu barani Afrika kwa wakati huo Zamalek ya Misri na bado aliendelea kuiongoza vizuri Simba na Taifa Stars  hali iliyopelekea kuendelea kuwa kipa namba moja hadi hivi leo

Hata hivyo sababu ambazo zimekuwa zikitolewa na  viongozi ni kuwa kiwango cha mchezaji huyo kimeshuka kitendo ambacho kimekuwa kikipingwa vikali na mashabiki wa soka ambao wanadai Kaseja hajachuja kwa kiasi hicho bali kutakuwa kuna chuki kati yake na baadhi ya viongozi

Nao baadhi ya wadau wameliambia gazeti la upendo kuwa Simba watakuja kumjutia kaseja kwani ana mchango mkubwa na hawajamuona golikipa yoyote Tanzania mwenye uwezo zaidi ya yake hivyo basi Simba walipaswa kufikiria kabla ya kufanya maamuzi ya kumuacha.

Emmanuel Bayo mkazi wa Kinondoni amesema Keseja ni golikipa mzuri sana kwa Tanzania kwani licha ya kuisadia Simba kwa muda mrefu amekuwa pia golikipa chaguo la kwanza kwa Taifa Stara hivyo sina shaka naye akiendelea kuidakia Simba.

‘Pia sababu zinazosemwa kuwa amechuja mimi sikubaliani nazo hivyo Simba wanabidi kuendelea kuwa naye na ataendelea kuwasaidia zaidi kutokana na kiwango anachokionyesha uwanjani pindi anapoiwakilisha Simba au Taifa stars’ alisema Bayo

Abubakar Rasul mkazi wa Buguruni alisema alidhani Simba wangeendelea kumuamini Kaeja kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa klabuni hapo hata kama angekuwa amechuja wangepaswa kuwa nae au kumpeleka kozi ya ukocha ili aje awe kocha wa makipa kutokana na mapenzi aliyo nayo juu ya Simba

‘Hali hii itawavunja moyo hata wachezaji wengine wenye mapenzi makubwa na Simba watacheza huku wakijua hata muda wao utakapoisha watatupwa bila kuthaminiwa mchango wao walioutoa kwa Simba’ alisema Rasul

Hivyo basi viongozi wa Simba hasa hawapaswi kuyapuuza maoni wanabidi wayafanyie kazi ili kuweza kuiboresha Simba ili hiƩndele kuwika Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Thursday, June 27, 2013

TRA:Kodi ya magari kulipwa kwa kwa njia ya mtandao kuanzia 1'Julai

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Benki kuu ya Tanzania (BOT) wamefanya maboresho katika ulipaji kodi kwa njia ya mtandao.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Fedha wa TRA Salehe Mshoro alisema kuanzia Julai mosi TRA na BOT  wataanzisha mfumo wa ukusanyaji kodi utakao unganisha na mifumo ya benki.kuu na benki za biashara.

Alisema kuwa mtu akienda kulipa kodi zile fedha zitakwenda BOT  na papo kwa hapo atapata taarifa kwa njia ya barua pepe  na taarifa zitakwenda kwa haraka TRA zitakazoonyesha kuwa kodi imelipwa.

Alidai kuwa mfumo huu utaondoa migongano ya mara kwa mara na pia watakuwa wamefanya  makubaliano kati ya TRA na wananchi ambao ndio walipa kodi.na pia mfumo huu wamejufanyia majaribu toka mwezi januari.

Aidha alisema mfumo huu utaanza kutumika kwa walipa kodi wakubwa wa malipo yanayoanzia millioni tano(5) ambao hao watakuwa mabalozi kwa wengine wadogo na alisema kumbukumbu zitaingizwa kwenye mamlaka na watapata taarifa.

Mlipa kodi atatakiwa kujisajili kwenye mtandao wa TRA ambao ni www.tra.go.tz akiingia kwenye wwbsite ya TRA anaweza kupata taarifa zake muhimu za usajili na namba za utambulisho na benki yake.

Naye Murugenzi wa mradi Ramadhani Sangeti alisema wamejiunga na mkongo mkubwa wa taifa  na endapo mkongo mkubwa hautapatikana ile mingine itasaidia,

Mategemeo ya TRA ni kuwa utaongeza urahisi wa ulipaji kodi na utaondoa kero za wananchi pia itapunguza muda na kumpunguzia mteja gharama, kwani ni mfumo salama wenye kutoa taarifa kwa wakati.

Mwisho aliwataka walipa kodi pindi watakapopata matatizo yoyote wapige namba za huduma ambazo ni bure  kwa upande wa TTCL na Vodacom ni 08001126 au Tigo ambazo n i 0713800333 na Airtel 0786800000

Saturday, June 22, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

22/06/2013
Na: Simon Mmbando

CUF KUANDAMANA 29 JUNI HADI IKULU,PROF.LIPUMBA KUONGOZA,MAANDAMANO KUPOKELEWA NA RAIS KIKWETE.

Waheshimiwa waandishi wa habari, kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya uongozi wote wa kitaifa wa Chama chetu, naomba kuchukua fursa hii kuwakaribisha Ofisi Kuu ya chama ili tupate fursa ya kuzungumza nanyi na kwa maana hiyo kuzungumza na watanzania kupia kwenu ili ujumbe uliokusudiwa na chama uweze kuwafikia wananchi popote pale walipo.
Tumewaita leo tarehe 22 Juni 2013 tukiwa na agenda moja kuu nayo ni kuwaeleza kwamba Chama cha Wananchi CUF kimeandaa Maandamano ya Amani siku ya tarehe 29 Juni 2013 maandamano ambayo yataanzia eneo la Buguruni kituo cha Mafuta saa nne kamili asubuhi, kupitia barabara ya Uhuru, Mnazimmoja, Bibi Titi, Posta mpya , Aridhi hadi Ikulu.
Maandamano hayo ambayo yataongozwa na Mwenyekiti wa Chama taifa Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, yanatarajiwa kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au mwakilishi wake, na kwamba yanalengo la kufikisha malalamiko ya wananchi kutokana na vitendo vya ukatili vinavyofanywa na jeshi la polisi na jeshi la wananchi ambalo kimsingi taifa letu linaelekea mahali pabaya.
Waheshimiwa waandishi wabari, mtakumbuka tarehe 15 Juni 2013 wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakihitimisha mkutano wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata nne za Arusha, palitokea mlipuko wa bomu uliopoteza maisha ya wananchi wane kwa mujibu wa taarifa za polisi na wengine wengi kujeruiwa vibaya.
Kwa kuwa jambo hili lipo katika hatua za uchunguzi, Chama cha CUF hakikusudii kuingilia uchunguzi unaoendelea lakini tunataka kufikisha ujumbe kwa rais kwamba hii si mara ya kwanza kuundwa kwa tume mbalimbali za uchunguzi hapa nchini. Kinachotusikitisha ni kuwa hata mara baada ya uchunguzi huo, hakuna ripoti inayotolewa hadharani kuonyesha chanzo cha tukio, wahusika na hatua zilizo au zinazotarajiwa kuchukuiliwa.
Tutamtaka Mheshimiwa rais kuhakikisha ripoti ya uchunguzi itokanayo na maafa yaliyotokea Arusha iwekwe wazi na serikali iwachukulie hatua stahiki wale wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo ili iwe funzo kwa wengine au wale wenye kuwa na malengo yanayofanana na hayo kwa kuwa Tanzania ni yetu sote na haitowezekana watu wachache wayachezee maisha ya watu kwa sababu ya kukidhi matakwa binafsi ambayo hayana tija kwa jamii.
Maandamano pia yanalenga kuishinikiza serikali kukomesha vitendo vya kinyama, vitendo vya kijangili vinavyofanywa na Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kuwakamata, kuwatesa, na kubaka wananchi wasio na hatia wa Mkoa wa Mtwara na hasa wanaoishi katika wilaya za Mtwara Mjini, MtwaraVijijini, na Newala huku baadhi yao wakichomewa nyumba zao moto na wengine wakiporwa mali zao.
Waheshimiwa waandishi wa habari, mtakumbuka hivi karibuni pamekuwa na fukuto la suala la gesi katika Mkoa wa Mtwara ambapo baadhi ya maafisa wa Serikali wamekuwa wakipotosha madai ya wananchi ikidaiwa kwamba wananchi wa mkoa huo wamesema hawako tayari kuona gesi yao inatumiwa na wananchi wengine kinyume na wale wa mikoa ya Lindi na Mtwara jambo ambalo si kweli lakini wanayafanya haya ili kuwajengea chuki dhidi ya watanzania wengine ionekane kwamba wananchi wa Mtwara na Lindi ni wabinafsi na wasioitakia mema nchi yetu.
Madai ya wananchi wa Mtwara yanatokana na uzoefu waliokuwa nao katika maeneo yote ambapo pana miradi ya kimaenedeleo itokanayo na maliasili ya nchi, maeneo hayo yamekuwa masikini na watu wachache wamekuwa wanatajirika, walichotaka kufahamu wananchi watanufaikaje na uwepo wa gesi katika maeneo yao kabla ya kuinufaisha nchi mzima kwa kuwa wao ndiyo watakuwa wa kwanza kuathirika ikiwa patatokea hitilafu yoyote itokanayo na uchimbwaji wa gesi hiyo.
Leo tunaweza kujifunza kutokana na uchimbaji wa Dhahabu Geita (GGM), uchimbaji wa Almasi Mwadui Shinyanga, Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Nyamongo na maeneo mengine mengi, nini hali ya maisha ya wananchi wa maeneo hayo.
Pamoja na upotoshwaji wa makusudi uliofanywa na unaoendelea kufanywa na watendaji wa serikali juu ya suala la gesi ya Mtwara, inashangaza hata Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambalo lilionekana awali kutenda haki kwa wananchi wa Mtwara baada ya wananchi kukosa imani dhidi ya Polisi kutokana na wizi na uporaji wa mali za wananchi huku wakichoma moto baadhi ya maduka kwa lengo la kuhalalisha vitendo vya hujuma pamoja na kuchoma moto soko la Nkana Read, Jeshi lililojijengea heshima kwa jamii nalo limeanza kuingia mkumbo wa kuwatesa raia bila makosa.
Mwanzoni mwa wiki hii Mkurugenzi wetu wa siasa wa wilaya ya Mtwara Mjini Mhe. Saibogi ambaye pia ni mwenyekiti wetu wa serikali ya Mtaa alitekwa na wanajeshi na kumpeleka katika Kambi yao iliyopo barabara ya kwenda Nanyamba ambapo walimvua nguo na kumpiga mijeredi usiku kucha bila hatia na kumuachia asubuhi yake huku wakiahidi kuwakamata viongozi wengine wa CUF ili kutoa funzo kwa wale wanaopigania haki za wananchi.
Matukio ya namna hii si ya kuyafumbia macho na yanatengeneza serikali yenye kiburi isiyotokana na maamuzi ya raia. Maisha ya namna hii hayawezi kuendeshwa katika nchi inayojiita huru kama yakwetu na badala yake mambo haya yanatukumbusha enzi za utawala wa kikoloni ambpo CUF kamwe hatupo tayari kuruhusu vitendo vya kishenzi kuona vinafanyika nchini petu.
Tulikianzisha Chama hiki kwa madhumuni ya kuwaunganisha watanzania wote popote walipo, bila kujali itikadi zao, waweze kukataa aina yoyote ya uonevu, ukandamizaji, unyanyasaji, ubaguzi na udhalilishaji wa kisiasa au kiuchumi.
Aidha tuna dhamira ya kulinda, kutekeleza na kuzienzi haki za Binadamu pamoja na kuinua uchumi wa nchi kwa siasa zitumikie uchumi badala ya uchumi kutumikia siasa kama inavyofanyika hivi sasa. CUF tunaamini katika siasa za ustaharabu ambazo zitatuwezesha kuwa na jamii salama yenye mshikamano na ushirikiano katika kuijenga nchi yetu, lakini wenzetu wanatumia upole wetu na ustaharabu wetu kutufanyia vitendo vinavyokiuka utu wa mtu na hatimaye kila aliyepewa mamlaka ya kuongoza sehemu ya nchi yetu anageuka kuwa mfalme na kuamrisha kamata Yule, mpe kesi Yule na mwache Yule. Uvumilivu wetu usiwe mtaji kwa CCM na serikali yake kutufanya watakalo, nasi ni binadamu.
Waheshimiwa waandishi wa habari, maandamano yetu yanalenga pia kuitaka serikali kuwasikiliza wananchi wa Mtwara kwa kukaa nao chini, kujua hoja zao na kutoa ufafanuzi pale patakapobidi, sisi tunaamini wanazo hoja za msingi na wakisikilizwa serikali itaona namna ya kuzifanyia kazi hoja hizo badala ya kukurupuka na kutoa kauli za kibabe eti hawa wanachochewa na vyama vya siasa au pana watu wasioitakia mema nchi ndiyo wanachochea, kauli hizi zinajenga chuki na zanakosa uzalendo wa taifa. Haiwezekani hao wanaojiita ndiyo wazalendo halisi wawe wanaifidi nchi alafu tuendelee kukaa kimya kama vile wananchi wa kusini ni watu wasioweza kufikiri na kupambanua baya na zuri.
Wakati wananchi hawa walipopeleka maombi yao kupitia kwa Mhe. Mohamedi Habibu Mnyaa Mbunge wa Mkanyageni, ilikuwa nafasi nzuri kwa serikali kuweza kusikiliza maombi yao na kutoa maamuzi, badala yake siasa zikatumika, maombi yakakataliwa leo Bunge linaunda kamati ya uchunguzi iende mtwara wakachunguze nini ikiwa tayari hoja zao zilikataliwa?
Ieleweke kuwa nchi yetu itajengwa na watanzania wenyewe kwa kushirikiana na kusikilizana. Amani ya kweli itapatikana ikiwa haki itaonekana kutendeka kwa jamii yote. Waheshimiwa waandishi wa habari, haya ni sehemu tu ya mambo ambayo tunakusidia kumfikishia rais wetu ili aweze kuyafanyia kazi.
Mungu Ibariki CUF, Mungu ibarika Tanzania.
Imetolewa na
Shaweji Mketo,
Naibu Mkurugenzi wa Mipango, Uchaguzi na Siasa,
tarehe 22 Juni 2013

Friday, June 21, 2013

Matusi yachangia Stars kufungwa:Gadi

Simon Mmbando.
Askofu Charles Gadi wa kanisa la Good News for all Minister  amesema kuwa lugha ya udhalilishaji na matusi vilichangia kufungwa kwa timu ya Taifa Stars.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo alisema ziposababu nyingi zilizo sababisha Taifa Stara kupoteza mchezo wake dhidi ya Ivory coast uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Askofu Gadi alisema sababu kubwa iliyopelekea Taifa Stara kupoteza mchezo wake ni Mizaha mingi ya washangiliaji na matusi yaliyokithiri ambayo mbele za Mungu huonekana kama sio maombi.

Unapo tukana Mungu husika kama vile akusikiapo unavyo omba hvyo sisi sote kama Watanzania tulimwamini Mungu na tukiamini tutapata ushindi. Ni jambo la ajabu kuona watu wanaomba msaada wa Mungu na wengine wanatukana matusi.

Hali hiyo hukinzana na Mungu na mwisho wake kushindwa kama hali hiyo ya matusi ikipitiliza ushindi kwetu itakuwa ni ndoto.

Aliendelea kusema kuwa goli la kwanza lilifungwa kwa maombi ya Watanzania waliokuwa pale na walio kuwa majumbani kwao wakiomba, lakini matusi yalio endelea ya kutukana maumbile ya siri ya Mama zetu,Wake zetu, Wakwe zetu, Dada zetu na Watoto wetu wa kike yalitukwamisha.

Matusi hayo yalikwamisha ushindi kwa Taifa Stara kwani unapo tukana maumbile ya akina mama ni sawa na kuchafua na kukejeli uumbaji wa Mungu kwa akina mama na hali hiyo hupelekea laana na hali ya kushindwa.

Alisema cha ajaba hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na imefikia wakati tuziombe mamlaka usika hasaBunge na Wabunge na akina mama wasiyafumbie macho mambo hayo bali watunge sheria zenye kutoa adhabu kali kwa watu wenye mazoea ya kutamka matusi.

Kama zilivyo nchi nyingine kutema bigijii unaweza kufungwa miezi mitatu kwanini nch yetu unalifumbia macho kosa matusi Mabaya kama hayo au yanaonekana ni situ cha kawaida, utadhani Uwanjani pale palikuwa na kiwanda cha kuzalisha matusi.

Hali hiyo ya matusi inachafua sura nzima ya tasnia ya michezo  na itatufanya tuwe wasindikizaji kwani mambo haya yana athari sana katika ulimwengu wa roho na yasipo tiliwa mkazo kuna uwezekano wakuwa poteza maajenti ambao huja nchini kutafut wachezaji na kuwauza nje ya nchi.

Kuhusu usalama kwa watazamaji alisema uwanja ulijaa kwa kiwango ambacho ni tatizo kama kukitokea jambo la hatari kwani watu walijazana hadi njia za lupita watu, wanaishauri serikali iweke screen kubwa nje ya uwanja ili kwa watakaochelewa
Kuingia uwanjani waangalie mpira lupita nje ya uwanja.

Taifa Star ilicheza mchezo huo dhidi ya Ivory coast Juni,16 mwaka huu na  kupoteza kwa kufungwa magoli 4-2 na kupoteza nafasi yakushiriki kombe la dunia litakalofanyika  nchini Brazil Juni, mwakani.

Mwisho alitoa pongezi kwa Wachezaji, Serikali,Wananchi, TFF na kamati (Saidia Taifa Star Ishinde) kwajitahada walizofanya katika maandalizi ya timu yetu, pia wakazi wote wa Dar es Salaam na wote waliofika uwanjani kwani walionyesha uzalendo wa kuipenda nchi yao.

Thursday, June 13, 2013

SIMBA YAPANGA KUMUUZA AMRI KIEMBA WYDAD CASABLANCA YA MOROCCO BAADA YA KUMSAINISHA MKATABA MPYA

               Siku moja baada ya Simba kumwongezea mkataba Amri Kiemba, klabu hiyo ya Msimbazi inatarajia kumpiga bei kiungo huyo mwenye kiwango kilichosimama kwenye mstari kwa timu ya Wydad Ac Casablanca ya Morocco.

Mpango wa kumuuza Kiemba umekuja baada ya mashushushu wa timu hiyo ya Morocco kuridhishwa na kiwango alichoonyesha wakati akiichezea Taifa Stars dhidi ya Morocco katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwakani.
Katika mchezo huo, Stars ilifungwa mabao 2-1, huku Kiemba akifunga bao nzuri la kufutia machozi kwa kiki ya mwendo mrefu nje ya boksi la hatari.
Zakaria Hanspope, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, amelithibitishia gazeti la Mwananchi jana kuwa, mazungumzo ya awali ya kuuzwa kwa kiungo huyo aliyewahi kucheza Yanga yako hatua za mwisho kukamilika.
“Ni kweli, mazungumzo ya awali yameshafanyika kati ya Simba na uongozi wa Wydad Ac Casablanca, leo tunamalizia tulipofikia,” alisema Hanspope.
“Niko Morocco kufanya mazungumzo ya mwisho na uongozi wa Wydad Casablanca, natumaini tutafikia mahala pazuri Mungu akijalia,” alisema Hanspope.
Mmoja wa vigogo wa Kundi la Friends of Simba ndiyo aliyeushtua uongozi juu ya mpango huo, ambao nao waliharakisha kumsainisha mkataba mpya kabla ya kumuuza. Juzi, Simba ilimsainisha Kiemba mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh35 mil.

MSANII WA HIP HOP LANGA AFARIKI DUNIA

Msanii wa muziki wa kizazi Langa Kileo amefariki dunia jioni ya leo katika hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua ugonjwa wa Malaria.

Langa ambaye aliingia rasmi kwenye muziki baada ya kuwa mmoja ya washindi Coca Cola Pop Star, ambapo aliunda kundi la WAKILISHA kwa pamoja na Shaa pamoja na Witness. Walifanikiwa kutoa nyimbo kadhaa ambazo zilitamba sana kwenye vituo vya Radio na Television.

HOTUBA YA MATUMIZI YA BAJETI YA SERIKALI YA ZANZIBAR MWAKA 2013-2014

  • Written by  Ajuaye Mcha

untitled 58b01

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee akielekea katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kuwasilisha Hotuba ya matumizi ya Bajeti ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2013-2014.mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.

untitled2 e5db1
Baadhi ya Makatibu wa kuu wa wizara za Serikali wakiwa katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia hotuba ya matumizi ya Bajeti ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2013-2014.iliowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
untitled3 500ce
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali wakifuatilia hotuba ya matumizi ya Bajeti ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2013-2014.iliowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee mbweni nje ya Mji wa Zanzibar

Tuesday, June 11, 2013

Hali ya Mandela inasemekana kuwa tete

Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, angali katika hali mbaya ingawa imeweza kudhibitiwa. Mandela amelazwa katika hospitali moja mjini Pretoria.
"mzee Mandela yuko hospitalini na hali yake bado haijabadilika.''
Maombi yakekuwa yakifanywa makanisani kote nchini Afrika Kusini kumuombea Mandela ambaye anatibiwa kwa ugonjwa wa mapafu.
Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 94, alipelekwa hospitalini mapema Jumamosi , ikiwa ni mara ya tatu kulazwa hospitalini mwaka huu.
Kwa mujibu wa duru za urais, Mandela amekuwa akiugua kwa muda mjini Johannesburg baada ya kukumbwa tena na ugonjwa wa mapafu.
Alilazwa hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi mnamo Jumamosi.
Kwa mujibu wa taarifa za urais, Rais President Jacob Zuma, amerejelea wito wake kwa watu nchini Afrika Kusini kumuombea Madiba wakati huu anapougua.
Lakini mwandishi wa BBC mjini Pretoria, Karen Allen, anasema kuwa kuna matumaini amdogo kuwa Mandela aliyeongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, huenda kupona.
Anasema kuwa wengi walipata matumani baada ya bintiye Mandela Zindzi, kusema kuwa babake yuko salama na kuwa anaendelea kupata nafuu.
Mkewe Mandela Graca Machel, alifutilia mbali, ziara yake mjini London Jumamosi ili kuwa kando ya mumewe.
Mandela alikuwa Rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 hadi 1999.
Alifungwa jela miaka 27 na anaaminika kuwahi kuugua ugonjwa wa mapafu alipokuwa akifanyishwa kazi ngumu katika machimbo ya mawe akiwa jela

Lwakatare aachiwa kwa dhamana Kisutu

Mkurugenzi wa Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema),  Wilfred Lwakatare 

Posted  Jumanne,Juni11  2013  saa 11:10 AM
Kwa ufupi
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam  imekubali kumwachia Mkurugenzi wa Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema),  Wilfred Lwakatare kwa dhamana ya Sh10Milioni.
Kwa habari zaidi ungana nami baadaye

Monday, June 10, 2013

"Ningekuwa Ruge, Ningemwomba Radhi Jaydee"Asema Sebo

Mtangazaji wa kipindi cha Sun Downer cha Magic FM, Sebo amesema kwamba shangwe zilizolipuka mara baada ya Jaydee kutajwa kuwa miongoni mwa wanaowania tuzo ya msanii bora wa kike ktk tuzo za KTMA, ni ishara ya mwanadada huyo kukubalika ktk jamii. Mtangazaji huyo amesema kwamba Jaydee ni mwanamke mwenye uthubutu ktk harakati za kuyasaka maisha na kwamba yeyote mwenye nia ya kukwamisha jitihada zake aibu na iwe juu yake. Ameongeza kuwa kukubalika kwa mwanadada huyu pia kulidhihirika pale ambapo watazamaji ktk tukio hilo walipomshinikiza Meneja wa msanii huyo (Gadna) kutaja kiingilio na tarehe ya maadhimisho ya miaka 13 ya Jaydee ktk uga wa muziki. Hivyo, Sebo anaona ni vyema Ruge akajishusha na kumaliza tofauti zake dhidi ya Jaydee.

Monday, June 10, MARA BAADA YA TAIFA STARS KUREJEA-POULSEN ANENA NA KUSEMA WANGEKUWA WANGECHEZA 11 UWANJANI WASINGEFUNGWA NA,MOROCCO

Kocha wa Timu bali matokeo ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amesema refa wa mechi ya Taifa Stars na Morocco iliyopigwa Marrakech Jumamosi kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la  Dunia Brazil mwakani aliuwa mchezo kwa kutoa kadi nyekundu kwa mchezaji Aggrey Morris.
Akitoa maoni ya mchezo huo, Poulsen alisema alisikitishwa na jinsi refa huyo alitoa adhabu kali ambayo haiendani na kanuni za FIFA.
Aggrey Morris alioneshwa kadi nyekundu baada ya kugongana na Abderazak Hemed Allah ambaye aliifungia Morocco bao la kwanza katika dakika ya 37.
“Hakuwa na sababu ya kumuonesha Morris kadi nyekundu kwani tayari alishawapa Morocco penalti, alisema Poulsen huku akiongeza, “FIFA imeshawaonya marefa mara kadhaa dhidi ya kuua mchezo kwa namna hii ya kutoa adhabu kali kupita kiasi.”
Poulsen alisifu wachezaji wake na kusema licha ya kucheza pungufu walipambana uwanjani na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa Amri Kiemba. Morocco walishinda kwa 2-1.
“Kama tungecheza kumi na moja hadi mwisho nina uhakika tungeshinda mechi hii lakini refa aliiua mechi na huwezi kufanya hivi katika mechi ngumu kama hii,” alisema Poulsen.
Kocha huyo alisema kupata goli la ugenini unapochez na timu ngumu kama Morocco ni jambo la kujivunia hasa mnapokuwa pungufu uwanjani.
Alisisitiza kuwa sasa wanaelekeza nguvu zote katika mechi shidi ya Ivory Coast Jumapili ijayo. “Mambo ya Morocco yamekwisha sasa tunafikiria namna ya kushinda mechi ya Jumapili.
Tanzania iko katika kundi C inayoongozwa na Ivory Coast yenye pointi 10, Tanzania 6, Morocco 5 na Gambia 1.
Taifa Stars imerejea Jumatatu alfajiri kutokea Marrakech Morocco na itaendelea na kambi ya wiki moja ili kujiandaa na mechi dhidi ya Ivory Coast.
Nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja alisema wachezaji walicheza kwa ari kubwa na walifurahishwa na jinsi watanzania walijitokeza kwa wingi.
“Tulipata faraja kubwa sana kuwaona watanzania wengi uwanjani…mambo ya Morocco yameisha sasa tuangalie Ivory Coast,” alisema.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe ambaye bia yake inadhamini Taifa Stars, alisema wacezaji walijitahidi hasa ikizingatiwa walicheza pungufu na hata wakafanikiwa kufunga bao moja.
“Katika hali kawaida, wachezaji wengine wangekata tamaa lakini bao hili moja linaonesha kuwa wachezaji walikuwa na ari ya kupata ushindi,” alisema Bw Kavishe.
Alisema wao kama wadhamini wana imani kubwa na Taifa Stars na kwamba wanaamini hii ni safari ya mafanikio ambayo ilianza mwaka mmoja uliopita tangu Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ianze udhamini huo.

Chadema yakubali Serikali tatu

Mbeya/Dar. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman ameweka bayana kuwa wanaunga mkono Rasimu ya Katiba na hasa suala la Muungano wa Tanzania kuundwa na Serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
 
Mwenyekiti wa Chadema, FreemanMbowe
Amesema mambo mengi yaliyopendekezwa na chama chake yamefanyiwa kazi na Tume ya Mabadiliko na kuishangaa CCM akidai kwamba inapinga rasimu hiyo hususan suala la Serikali tatu wakati kimsingi watu wa Tanzania Bara wamekuwa wakipunjika kwenye muundo wa sasa wa Muungano.
 
Akihutubia mkutano wa kampeni ya kuwania udiwani wa Kata ya Iyela katika Uwanja wa Bongonela, Mbeya jana jioni, Mbowe alisema chama chake kinataka kuona Serikali ya Tanganyika ikifufuliwa. Alikuwa akimnadi mgombea wa Chadema, Charles Mkela.
 
Alisema Chadema kinataka kuona Wazanzibari wakiwa na Serikali yao ili wajiamulie mambo yao na pia Watanganyika wawe na uongozi wao lakini waunganishwe na Serikali ya Muungano.
 
Alisema muundo wa sasa wa Muungano una matatizo. Kwa mfano, mbunge wa Zanzibar anawakilisha watu wachache zaidi ukilinganisha na mbunge wa Bara. Wananchi mtashangaa sote tunalipwa sawa.”
 
“Ila zikija Serikali tatu ina maana kuwa kila upande wa Muungano utatumia rasilimali zake. Haya mambo kulipana fedha nyingi kwa kazi kidogo yatakoma.”

Saturday, June 8, 2013

Kunauwezekano wa kugawanywa ikulu ya rais:Warioba

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania, Jaji Joseph Warioba amesema iwapo Mfumo wa Serikali Tatu utaridhiwa na wananchi ni lazima mambo yaliyo ndani ya Muungano yatagawanywa ikiwa ni pamoja na Ikulu ya Rais. Amesema kutokana na taifa kufanya mabadiliko ya Katiba ni lazima kuwepo mpangilio wa kugawana mambo mbalimbali yaliyokuwa chini ya Muungano ikiwamo majengo, wafanyakazi, Ikulu, hata vitendea kazi na kwamba utaratibu huo ni kama ule uliotumika wakati Tanganyika na Zanzibar zilipoungana. Kauli ya hiyo ya Jaji Warioba imekuja siku tatu tangu Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kueleza kuwa Tanzania Bara itaanza mchakato wa kutunga Katiba yake Aprili mwaka 2014 na kumalizika Desemba mwaka huohuo. Jaji Warioba aliyasema hayo katika mahojiano maalumu na waandishi wandamizi wa habari jijini Dar es salamu, Tanzania. Hata hivyo aliongeza kuwa suala hilo linahitajia mazungumzo ya pande zote mbili, baada ya kukamilika kwa mchakato huu kwa sababu hii ni rasimu tu, ambayo itajadiliwa na wananchi kabla ya kuanza kwa Bunge la Katiba na baadaye kuwepo kwa kura ya maoni.

Cesc Fabregas azigombanisha Man United na Arsenal.

Klabu za Manchester United na Arsenal zimeingia kwenye vitakali ya kuwania saini ya kiungo wa kimataifa wa Hispania Cesc Fabregas anawaniwa na klabu za Manchester United na Arsenal baada ya klabu yake ya Fc Barcelona kudaiwa kuwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili yake .
Fabregas ambaye alicheza nchini England kwenye klabu ya Arsenal kwa muda wa miaka nane ameshindwa kufikia kiwango kilichotarajiwa na Barcelona wakati inamnunua toka Arsenal na kwa sasa iko tayari kumuuza ili kutengeneza fedha za kununua mchezaji mwingine .
Kocha mpya wa Manchester United David Moyes amegundua kuwa United ina tatizo kwenye safu ya kiungo na yuko tayari kuidhinisha paundi milioni 40 kumnunua Cesc , hata hivyo Arsenal ndio wenye haki ya kwanza ya kuzungumza na kiungo huyo kwa mujibu wa makubaliano baina ya Barca na Arsenal wakati wa mauzo yake toka London kwenda Hispania na endapo watakuwa tayari kumnunua basi Unitd wanaweza kupoteza nafasi ya kumsajili.
Kwa upande mwingine kocha wa Arsenal Arsene Wenger hapo jana alianza rasmi mchakato wa usajili kwenye kikosi chake baada ya kutuma ofa ya paundi milioni 22 kwa ajili ya kiungo wa Everton Marouanne Fellaini .
United nao wanajiandaa kumthibitisha beki wa timu ya taifa ya Uruguay kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 na klabu ya Penarol Guillermo Varela ambaye alithibitisha mwenyewe kufanyiwa vipimo vya afya huko Manchester.

ASILIMIA 15 YA MAPATO YA SHOW YANGU YA "THE FINEST" NITATOA KWA MAMA WA MAREHEMU NGWEA:MWANA FA

FA: ASILIMIA 15 YA MAPATO YA SHOW YANGU YA "THE FINEST" NITATOA KWA MAMA WA MAREHEMU MANGWEA.

Baada ya show ya Mwana FA "The Finest" Kuahirishwa wiki iliyopita kutokana na msina wa Rapper Abert Mangwea, aliyefariki jumanne ya tarehe 28 May na kuzikwa siku ya jana Morogoro,
Kama Zamani The Finest,Imetangazwa tena, na safari hii asilimia 15 ya mapato kutoka katika show hiyo, yatapelekwa kwa mama mzazi wa Ngwea.

"nimesema kwamba nitoe hela mfukoni kwangu moja kwa moja, niipeleke huku, kwahiyo chochote nitakacho kipata, nataka kutoa 15 percent nimpelekee bi mkubwa...."amesema Fa

"unajua kitu kama cha kumuita ngwea marehem,  bado kilikuwa hakija click kichwani kwangu, hakiji, yaani watu wakimuitwa mangwea marehem naona aaaah, hawa jamaa wanasema vitu gani, bado inanisumbua "

" Nafkiri Pengine sikufanya vyakutosha wakati yuko hai, lakini bado naweza kufanya kitu kama anaona huko aliko naomba awe na moyo mwepesi na mimi, nimeona ntamuandali hiki ambacho nakipata sasa hivi, nimuangalie mama yake, kama ambavyo pengine yeye angefanya kama ingekua album yakwake.amesema mwana FA.

POULSEN AHAIDI SOKA LA KASI KATIKA MECHI DHIDI YA MOROCCO NAYE KASEJA ASEMA HAWAIOGOPI MOROCCO ILA WANAIHESHIMU

Marrkech, Morocco
Huku Timu ya Taifa Taifa Stars ikikabiliwa na mechi muhimu kesho (Jumamosi) dhidi ya Morocco kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia, Kocha Kim Poulsen amesema amejiandaa kucheza mpira wa kasi na wenye pasi za uhakika ili kuivuruga beki ya Morocco.
Kocha huyo ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa ni muhimu kuhakikisha Morocco hawaupati mpira kwa urahisi.
“Wachezaji wako katika hali nzuri kabisa na wana ari ya kushinda mechi hii…tuna nguvu na tunajua namna ya kuwapiga Morocco,” alisema kocha huyo.
Alisema suala si mchezaji gani anaanza au washambulizi ni wangapi, bali ni kazi itakayofanyika uwanjani na ubora wa wachezaji wa Taifa Stars, inayofurahia udhamnini mnono wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Alisema Morocco ni timu kubwa na ina wachezaji wengi wa kulipwa lakini inafungika na Taifa Stars itaweka nguvu kuanzia mwanzo wa mechi.
“Unapocheza mechi kama hii inabidi uweke nguvu dakika za kwanza za mechi ili umpe mpinzani wakati mgumu kwa hivyo dakika za mwanzo zitakuwa muhimu sana katika mechi hii,” alisema.
Poulsen alisema baadhi ya watu nchini Morocco bado wanaamini kuwa ushindi wa mechi ya awali Jijini Dar es Salaam wa 3-1 dhidi ya Morocco ulikuwa wa kibahati tu. “Tunataka kuwadhihirishia kuwa tunaweza na Taifa Stars sio timu ndogo kama wanayodhani.”
Alisema mazingira ya kambi ni mazuri kabisa na wachezaji wote wako katika hali nzuri na tayari kwa mchezo huu.
“Katika hali ya kawaida ungetegemea hujuma nyingi ikiwemo hoteli mbovu, viwanja vibovu vya mazoezi na kadhalika lakini hapa ni tofauti kabisa…kwani mazingira ni mazuri,” alisema Poulsen.
Taifa Stars imeweka kambi katika Hoteli ya Pullman iliyoko nje kidogo ya Mji wa Marrakech.
Naye nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja alisema wamefanya mazoezi ya kutosha hasa ikizingatiwa kambi ilianzia Addis Ababa, Ethiopia ambako walicheza mechi ya kirafiki na Sudan na kutoa sare ya 0-0 kabla ya kuelekea Marrakech.
“Morocco ni timu kubwa, tunapaswa kuiheshimu lakini sio kuiogopa…tutapambana ili timu ipate matokeo,” alisema Kaseja.
Naye Meneja wa Bia ya Kilimanajro Premium Lager, George Kavishe, akizungumza kutoka Dar es Salaam alisema wao kama wadhamini wa Taifa Stars wana imani kubwa sana na Stars na wanaitaka iwape Watanzania raha kwa mara nyingine kwa kushinda mechi hiyo.
“Tumewaona wakifanya vizuri nyumbani kwa kushinda mechi tano mfululizo na sasa ni muda wa kupata ushindi nje,” alisema.
Stars iko katika kundi C pamoja na Ivory Coast, Morocco na Gambia. Kundi hilo linaongozwa na Ivory Coast yenye pointi 7, Tanzania 6, Morocco 2 na Gambia 1.
Mechi ya kesho itapigwa katika Uwanja wa Marrakech saa tatu usiku kwa saa za Morocco ambayo itakuwa saa tano kamili Tanzania.
Baada ya Morocco Stars itacheza na Ivory Coast nyumbani Jumapili ijayo na mechi ya mwisho itakuwa dhidi ya Gambia Septemba mwaka huu.

Thursday, June 6, 2013

TANZANIA YAPAA VIWANGO VYA UBORA VINAVYOTOLEWA NA FIFA

USHINDI wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars waliopata katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Morocco umesaidia kuipandisha nchi katika viwango vya ubora wa soka duniani.

Katika orodha hizo za kila mwezi zilizotolewa leo Tanzania imekwea kwa nafasi tatu kutoka nafasi ya 119 waliyokuwepo mwezi uliopita mpaka nafasi ya 116 hivyo kuendelea kufanya vyema ukilinganisha na mwaka jana. 

Mabingwa wa Dunia na Ulaya, Hispania wameendelea kung’ang’ania kileleni mwa orodha hizo wakifuatiwa na Ujerumani katika nafasi ya pili na Argentina katika nafasi ya tatu huku kwenye nafasi ya nne kukiwa na ingizo jipya la nchi ya Croatia waliopanda wa nafasi tano mpaka kufikia ya nne na tano bora inafungwa na Ureno.

Kwa upande wa Afrika, Ivory Coast wameendelea kushika nafasi ya kwanza baada ya kupanda kwa nafasi moja duniani mpaka nafasi ya 12 wakifuatiwa na Ghana katika nafasi ya pili ambao wao wamedondoka kwa nafasi mbili mpaka ya 22 duniani. Mali wao wako nafasi ya tatu wakifuatiwa na mabingwa soka barani Afrika Nigeria katika nafasi ya nne na tano bora Algeria.inafungwa na

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, JAJI JOSEPH S. WARIOBA, KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UZINDUZI WA RASIMU YA KATIBA TAREHE 03 JUNI, 2013 KWENYE VIWANJA VYA UKUMBI WA KARIMJEE,
DAR ES SALAAM.

·         Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilali – Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano,
·         Mhe. Mizengo K. P. Pinda (Mb.) - Waziri Mkuu,
·         Mhe. Seif Sharif Hamad – Makamu wa Kwanza wa Rais – Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
·         Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (Mb.) - Makamo wa Pili wa Rais - Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
·         Mhe. Mathias Chikawe – Waziri wa Katiba na Sheria,
·         Mhe. Abubakar Khamis Bakary - Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
·         Mhe. Jaji Frederick M Werema - Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
·         Mhe. Othman Masoud Othuman - Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,
·         Viongozi wa Vyama vya Siasa,
·         Waheshimiwa Wajumbe wa Tume na Wajumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
·         Ndugu Wananchi,
·         Wageni Waalikwa
·         Waandishi wa Habari Mabibi na Mabwana.

1.      UTANGULIZI

Ndugu Wananchi,
Awali ya yote namshukuru mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kufikia hatua hii ya leo ya kuzindua Rasimu ya Katiba. pia, niwashukuru ninyi nyote mliohudhuria halfa hii ikiwa ni mwendelezo wa mchakato muhimu wa Mabadiliko ya Katiba ya nchi yetu.

Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilipitishwa Bungeni Novemba, 2011 na kufanyiwa mabadiliko Februari, 2012. Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliundwa kwa mujibu wa Kifungu 6(1) cha sheria hiyo (Cap.83). Wajumbe 34 wa Tume waliteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, mwezi Aprili, 2012. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Tume imepewa miezi kumi na minane kukamilisha kazi yake kuanzia siku ilipoanza kazi rasmi ambayo ilikuwa Mei 2, 2012.

Tume iliandaa ratiba ya utekelezaji wa majukumu yake. Kufuatana na ratiba hiyo Tume ilijipanga kukusanya maoni ya wananchi katika kipindi cha miezi mitano kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba, 2012. Kazi hiyo ilifanywa kama tulivyopanga. Tume ilijigawa katika makundi na ilitembelea mkoa yote thelathini.

Tume ilifanya mikutano 1,942 ambayo ilihudhuriwa na wananchi wapatao 1,365,337 ambao kati ya hao wananchi 333,537 walitoa maoni ama kwa mazungumzo ya ana kwa ana au kwa maandishi. Tume pia ilipata maoni ya wananchi wengi, wa ndani na nje ya nchi kwa njia mbali mbali kama vile; Mikutano ya hadhara, Fomu maalum za Tume, barua kupitia Masanduku ya Barua ya Tume, Mitandao ya Kijamii ya barua pepe; facebook ya Tume, Tovuti ya Tume; Makala mbalimbali kutoka kwenye magazeti na ujumbe mfupi wa simu.

Tume ilitumia mwezi Januari, 2013 kukusanya maoni ya makundi mbali mbali katika jamii, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa, taasisi za Serikali, taasisi za dini, wakulima, wafugaji, wafanyakazi, asasi za kiraia na kadhalika. Makundi zaidi ya 160 yalikutana na Tume na kutoa maoni. Tume pia ilipata maoni ya viongozi wa juu wa Serikali walioko madarakani na waliostaafu. Kwa jumla viongozi 43walitoa maoni.

Tume ilipanga kutumia miezi mitatu ya Februari, Machi na Aprili kuchambua maoni ya wananchi na kuandaa Rasimu ya Katiba. Lakini tuligundua kwamba maoni tuliyopata yalikuwa mengi sana, na pamoja na matumizi ya teknolojia ya kisasa, tulitambua umuhimu wa kuongeza muda hadi mwisho wa mwezi Mei, Maoni ya wananchi yaligusa mambo yote yanayohusu Katiba na mengi ya maoni hayo yalikinzana. Aidha, baadhi ya maoni yaligusia masuala ya Kisera, Kisheria na Kiutendaji. Tulifanya uchambuzi makini na wa ndani wa maoni hayo na kazi hiyo tumeikamilisha na rasimu imeandaliwa na Tume na leo tupo hapa kwa ajili ya kuizindua, ambapo Wananchi watapata nafasi ya kuisoma. Kwa leo, kwa niaba ya Tume, napenda kutaja maeneo machache tu ambayo tunayapendekeza.

·         IBARA ZINAZOPENDEKEZWA KWENYE RASIMU YA KATIBA

Ndugu Wananchi,
Katiba yetu ya sasa ina ibara 152. Tume ilifanya jitihada kubwa sana kuandaa rasimu ambayo siyo ndefu. Lakini katika hali halisi haikuwezekana. Rasimu ya Katiba tunayopendekeza ina ibara 240.

·         MISINGI MIKUU YA TAIFA

Utangulizi wa Katiba ya sasa ndio unaobeba misingi mikuu ya Taifa ambayo ni Uhuru, Haki, Udugu na Amani. Tume inaamini kwamba misingi hii ni mizito na inastahili kubaki kwenye Katiba mpya. Hata hivyo, Tume imeona ni busara kuongeza misingi mingine mitatu ya Usawa, Umoja na Mshikamano. Hivyo, Tume imependekeza Katiba iwe na Misingi Mikuu saba ya Taifa;yaani; Uhuru, Haki, Udugu, Usawa, Umoja, Amani na Mshikamano.

·         TUNU ZA TAIFA

Katiba yetu ya sasa haina sehemu inayoelezea tunu za Taifa (National Values). Wananchi wengi walitoa maoni kwamba Katiba itaje Tunu za Taifa. Tume imependekeza Tunu zifuatazo zitajwe ndani ya Katiba. Tunu hizo ni;- Utu, Uzalendo, Uadilifu, Umoja, Uwazi, Uwajibikaji na Lugha yetu ya taifa ya Kiswahili.

·         MALENGO YA TAIFA

Tume ilipozunguka nchi nzima wananchi walizungumzia sana kuhusu malengo ya taifa. Walitaka Katiba ionyeshe dira ya taifa. Wananchi wanayo ndoto yao ya Tanzania ya kesho na kesho kutwa. Kwa kuzingatia maoni ya wananchi, kuna sura nzima inayohusu Malengo mahsusi na ya msingi ya mwelekeo wa shughuli za Kiserikali na Sera za Kitaifa. Rasimu ya Katiba inaeleza kuwa Malengo ya Kitaifa yaliyoainishwa ndani ya Rasimu yatakuwa ni Mwongozo kwa Serikali, Bunge, Mahakama, Vyama vya Siasa, Taasisi na Mamlaka nyingine, na kwa kila mwananchi katika matumizi au kutafsiri Masharti ya Katiba au Sheria nyingine za Nchi.
Kwa msingi huo, Tume imependekeza malengo makuu ya taifa yapanuliwe kwa mpangilio wa kuonesha malengo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, kimazingira na sera ya mambo ya nje. Malengo hayo yameingizwa kwenye Rasimu ya Katiba.

·         VYOMBO VYA KIKATIBA

Wananchi walizungumzia suala la kubainishwa kwa vyombo vya Kikatiba na kuingizwa kwenye Katiba ili viwe na nguvu ya Kikatiba katika utekelezaji wa majukumu yao. Tume imependekeza baadhi ya vyombo vifuatavyo viwe vya Kikatiba; Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali, Baraza la Mawaziri, Kamati Maalum ya Makatibu Wakuu na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri; Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa, Tume Huru ya Uchaguzi, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Tume ya Utumishi wa Umma, Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

·         MAADILI YA VIONGOZI NA MIIKO YA UONGOZI

Wananchi wengi pia walizungumzia kwa upana sana kuhusu maadili na miiko ya Viongozi, kwa kuzingatia maoni ya wananchi Tume inapendekeza maadili ya viongozi wa umma, pamoja na miiko ya uongozi yawekwe kwenye Katiba. Tume pia imependekeza kuwa Sekretariati ya Maadili ibadilishwe kuwa Tume yenye mamlaka makubwa ya kusimamia maadili ya viongozi wanaovunja miiko ya uongozi.

·         HAKI ZA BINADAMU

Kuhusu haki za binadamu wananchi walitaka haki hizi ziimarishwe na kusiwe na vikwazo visivyo vya lazima. Tume imependekeza mabadiliko katika baadhi ya haki za binadamu kwa madhumuni ya kuziimarisha. Moja ya mabadiliko hayo ni kuhusu uhuru wa mwananchi kushiriki shughuli za umma. Tume inapendekeza kwamba vikwazo vilivyowekwa kuzuia mgombea huru viondolewe. Kwa maana nyingine Tume inapendekeza mgombea binafsi aruhusiwe.

Tume pia, inapendekeza haki mpya ziingizwe kwenye Katiba ikiwa ni pamoja na haki ya wafanyakazi, , haki ya mtoto, haki za Watu wenye Ulemavu, Haki za Wanawake, Haki za Wazee, Haki za Makundi Madogo katika Jamii, Haki ya Elimu na Kujifunza, Haki ya kupata habari, Haki na uhuru wa habari na vyombo vya habari na kadhalika.

·         URAIA

Wananchi wengi walipendekeza kuwa suala la Uraia libainishwe wazi kwenye Katiba. Tume imependekeza kwa kutaja Raia wa Jamhuri ya Muungano na haki zake.

·         MIKOPO NA DENI LA TAIFA

Ndugu Wananchi,
Wananchi walizungumzia suala la uwepo wa Ukomo wa nchi kukopa na uwepo wa utaratibu wa kulipa Deni la Taifa ili kuilinda Nchi isiwe na deni kubwa. Kwa kuzingatia maoni ya Wananchi, Tume imependekeza kuwa, Serikali itawajibika kutoa taarifa Bungeni kuhusu Mikopo kwa kuainisha kiasi cha deni lililopo, riba yake na matumizi ya fedha za Mikopo na utaratibu wa kulipa Madeni ya Taifa.

·         MFUMO WA UTAWALA

Kuhusu utawala, Tume inapendekeza Tanzania iendelee na mfumo wa Jamhuri kwa maana ya nchi inayoongozwa na Rais Mtendaji ambaye ni Mkuu wa nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.

·         UCHAGUZI WA RAIS
o    Umri wa kugombea Urais

Tume ilipokea maoni yanayokinzana kuhusu umri wa mwananchi kugombea Urais. Baadhi walipendekeza mtu akishakuwa na sifa ya kupiga kura awe pia na sifa ya kugombea Urais. Umri wa mtu kuruhusiwa kupiga kura ni miaka 18. Wengine walipendekeza umri uliopo kwenye Katiba wa mtu kugombea Urais, yaani kuanzia miaka 40 na kuendelea, uendelee kubaki kama ulivyo.

Wengine walisema Umri wa mtu kuruhusiwa kugombea Urais uwe miaka 35 au miaka 50 na kuendelea.

Tume imeyachambua maoni yote hayo, ikafanya utafiti kwa kupitia Katiba za Nchi zingine na uhalisia wa watu wanaogombea na kuchaguliwa kuwa Marais katika Nchi mbalimbali Duniani ambazo zingine zimeruhusu wagombea wa nafasi ya Urais kuwa na umri chini ya miaka 40.

Wengi walioomba kugombea nafasi hiyo walikuwa na umri wa miaka 40 au zaidi.

Kwa kuzingatia maoni ya wananchi, utafiti na hali halisi, Tume inapendekeza Rais aendelea kuchaguliwa na wananchi na pamoja na sifa nyingine, mtu anayeomba urais asiwe chini ya miaka 40.

Uchaguzi wa Rais itakuwa kama ilivyo sasa, yaani mgombea Urais atakuwa na mgombea mwenza kwa utaratibu kama ilivyo sasa. Isipokuwa, Tume imependekeza Mgombea Urais anaweza kupendekezwa na Chama cha Siasa au kuwa Mgombea Huru.

Mgombea wa nafasi ya Rais atatangazwa kuwa mshindi iwapo atakuwa amepata kura zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote zilizopigwa.

Hata hivyo, matokeo ya uchaguzi wa Rais yanaweza kulalamikiwa Mahakamani, lakini siyo kila mtu anaweza kufungua kesi. Wanaoweza kufungua kesi ni wagombea Urais. Aidha, ni Mahakama ya Juu pekee ndiyo itakuwa na Mamlaka na uwezo wa kusikiliza malalamiko kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais na shauri lazima liamuliwe ndani ya mwezi mmoja, yaani siku therathini.

Rais aliyeshinda ataapishwa siku thelathini tangu alipotangazwa kuwa mshindi au kuthibitishwa na Mahakama.

·         MADARAKA YA RAIS

Ndugu Wananchi,
Tume inapendekeza kwamba, Rais abaki na madaraka ya uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu. Hata hivyo inapendekezwa Rais ashirikiane na taasisi na vyombo vingine katika uteuzi. Kwa mfano:

Uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri, Rais atateua na Bunge litathibitisha.

Kuhusu Jaji Mkuu na Naibu Jaji Mkuu Rais atawateua kutokana na majina ya watu waliopendekezwa na Tume ya Uutumishi wa Mahakama na baada ya hapo Bunge litathibitisha.

Kuhusu Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama inapendekezwa kianzishwe chombo kipya kitakachoitwa Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa, ambalo kati ya majukumu yake itakuwa ni kumshauri Rais kuhusu uteuzi wa Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Kuhusu Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu watateuliwa na Rais kutokana na mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma.

·         KINGA YA RAIS

Tume baada ya kupitia maoni ya Wananchi, inapendekeza Rais abaki na kinga kama ilivyo sasa na anaweza kushitakiwa na Bunge kama ilivyo Katiba ya sasa.

·         IDADI YA MAWAZIRI

Inapendekezwa Rais aunde Serikali ndogo iliyo na Mawaziri wasiozidi kumi na tano na mawaziri hao wasiwe wabunge. Mawaziri hawatahudhuria vikao vya Bunge isipokuwa kama watahitajika kutoa ufafanuzi kwenye kamati za Bunge.

·         BUNGE

Ndugu Wananchi,
Kuhusu Bunge kutakuwa na wabunge wa aina mbili. Kutakuwa na Wabunge wa kuchaguliwa na wabunge watano wa kuteuliwa na Rais kuwakilisha Watu wenye Ulemavu.

Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili mmoja mwanamke na mwingine mwanamume.

Tume inapendekeza kwamba, Mbunge akifukuzwa na Chama cha Siasa abaki kuwa Mbunge lakini akihama Chama atapoteza Ubunge wake.

Inapendekezwa ukomo wa Ubunge uwe vipindi vitatu vya miaka mitano mitano. Hata hivyo, wananchi wanaweza kumwondoa mbunge wao kabla ya mwisho wa kipindi chake.

Inapendekezwa pia kusiwepo na uchaguzi mdogo isipokuwa kama nafasi inayokuwa wazi inatokana na Mbunge huru ndipo utafanyika uchaguzi mdogo kujaza nafasi hiyo, lakini kama nafasi ikiwa wazi kutokana na Mbunge wa Chama cha Siasa basi nafasi hiyo, ijazwe na mtu kutoka Chama hicho.

Inapendekezwa Spika na Naibu Spika wasitokane na Wabunge na wasiwe Viongozi wa vyama vya Siasa.

·         TUME YA UCHAGUZI

Tume imefanya uchambuzi wa maoni ya wananchi kuhusu Tume ya Uchaguzi. Tume inapendekeza jina la tume liwe Tume Huru ya Uchaguzi. Tume pia inapendekeza sifa za wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ziwekwe kwenye Katiba. Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi watapatikana kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizoainishwa ndani ya Katiba kwa kuomba. Majina ya waombaji yatachambuliwa na Kamati ya Uteuzi ambayo Mwenyekiti wake atakuwa Jaji Mkuu na wajumbe wengine sita ambao ni Majaji Wakuu wa nchi Washirika, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Maspika wa Mabunge wa nchi Washirika na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu.

Kamati ya uteuzi itapendekeza majina ya watu wanaofaa kwa Rais ambaye atateua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wengine. Bunge litathibitisha uteuzi wao. Wabunge na viongozi wa aina hiyo hawatakuwa na sifa za kuwa wajumbe wa tume ya uchaguzi.

Inapendekezwa Tume huru ya Uchaguzi isimamie masuala ya uchaguzi, kura ya maoni na Usajili wa Vyama vya Siasa.

·         MAHAKAMA

Kuhusu Mahakama inapendekezwa kuanzishwa kwa Mahakama ya Juu (Supreme Court) Majaji wa Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani watateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

·         MUUNDO WA MUUNGANO

Ndugu Wananchi,
Suala la muundo wa Muungano ndilo lililokuwa gumu kuliko masuala yote. Tume ilitumia muda mwingi kuchambua maoni ya wananchi. Pamoja na kwamba hadidu za rejea zilielekeza Tume kuzingatia uwepo wa Muungano, baadhi ya wananchi walitoa maoni kwamba Muungano uvunjwe na Tume iliyapokea maoni hayo. Licha ya kwamba waliotaka kuvunjwa muungano walikuwa wachache sana, Tume ilichambua sababu walizotoa na kuridhika kwamba hazikuwa na uzito.

Wananchi walio wengi walitaka Muungano uendelee. Kati yao wapo waliopendekeza Muungano wa Serikali moja, Serikali mbili, Serikali tatu, Serikali nne na muungano wa mkataba. Sababu za wale waliopendekeza Serikali nne hazikuwa na uzito, kwa hiyo Tume ikaamua kutopendekeza muundo huo.

Wananchi waliopendekeza Serikali moja walikuwa wachache lakini sababu zao zilkuwa na uzito. Hata hivyo, Tume kwa kuzingatia hali halisi iliona ni changamoto kubwa kuwa na Muungano wa Serikali Moja.

Wananchi waliopendekeza Muungano wa Mkataba walikuwa wengi (hasa wananchi wa Zanzibar) na sababu zao zilikuwa na uzito. Lakini uchambuzi wa Tume ilionekana wazi kwamba ili kupata mkataba lazima kwanza kuwe na nchi mbili huru kabisa lakini hakukuwa na mazingira ya uhakika ya kupata mkataba wa muungano. Tume iliona kuna changamoto ya muungano kuvunjika ingawa waliotoa maoni walisisitiza muungano ubaki. Hivyo, Tume iliamua kutopendekeza muundo huo.

Wananchi waliopendekeza Tanzania iendelee na Muundo wa sasa wa Serikali mbili walikuwa wengi na sababu zao zilikuwa nzito. Hata hivyo, wananchi katika kundi hili walipendekeza mabadiliko mengi na makubwa. Tathmini ya Tume ilionyesha kwamba isingewezekana kufanya mabadiliko yote yaliyopendekezwa.

Wananchi waliopendekeza muundo wa Serikali tatu walikuwa wengi kuliko makundi yote. Sababu zao zilikuwa nzito lakini pia kulikuwa na changamoto nyingi na nzito. Pamoja na maoni ya wananchi Tume ilirejea sababu za kupendekeza muundo huu zilizotolewa na Tume zilizopita na Tafiti zilizofanywa na Tume kuhusu aina mbalimbali za Muungano. Baada ya yote hayo Tume ilifikia uamuzi wa kupendekeza mfumo wa Serikali tatu. Yaani Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

·         ORODHA YA MAMBO YA MUUNGANO

Ndugu Wananchi,
Tume imependekeza katika Rasimu ya Katiba kuwa orodha ya Mambo ya Muungano yawe 7 badala ya 22 yaliyopo sasa.
Mambo ya muungano yanayopendekwa ni:
1.      Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2.      Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
3.      Uraia na Uhamiaji
4.      Sarafu na Benki Kuu
5.      Mambo ya Nje
6.      Usajili wa Vyama vya Siasa
7.      Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya Kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano.

·         BENKI KUU

Kwa kuwa Tume imependekeza Muungano wa Shirikisho kutokana na uzito wa maoni ya wananchi. Hivyokutakuwa na Benki Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakayokuwa na wajibu wa kusimamia masuala ya Sarafu na Fedha za Kigeni na Benki za Washirika wa Muungano.

·         BENKI ZA SERIKALI ZA WASHIRIKA

Kutokana na pendekezo la kuwepo kwa Serikali ya Shirikisho la Nchi tatu, inapendekezwa kuwepo kwa Benki zitakazokuwa na jukumu la kutunza akaunti ya fedha za Serikali za kila Mshirika wa Muungano na kuzisimamia benki za biashara katika mamlaka zao.

·         BAADHI YA MAMBO AMBAYO HAYAMO KWENYE RASIMU YA KATIBA
o    Serikali ya Majimbo

Ndugu Wananchi,
Tume ilipokea maoni kuhusu mambo mengine muhimu ambayo hayamo katika rasimu hii. Moja ya mambo hayo ni Serikali za Majimbo. Tume ilichambua maoni na sababu za wananchi kupendekeza Serikali za Majimbo lakini Tume ilibaini changamoto nyingi na ikaamua kutopendekeza muundo huu.

Kwanza, baada ya kuamua kupendekeza Muundo wa Muungano wa Serikali Tatu, ilionekana ni dhahiri kuongeza ngazi nyingine ya Serikali ingeleta gharama kubwa. Serikali nyingine kumi zingekuwa na Wakuu wa Majimbo, Mabaraza ya Mawaziri na Mabunge na gharama yake ingekuwa kubwa.

Pili, katika kutembelea nchi Tume ilishuhudia dalili za wazi za mivutano ya Udini, ukanda,malalamiko ya upendeleo wa baadhi ya maeneo na ukabila. Dalili zilikuwa wazi kwamba utawala wa majimbo ungeirudisha nchi kwenye utawala utakaoigawa nchi kwa misingi ya ukabila, udini na ukanda na kuzigawa rasilimali za taifa kikanda na hivyo kuleta tofauti kubwa ya kimaendeleo katika nchi.

·         Mahakama ya Kadhi

Ndugu wananchi,
Jambo la pili ni mahakama ya kadhi. Tume ilipokea maoni mengi kuhusu suala hili. Baadhi ya wananchi walitaka mahakama ya kadhi iingizwe kwenye Katiba na wengine walipinga. Baada ya kuamua kuwa Muundo wa Muungano uwe wa Serikali Tatu, Tume iliona kuwa Mahakama ya Kadhi siyo suala la Muungano na imeliacha ili lishughulikiwe na Washirika wa Muungano.
Hata hivyo ilionekana kuwa suala siyo kuwapo au kutokuwapo kwa mahakama ya kadhi. Mahakama hizo zinaweza kuwapo bila ya kuwa katika Katiba. Zanzibar kuna mahakama ya kadhi bila kuingizwa kwenye Katiba ya Zanzibar. Kwa kutumia uzoefu huo hata Tanzania Bara inaweza kupata ufumbuzi wa suala hili.

·         Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya

Jambo la Tatu ni Kuwepo au kutokuwepo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya. Baadhi ya Wananchi walitaka Wakuu wa Mikoa na Wilaya wasiwepo, wengine walitaka Wakuu wa Mikoa na Wilaya waendelee kuwepo lakini wachaguliwe na wananchi na waengine wakasema wawepo na waendelee kuteuliwa na Rais kama ilivyo sasa. Tume ilitafakari kuhusu suala hili na kuamua kwamba siyo suala la Muungano na kwa kuwa Muundo wa Muungano imependekezwa uwe wa Serikali Tatu, Tume iliona suala la uwepo au kutokuwepo na namna ya upatikanaji wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya lishughulikiwe na Washirika wa Muungano.

·         Serikali za Mitaa

Kuhusu Serikali za Mitaa, Tume ilipokea maoni kutoka kwa wananchi kuhusu kuziimarisha Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzipatia uhuru kamili wa kujiamulia mambo yao bila kuingiliwa na Serikali Kuu. Tume ilitafakari suala hili na kuamua kwamba siyo jambo la Muungano na hivyo, litashughulikiwa kwenye Katiba za Washirika wa Muungano.

·         Uraia wa Nchi mbili

Ndugu Wananchi,
Jambo la tatu ni Uraia wa Nchi mbili. Tume ilipokea maoni kutoka kwa wananchi mbalimbali kuhusu kuwekwa kwenye Katiba suala la Uraia wa nchi mbili. Baada ya kufanya uchambuzi kwa kutengenisha mambo yapi ni ya Kikatiba na yapi yanaweza kutekelezwa bila kuingizwa kwenye Katiba bali kwenye Sheria inayohusu jambo husika, Tume imependekeza kuwa suala la Uraia wa nchi mbili linaweza kuwekwa kwenye Sheria badala ya kuwekwa kwenye Katiba. hii ni kwa sababu kutokana na utafiti uliofanywa na Tume, suala hilo linaweza kubadilika wakati wowote na hivyo likiwa kwenye Katiba linaweza kuifanya Katiba kubadilishwa mara kwa mara.

MWISHO

Naomba nichukue fursa hii kwa niaba ya Tume kuwashukuru Watanzania wote kwa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba, kuanzia hatua ya kutoa maoni na kuwachagua wawakilishi wenu watakaopata fursa ya kuipitia, kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba. Ushirikiano huu ulikuwa muhimu sana kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba hasa ukizingatia kuwa lengo ni kupata Katiba Mpya ambayo itaakisi ndoto na matakwa ya Wananchi wa Tanzania.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba, inatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar:
1.      Kwa kuipatia vifaa afisi na mahitaji ya lazima
2.      Kwa kuiwezesha Tume kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu,
3.      Kwa kutokuingilia Uhuru wa Tume wakati wa Utekelezaji wa Majukumu yake na
4.      Kutoa Wataalam wenye Weledi, Mahiri, Makini na Waadilifu ambao wameunda Sekretarieti ya Tume.

Ndugu Wananchi,
Shukrani za pekee ziwaendee:
1.      Wakuu wa Mikoa,
2.      Wakuu wa Wilaya,
3.      Wakurugenzi / Makatibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa,
4.      Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Wilaya,
5.      Watendaji wa Kata, Vijiji, Mitaa na Masheha.

Kwa kuisaidia Tume kutekeleza Majukumu yake kwa ufanisi. Aidha, tunazishukuru Asasi za Kiraia, Taasisi, Jumuiya za Kidini, Vyama vya Siasa na Makundi mbalimbali kwa namna walivyoshiriki katika kuhamasisha wananchi kushiriki katika kutoa maoni.

Mwisho ingawa siyo kwa umuhimu, Tunawashukuru Wanahabari wote kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuisaidia Tume kufikisha taarifa mbalimbali za Tume kwa Wananchi na katika kuhamasisha Wananchi kushiriki katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.

Nachukua nafasi hii kuwaomba Wananchi kupitia Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, Mabaraza ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye Malengo yanyofanana kushiriki vyema, kwa umakini, utulivu na kwa amani katika hatua hii ya kuipitia, kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba.

Tume imekuwa ikithamini na itandelea kuthamini mawazo na maoni kutoka kwa Watanzania wote.

Rasimu ya Katiba itapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya
www.katiba.go.tz

SASA NAKUOMBA MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS UIZINDUE RASMI RASIMU YA KATIBA

Ahsanteni kwa kunisikiliza.

TOA MAONI TUPATE KATIBA MPY
A
·  DefaultRASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa
HIVI SASA, Ni matangazo ya moja kwa moja (live) kutoka ukumbi wa mikutano wa karimjee yakirushwa na TBC1. mgeni rasmi ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JAKAYA MRISHO KIKWETE... KATIBA MPYA KWA TANZANIA YENYE NEEMA

TUFUATILIE

TOA MAONI YAKO