Mbeya/Dar. Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman ameweka bayana kuwa wanaunga mkono Rasimu ya Katiba na hasa
suala la Muungano wa Tanzania kuundwa na Serikali tatu kama
ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Amesema mambo mengi yaliyopendekezwa na
chama chake yamefanyiwa kazi na Tume ya Mabadiliko na kuishangaa CCM
akidai kwamba inapinga rasimu hiyo hususan suala la Serikali tatu wakati
kimsingi watu wa Tanzania Bara wamekuwa wakipunjika kwenye muundo wa
sasa wa Muungano.
Akihutubia mkutano wa kampeni ya
kuwania udiwani wa Kata ya Iyela katika Uwanja wa Bongonela, Mbeya jana
jioni, Mbowe alisema chama chake kinataka kuona Serikali ya Tanganyika
ikifufuliwa. Alikuwa akimnadi mgombea wa Chadema, Charles Mkela.
Alisema Chadema kinataka kuona
Wazanzibari wakiwa na Serikali yao ili wajiamulie mambo yao na pia
Watanganyika wawe na uongozi wao lakini waunganishwe na Serikali ya
Muungano.
Alisema muundo wa sasa wa Muungano una
matatizo. Kwa mfano, mbunge wa Zanzibar anawakilisha watu wachache zaidi
ukilinganisha na mbunge wa Bara. Wananchi mtashangaa sote tunalipwa
sawa.”
“Ila zikija Serikali tatu ina maana
kuwa kila upande wa Muungano utatumia rasilimali zake. Haya mambo
kulipana fedha nyingi kwa kazi kidogo yatakoma.”
No comments:
Post a Comment