Saturday, June 8, 2013

Cesc Fabregas azigombanisha Man United na Arsenal.

Klabu za Manchester United na Arsenal zimeingia kwenye vitakali ya kuwania saini ya kiungo wa kimataifa wa Hispania Cesc Fabregas anawaniwa na klabu za Manchester United na Arsenal baada ya klabu yake ya Fc Barcelona kudaiwa kuwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili yake .
Fabregas ambaye alicheza nchini England kwenye klabu ya Arsenal kwa muda wa miaka nane ameshindwa kufikia kiwango kilichotarajiwa na Barcelona wakati inamnunua toka Arsenal na kwa sasa iko tayari kumuuza ili kutengeneza fedha za kununua mchezaji mwingine .
Kocha mpya wa Manchester United David Moyes amegundua kuwa United ina tatizo kwenye safu ya kiungo na yuko tayari kuidhinisha paundi milioni 40 kumnunua Cesc , hata hivyo Arsenal ndio wenye haki ya kwanza ya kuzungumza na kiungo huyo kwa mujibu wa makubaliano baina ya Barca na Arsenal wakati wa mauzo yake toka London kwenda Hispania na endapo watakuwa tayari kumnunua basi Unitd wanaweza kupoteza nafasi ya kumsajili.
Kwa upande mwingine kocha wa Arsenal Arsene Wenger hapo jana alianza rasmi mchakato wa usajili kwenye kikosi chake baada ya kutuma ofa ya paundi milioni 22 kwa ajili ya kiungo wa Everton Marouanne Fellaini .
United nao wanajiandaa kumthibitisha beki wa timu ya taifa ya Uruguay kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 na klabu ya Penarol Guillermo Varela ambaye alithibitisha mwenyewe kufanyiwa vipimo vya afya huko Manchester.

No comments:

Post a Comment