Tuesday, July 2, 2013

Simba yamuacha Kaseja

Suala hapa sio kuachwa kwa Kaseja bali Simba walipaswa kuendelea kumuamini  kwani bado ana mchango kwa simba na Taifa stars kutokana na mchango wake ambao amekuwa akiutoa ndani na nje ya uwanja


Kimsingi mchezaji akimaliza mkataba wake huwa anakuwa huru kutafuta klabu yoyote endapo klabu yake haitokuwa na nia ya kumwongezea mkataba mpya

Ikumbukwe kua Kaseja ameidakia Simba kwa miaka kumi yenye mafanikio makubwa  na kuiwezesha kubeba mataji mengi ya ligi kuu bara pamoja na kuiwakilisha vizuri katika michuano ya vilabu barani Afrika

Kwani mnamo mwaka 2003 alifanikiwa kuingoza simba kuwandoa mabingwa wa vilabu barani Afrika kwa wakati huo Zamalek ya Misri na bado aliendelea kuiongoza vizuri Simba na Taifa Stars  hali iliyopelekea kuendelea kuwa kipa namba moja hadi hivi leo

Hata hivyo sababu ambazo zimekuwa zikitolewa na  viongozi ni kuwa kiwango cha mchezaji huyo kimeshuka kitendo ambacho kimekuwa kikipingwa vikali na mashabiki wa soka ambao wanadai Kaseja hajachuja kwa kiasi hicho bali kutakuwa kuna chuki kati yake na baadhi ya viongozi

Nao baadhi ya wadau wameliambia gazeti la upendo kuwa Simba watakuja kumjutia kaseja kwani ana mchango mkubwa na hawajamuona golikipa yoyote Tanzania mwenye uwezo zaidi ya yake hivyo basi Simba walipaswa kufikiria kabla ya kufanya maamuzi ya kumuacha.

Emmanuel Bayo mkazi wa Kinondoni amesema Keseja ni golikipa mzuri sana kwa Tanzania kwani licha ya kuisadia Simba kwa muda mrefu amekuwa pia golikipa chaguo la kwanza kwa Taifa Stara hivyo sina shaka naye akiendelea kuidakia Simba.

‘Pia sababu zinazosemwa kuwa amechuja mimi sikubaliani nazo hivyo Simba wanabidi kuendelea kuwa naye na ataendelea kuwasaidia zaidi kutokana na kiwango anachokionyesha uwanjani pindi anapoiwakilisha Simba au Taifa stars’ alisema Bayo

Abubakar Rasul mkazi wa Buguruni alisema alidhani Simba wangeendelea kumuamini Kaeja kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa klabuni hapo hata kama angekuwa amechuja wangepaswa kuwa nae au kumpeleka kozi ya ukocha ili aje awe kocha wa makipa kutokana na mapenzi aliyo nayo juu ya Simba

‘Hali hii itawavunja moyo hata wachezaji wengine wenye mapenzi makubwa na Simba watacheza huku wakijua hata muda wao utakapoisha watatupwa bila kuthaminiwa mchango wao walioutoa kwa Simba’ alisema Rasul

Hivyo basi viongozi wa Simba hasa hawapaswi kuyapuuza maoni wanabidi wayafanyie kazi ili kuweza kuiboresha Simba ili hiƩndele kuwika Tanzania na Afrika kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment