Katika orodha hizo za kila mwezi zilizotolewa leo Tanzania
imekwea kwa nafasi tatu kutoka nafasi ya 119 waliyokuwepo mwezi uliopita mpaka
nafasi ya 116 hivyo kuendelea kufanya vyema ukilinganisha na mwaka jana.
Mabingwa wa Dunia na Ulaya, Hispania wameendelea
kung’ang’ania kileleni mwa orodha hizo wakifuatiwa na Ujerumani katika nafasi
ya pili na Argentina katika nafasi ya tatu huku kwenye nafasi ya nne kukiwa na
ingizo jipya la nchi ya Croatia waliopanda wa nafasi tano mpaka kufikia ya nne
na tano bora inafungwa na Ureno.
Kwa upande wa Afrika, Ivory Coast wameendelea kushika nafasi
ya kwanza baada ya kupanda kwa nafasi moja duniani mpaka nafasi ya 12
wakifuatiwa na Ghana katika nafasi ya pili ambao wao wamedondoka kwa nafasi
mbili mpaka ya 22 duniani. Mali wao wako nafasi ya tatu wakifuatiwa na
mabingwa soka barani Afrika Nigeria katika nafasi ya nne na tano bora Algeria.inafungwa
na
No comments:
Post a Comment