Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Benki kuu ya Tanzania (BOT) wamefanya
maboresho katika ulipaji kodi kwa njia ya mtandao.
Akizungumza na
waandishi wa habari Mkurugenzi wa Fedha wa TRA Salehe Mshoro alisema kuanzia
Julai mosi TRA na BOT wataanzisha mfumo
wa ukusanyaji kodi utakao unganisha na mifumo ya benki.kuu na benki za
biashara.
Alisema kuwa mtu
akienda kulipa kodi zile fedha zitakwenda BOT
na papo kwa hapo atapata taarifa kwa njia ya barua pepe na taarifa zitakwenda kwa haraka TRA
zitakazoonyesha kuwa kodi imelipwa.
Alidai kuwa mfumo
huu utaondoa migongano ya mara kwa mara na pia watakuwa wamefanya makubaliano kati ya TRA na wananchi ambao ndio
walipa kodi.na pia mfumo huu wamejufanyia majaribu toka mwezi januari.
Aidha alisema
mfumo huu utaanza kutumika kwa walipa kodi wakubwa wa malipo yanayoanzia
millioni tano(5) ambao hao watakuwa mabalozi kwa wengine wadogo na alisema
kumbukumbu zitaingizwa kwenye mamlaka na watapata taarifa.
Mlipa kodi
atatakiwa kujisajili kwenye mtandao wa TRA ambao ni www.tra.go.tz akiingia kwenye wwbsite ya TRA
anaweza kupata taarifa zake muhimu za usajili na namba za utambulisho na benki
yake.
Naye Murugenzi wa
mradi Ramadhani Sangeti alisema wamejiunga na mkongo mkubwa wa taifa na endapo mkongo mkubwa hautapatikana ile
mingine itasaidia,
Mategemeo ya TRA
ni kuwa utaongeza urahisi wa ulipaji kodi na utaondoa kero za wananchi pia
itapunguza muda na kumpunguzia mteja gharama, kwani ni mfumo salama wenye kutoa
taarifa kwa wakati.
Mwisho aliwataka
walipa kodi pindi watakapopata matatizo yoyote wapige namba za huduma ambazo ni
bure kwa upande wa TTCL na Vodacom ni
08001126 au Tigo ambazo n i 0713800333 na Airtel 0786800000
No comments:
Post a Comment