Simon Mmbando.
Askofu Charles
Gadi wa kanisa la Good News for all Minister
amesema kuwa lugha ya udhalilishaji na matusi vilichangia kufungwa kwa timu
ya Taifa Stars.
Akizungumza na
waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo alisema
ziposababu nyingi zilizo sababisha Taifa Stara kupoteza mchezo wake dhidi ya
Ivory coast uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Askofu Gadi
alisema sababu kubwa iliyopelekea Taifa Stara kupoteza mchezo wake ni Mizaha
mingi ya washangiliaji na matusi yaliyokithiri ambayo mbele za Mungu huonekana
kama sio maombi.
Unapo tukana
Mungu husika kama vile akusikiapo unavyo omba hvyo sisi sote kama Watanzania
tulimwamini Mungu na tukiamini tutapata ushindi. Ni jambo la ajabu kuona watu
wanaomba msaada wa Mungu na wengine wanatukana matusi.
Hali hiyo
hukinzana na Mungu na mwisho wake kushindwa kama hali hiyo ya matusi
ikipitiliza ushindi kwetu itakuwa ni ndoto.
Aliendelea kusema
kuwa goli la kwanza lilifungwa kwa maombi ya Watanzania waliokuwa pale na walio
kuwa majumbani kwao wakiomba, lakini matusi yalio endelea ya kutukana maumbile
ya siri ya Mama zetu,Wake zetu, Wakwe zetu, Dada zetu na Watoto wetu wa kike
yalitukwamisha.
Matusi hayo
yalikwamisha ushindi kwa Taifa Stara kwani unapo tukana maumbile ya akina mama ni
sawa na kuchafua na kukejeli uumbaji wa Mungu kwa akina mama na hali hiyo
hupelekea laana na hali ya kushindwa.
Alisema cha ajaba
hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na imefikia wakati tuziombe mamlaka usika
hasaBunge na Wabunge na akina mama wasiyafumbie macho mambo hayo bali watunge
sheria zenye kutoa adhabu kali kwa watu wenye mazoea ya kutamka matusi.
Kama zilivyo nchi
nyingine kutema bigijii unaweza kufungwa miezi mitatu kwanini nch yetu
unalifumbia macho kosa matusi Mabaya kama hayo au yanaonekana ni situ cha
kawaida, utadhani Uwanjani pale palikuwa na kiwanda cha kuzalisha matusi.
Hali hiyo ya
matusi inachafua sura nzima ya tasnia ya michezo na itatufanya tuwe wasindikizaji kwani mambo
haya yana athari sana katika ulimwengu wa roho na yasipo tiliwa mkazo kuna
uwezekano wakuwa poteza maajenti ambao huja nchini kutafut wachezaji na kuwauza
nje ya nchi.
Kuhusu usalama
kwa watazamaji alisema uwanja ulijaa kwa kiwango ambacho ni tatizo kama
kukitokea jambo la hatari kwani watu walijazana hadi njia za lupita watu,
wanaishauri serikali iweke screen kubwa nje ya uwanja ili kwa watakaochelewa
Kuingia uwanjani
waangalie mpira lupita nje ya uwanja.
Taifa Star
ilicheza mchezo huo dhidi ya Ivory coast Juni,16 mwaka huu na kupoteza kwa kufungwa magoli 4-2 na kupoteza
nafasi yakushiriki kombe la dunia litakalofanyika nchini Brazil Juni, mwakani.
Mwisho alitoa
pongezi kwa Wachezaji, Serikali,Wananchi, TFF na kamati (Saidia Taifa Star
Ishinde) kwajitahada walizofanya katika maandalizi ya timu yetu, pia wakazi
wote wa Dar es Salaam na wote waliofika uwanjani kwani walionyesha uzalendo wa
kuipenda nchi yao.
No comments:
Post a Comment