HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA
MABADILIKO YA KATIBA, JAJI JOSEPH S. WARIOBA, KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI WA
HABARI KUHUSU UZINDUZI WA RASIMU YA KATIBA TAREHE 03 JUNI, 2013 KWENYE VIWANJA
VYA UKUMBI WA KARIMJEE,
DAR ES SALAAM.
·
Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilali – Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano,
·
Mhe. Mizengo K. P. Pinda (Mb.) - Waziri Mkuu,
·
Mhe. Seif Sharif Hamad – Makamu wa Kwanza wa Rais – Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar,
·
Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (Mb.) - Makamo wa Pili wa Rais -
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
·
Mhe. Mathias Chikawe – Waziri wa Katiba na Sheria,
·
Mhe. Abubakar Khamis Bakary - Waziri wa Katiba na Sheria wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
·
Mhe. Jaji Frederick M Werema - Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,
·
Mhe. Othman Masoud Othuman - Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,
·
Viongozi wa Vyama vya Siasa,
·
Waheshimiwa Wajumbe wa Tume na Wajumbe wa Sekretarieti ya
Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
·
Ndugu Wananchi,
·
Wageni Waalikwa
·
Waandishi wa Habari Mabibi na Mabwana.
1.
UTANGULIZI
Ndugu
Wananchi,
Awali ya yote namshukuru mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kufikia hatua hii ya
leo ya kuzindua Rasimu ya Katiba. pia, niwashukuru ninyi nyote mliohudhuria
halfa hii ikiwa ni mwendelezo wa mchakato muhimu wa Mabadiliko ya Katiba ya
nchi yetu.
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilipitishwa Bungeni Novemba, 2011 na kufanyiwa
mabadiliko Februari, 2012. Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliundwa kwa mujibu wa
Kifungu 6(1) cha sheria hiyo (Cap.83). Wajumbe 34 wa Tume waliteuliwa na
kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,
mwezi Aprili, 2012. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Tume imepewa
miezi kumi na minane kukamilisha kazi yake kuanzia siku ilipoanza kazi rasmi
ambayo ilikuwa Mei 2, 2012.
Tume iliandaa ratiba ya utekelezaji wa majukumu yake. Kufuatana na ratiba hiyo
Tume ilijipanga kukusanya maoni ya wananchi katika kipindi cha miezi mitano
kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba, 2012. Kazi hiyo ilifanywa kama tulivyopanga.
Tume ilijigawa katika makundi na ilitembelea mkoa yote thelathini.
Tume ilifanya mikutano 1,942 ambayo ilihudhuriwa na wananchi wapatao
1,365,337 ambao kati ya hao wananchi 333,537 walitoa maoni ama kwa
mazungumzo ya ana kwa ana au kwa maandishi. Tume pia ilipata maoni ya wananchi
wengi, wa ndani na nje ya nchi kwa njia mbali mbali kama vile; Mikutano ya
hadhara, Fomu maalum za Tume, barua kupitia Masanduku ya Barua ya Tume,
Mitandao ya Kijamii ya barua pepe; facebook ya Tume, Tovuti ya Tume; Makala
mbalimbali kutoka kwenye magazeti na ujumbe mfupi wa simu.
Tume ilitumia mwezi Januari, 2013 kukusanya maoni ya makundi mbali mbali katika
jamii, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa, taasisi za Serikali, taasisi za
dini, wakulima, wafugaji, wafanyakazi, asasi za kiraia na kadhalika. Makundi
zaidi ya 160 yalikutana na Tume na kutoa maoni. Tume pia ilipata maoni ya
viongozi wa juu wa Serikali walioko madarakani na waliostaafu. Kwa jumla
viongozi 43walitoa maoni.
Tume ilipanga kutumia miezi mitatu ya Februari, Machi na Aprili kuchambua maoni
ya wananchi na kuandaa Rasimu ya Katiba. Lakini tuligundua kwamba maoni
tuliyopata yalikuwa mengi sana, na pamoja na matumizi ya teknolojia ya kisasa,
tulitambua umuhimu wa kuongeza muda hadi mwisho wa mwezi Mei, Maoni ya wananchi
yaligusa mambo yote yanayohusu Katiba na mengi ya maoni hayo yalikinzana.
Aidha, baadhi ya maoni yaligusia masuala ya Kisera, Kisheria na Kiutendaji.
Tulifanya uchambuzi makini na wa ndani wa maoni hayo na kazi hiyo
tumeikamilisha na rasimu imeandaliwa na Tume na leo tupo hapa kwa ajili ya
kuizindua, ambapo Wananchi watapata nafasi ya kuisoma. Kwa leo, kwa niaba ya
Tume, napenda kutaja maeneo machache tu ambayo tunayapendekeza.
·
IBARA ZINAZOPENDEKEZWA KWENYE RASIMU YA KATIBA
Ndugu
Wananchi,
Katiba yetu ya sasa ina ibara 152. Tume ilifanya jitihada kubwa sana
kuandaa rasimu ambayo siyo ndefu. Lakini katika hali halisi haikuwezekana. Rasimu
ya Katiba tunayopendekeza ina ibara 240.
·
MISINGI MIKUU YA TAIFA
Utangulizi wa Katiba
ya sasa ndio unaobeba misingi mikuu ya Taifa ambayo ni Uhuru, Haki, Udugu na
Amani. Tume inaamini kwamba misingi hii ni mizito na inastahili kubaki
kwenye Katiba mpya. Hata hivyo, Tume imeona ni busara kuongeza misingi mingine
mitatu ya Usawa, Umoja na Mshikamano. Hivyo, Tume imependekeza Katiba iwe na
Misingi Mikuu saba ya Taifa;yaani; Uhuru, Haki, Udugu, Usawa, Umoja, Amani
na Mshikamano.
·
TUNU ZA TAIFA
Katiba yetu ya sasa
haina sehemu inayoelezea tunu za Taifa (National Values). Wananchi wengi
walitoa maoni kwamba Katiba itaje Tunu za Taifa. Tume imependekeza Tunu
zifuatazo zitajwe ndani ya Katiba. Tunu hizo ni;- Utu, Uzalendo, Uadilifu,
Umoja, Uwazi, Uwajibikaji na Lugha yetu ya taifa ya Kiswahili.
·
MALENGO YA TAIFA
Tume ilipozunguka
nchi nzima wananchi walizungumzia sana kuhusu malengo ya taifa. Walitaka Katiba
ionyeshe dira ya taifa. Wananchi wanayo ndoto yao ya Tanzania ya kesho na kesho
kutwa. Kwa kuzingatia maoni ya wananchi, kuna sura nzima inayohusu Malengo
mahsusi na ya msingi ya mwelekeo wa shughuli za Kiserikali na Sera za Kitaifa.
Rasimu ya Katiba inaeleza kuwa Malengo ya Kitaifa yaliyoainishwa ndani ya
Rasimu yatakuwa ni Mwongozo kwa Serikali, Bunge, Mahakama, Vyama vya Siasa,
Taasisi na Mamlaka nyingine, na kwa kila mwananchi katika matumizi au kutafsiri
Masharti ya Katiba au Sheria nyingine za Nchi.
Kwa msingi huo, Tume imependekeza malengo makuu ya taifa yapanuliwe kwa
mpangilio wa kuonesha malengo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, kimazingira
na sera ya mambo ya nje. Malengo hayo yameingizwa kwenye Rasimu ya Katiba.
·
VYOMBO VYA KIKATIBA
Wananchi
walizungumzia suala la kubainishwa kwa vyombo vya Kikatiba na kuingizwa kwenye Katiba
ili viwe na nguvu ya Kikatiba katika utekelezaji wa majukumu yao. Tume
imependekeza baadhi ya vyombo vifuatavyo viwe vya Kikatiba; Tume ya Uhusiano na
Uratibu wa Serikali, Baraza la Mawaziri, Kamati Maalum ya Makatibu Wakuu na
Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri; Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa, Tume
Huru ya Uchaguzi, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Tume ya Utumishi wa Umma, Tume
ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
·
MAADILI YA VIONGOZI NA MIIKO YA UONGOZI
Wananchi wengi pia
walizungumzia kwa upana sana kuhusu maadili na miiko ya Viongozi, kwa
kuzingatia maoni ya wananchi Tume inapendekeza maadili ya viongozi wa umma,
pamoja na miiko ya uongozi yawekwe kwenye Katiba. Tume pia imependekeza
kuwa Sekretariati ya Maadili ibadilishwe kuwa Tume yenye mamlaka makubwa ya
kusimamia maadili ya viongozi wanaovunja miiko ya uongozi.
·
HAKI ZA BINADAMU
Kuhusu haki za
binadamu wananchi walitaka haki hizi ziimarishwe na kusiwe na vikwazo visivyo
vya lazima. Tume imependekeza mabadiliko katika baadhi ya haki za binadamu kwa
madhumuni ya kuziimarisha. Moja ya mabadiliko hayo ni kuhusu uhuru wa
mwananchi kushiriki shughuli za umma. Tume inapendekeza kwamba vikwazo
vilivyowekwa kuzuia mgombea huru viondolewe. Kwa maana nyingine Tume
inapendekeza mgombea binafsi aruhusiwe.
Tume pia, inapendekeza haki mpya ziingizwe kwenye Katiba ikiwa ni pamoja
na haki ya wafanyakazi, , haki ya mtoto, haki za Watu wenye Ulemavu, Haki za
Wanawake, Haki za Wazee, Haki za Makundi Madogo katika Jamii, Haki ya Elimu na
Kujifunza, Haki ya kupata habari, Haki na uhuru wa habari na vyombo vya habari
na kadhalika.
·
URAIA
Wananchi wengi
walipendekeza kuwa suala la Uraia libainishwe wazi kwenye Katiba. Tume
imependekeza kwa kutaja Raia wa Jamhuri ya Muungano na haki zake.
·
MIKOPO NA DENI LA TAIFA
Ndugu
Wananchi,
Wananchi walizungumzia suala la uwepo wa Ukomo wa nchi kukopa na uwepo wa
utaratibu wa kulipa Deni la Taifa ili kuilinda Nchi isiwe na deni kubwa. Kwa
kuzingatia maoni ya Wananchi, Tume imependekeza kuwa, Serikali itawajibika
kutoa taarifa Bungeni kuhusu Mikopo kwa kuainisha kiasi cha deni lililopo, riba
yake na matumizi ya fedha za Mikopo na utaratibu wa kulipa Madeni ya Taifa.
·
MFUMO WA UTAWALA
Kuhusu utawala, Tume
inapendekeza Tanzania iendelee na mfumo wa Jamhuri kwa maana ya nchi
inayoongozwa na Rais Mtendaji ambaye ni Mkuu wa nchi, Kiongozi wa Serikali na
Amiri Jeshi Mkuu.
·
UCHAGUZI WA RAIS
o
Umri wa kugombea Urais
Tume ilipokea maoni
yanayokinzana kuhusu umri wa mwananchi kugombea Urais. Baadhi walipendekeza mtu
akishakuwa na sifa ya kupiga kura awe pia na sifa ya kugombea Urais. Umri wa
mtu kuruhusiwa kupiga kura ni miaka 18. Wengine walipendekeza umri uliopo
kwenye Katiba wa mtu kugombea Urais, yaani kuanzia miaka 40 na kuendelea,
uendelee kubaki kama ulivyo.
Wengine walisema Umri wa mtu kuruhusiwa kugombea Urais uwe miaka 35 au miaka 50
na kuendelea.
Tume imeyachambua maoni yote hayo, ikafanya utafiti kwa kupitia Katiba za Nchi
zingine na uhalisia wa watu wanaogombea na kuchaguliwa kuwa Marais katika Nchi
mbalimbali Duniani ambazo zingine zimeruhusu wagombea wa nafasi ya Urais kuwa
na umri chini ya miaka 40.
Wengi walioomba kugombea nafasi hiyo walikuwa na umri wa miaka 40 au zaidi.
Kwa kuzingatia maoni ya wananchi, utafiti na hali halisi, Tume inapendekeza
Rais aendelea kuchaguliwa na wananchi na pamoja na sifa nyingine, mtu anayeomba
urais asiwe chini ya miaka 40.
Uchaguzi wa Rais itakuwa kama ilivyo sasa, yaani mgombea Urais atakuwa na
mgombea mwenza kwa utaratibu kama ilivyo sasa. Isipokuwa, Tume imependekeza Mgombea
Urais anaweza kupendekezwa na Chama cha Siasa au kuwa Mgombea Huru.
Mgombea wa nafasi ya Rais atatangazwa kuwa mshindi iwapo atakuwa amepata
kura zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote zilizopigwa.
Hata hivyo, matokeo ya uchaguzi wa Rais yanaweza kulalamikiwa Mahakamani,
lakini siyo kila mtu anaweza kufungua kesi. Wanaoweza kufungua kesi ni wagombea
Urais. Aidha, ni Mahakama ya Juu pekee ndiyo itakuwa na Mamlaka na uwezo wa
kusikiliza malalamiko kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais na shauri lazima
liamuliwe ndani ya mwezi mmoja, yaani siku therathini.
Rais aliyeshinda ataapishwa siku thelathini tangu alipotangazwa kuwa mshindi
au kuthibitishwa na Mahakama.
·
MADARAKA YA RAIS
Ndugu
Wananchi,
Tume inapendekeza kwamba, Rais abaki na madaraka ya uteuzi wa viongozi wa ngazi
za juu. Hata hivyo inapendekezwa Rais ashirikiane na taasisi na vyombo vingine
katika uteuzi. Kwa mfano:
Uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri, Rais atateua na Bunge litathibitisha.
Kuhusu Jaji Mkuu na Naibu Jaji Mkuu Rais atawateua kutokana na majina ya
watu waliopendekezwa na Tume ya Uutumishi wa Mahakama na baada ya hapo Bunge
litathibitisha.
Kuhusu Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama inapendekezwa kianzishwe
chombo kipya kitakachoitwa Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa, ambalo kati ya
majukumu yake itakuwa ni kumshauri Rais kuhusu uteuzi wa Wakuu wa vyombo vya
ulinzi na usalama.
Kuhusu Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu watateuliwa na Rais
kutokana na mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma.
·
KINGA YA RAIS
Tume baada ya kupitia
maoni ya Wananchi, inapendekeza Rais abaki na kinga kama ilivyo sasa na anaweza
kushitakiwa na Bunge kama ilivyo Katiba ya sasa.
·
IDADI YA MAWAZIRI
Inapendekezwa Rais
aunde Serikali ndogo iliyo na Mawaziri wasiozidi kumi na tano na
mawaziri hao wasiwe wabunge. Mawaziri hawatahudhuria vikao vya Bunge isipokuwa
kama watahitajika kutoa ufafanuzi kwenye kamati za Bunge.
·
BUNGE
Ndugu
Wananchi,
Kuhusu Bunge kutakuwa na wabunge wa aina mbili. Kutakuwa na Wabunge wa
kuchaguliwa na wabunge watano wa kuteuliwa na Rais kuwakilisha Watu
wenye Ulemavu.
Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili mmoja mwanamke na mwingine
mwanamume.
Tume inapendekeza kwamba, Mbunge akifukuzwa na Chama cha Siasa abaki kuwa
Mbunge lakini akihama Chama atapoteza Ubunge wake.
Inapendekezwa ukomo wa Ubunge uwe vipindi vitatu vya miaka mitano mitano. Hata
hivyo, wananchi wanaweza kumwondoa mbunge wao kabla ya mwisho wa kipindi
chake.
Inapendekezwa pia kusiwepo na uchaguzi mdogo isipokuwa kama nafasi
inayokuwa wazi inatokana na Mbunge huru ndipo utafanyika uchaguzi mdogo kujaza
nafasi hiyo, lakini kama nafasi ikiwa wazi kutokana na Mbunge wa Chama cha
Siasa basi nafasi hiyo, ijazwe na mtu kutoka Chama hicho.
Inapendekezwa Spika na Naibu Spika wasitokane na Wabunge na wasiwe Viongozi
wa vyama vya Siasa.
·
TUME YA UCHAGUZI
Tume imefanya
uchambuzi wa maoni ya wananchi kuhusu Tume ya Uchaguzi. Tume inapendekeza jina
la tume liwe Tume Huru ya Uchaguzi. Tume pia inapendekeza sifa za
wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ziwekwe kwenye Katiba. Wajumbe wa Tume Huru ya
Uchaguzi watapatikana kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizoainishwa ndani
ya Katiba kwa kuomba. Majina ya waombaji yatachambuliwa na Kamati ya Uteuzi
ambayo Mwenyekiti wake atakuwa Jaji Mkuu na wajumbe wengine sita ambao ni
Majaji Wakuu wa nchi Washirika, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Maspika
wa Mabunge wa nchi Washirika na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu.
Kamati ya uteuzi itapendekeza majina ya watu wanaofaa kwa Rais ambaye atateua
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wengine. Bunge litathibitisha uteuzi
wao. Wabunge na viongozi wa aina hiyo hawatakuwa na sifa za kuwa wajumbe wa
tume ya uchaguzi.
Inapendekezwa Tume huru ya Uchaguzi isimamie masuala ya uchaguzi, kura ya
maoni na Usajili wa Vyama vya Siasa.
·
MAHAKAMA
Kuhusu Mahakama
inapendekezwa kuanzishwa kwa Mahakama ya Juu (Supreme Court) Majaji wa Mahakama
ya Juu na Mahakama ya Rufani watateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume ya
Utumishi wa Mahakama.
·
MUUNDO WA MUUNGANO
Ndugu
Wananchi,
Suala la muundo wa Muungano ndilo lililokuwa gumu kuliko masuala yote.
Tume ilitumia muda mwingi kuchambua maoni ya wananchi. Pamoja na kwamba hadidu
za rejea zilielekeza Tume kuzingatia uwepo wa Muungano, baadhi ya wananchi
walitoa maoni kwamba Muungano uvunjwe na Tume iliyapokea maoni hayo. Licha ya
kwamba waliotaka kuvunjwa muungano walikuwa wachache sana, Tume ilichambua
sababu walizotoa na kuridhika kwamba hazikuwa na uzito.
Wananchi walio wengi walitaka Muungano uendelee. Kati yao wapo waliopendekeza
Muungano wa Serikali moja, Serikali mbili, Serikali tatu, Serikali nne na
muungano wa mkataba. Sababu za wale waliopendekeza Serikali nne hazikuwa na
uzito, kwa hiyo Tume ikaamua kutopendekeza muundo huo.
Wananchi waliopendekeza Serikali moja walikuwa wachache lakini sababu zao
zilkuwa na uzito. Hata hivyo, Tume kwa kuzingatia hali halisi iliona ni
changamoto kubwa kuwa na Muungano wa Serikali Moja.
Wananchi waliopendekeza Muungano wa Mkataba walikuwa wengi (hasa wananchi wa
Zanzibar) na sababu zao zilikuwa na uzito. Lakini uchambuzi wa Tume ilionekana
wazi kwamba ili kupata mkataba lazima kwanza kuwe na nchi mbili huru kabisa
lakini hakukuwa na mazingira ya uhakika ya kupata mkataba wa muungano. Tume
iliona kuna changamoto ya muungano kuvunjika ingawa waliotoa maoni walisisitiza
muungano ubaki. Hivyo, Tume iliamua kutopendekeza muundo huo.
Wananchi waliopendekeza Tanzania iendelee na Muundo wa sasa wa Serikali mbili
walikuwa wengi na sababu zao zilikuwa nzito. Hata hivyo, wananchi katika kundi
hili walipendekeza mabadiliko mengi na makubwa. Tathmini ya Tume ilionyesha
kwamba isingewezekana kufanya mabadiliko yote yaliyopendekezwa.
Wananchi waliopendekeza muundo wa Serikali tatu walikuwa wengi kuliko makundi
yote. Sababu zao zilikuwa nzito lakini pia kulikuwa na changamoto nyingi na
nzito. Pamoja na maoni ya wananchi Tume ilirejea sababu za kupendekeza muundo
huu zilizotolewa na Tume zilizopita na Tafiti zilizofanywa na Tume kuhusu aina
mbalimbali za Muungano. Baada ya yote hayo Tume ilifikia uamuzi wa kupendekeza mfumo
wa Serikali tatu. Yaani Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanzania
Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
·
ORODHA YA MAMBO YA MUUNGANO
Ndugu
Wananchi,
Tume imependekeza katika Rasimu ya Katiba kuwa orodha ya Mambo ya Muungano yawe
7 badala ya 22 yaliyopo sasa.
Mambo ya muungano yanayopendekwa ni:
1.
Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2.
Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
3.
Uraia na Uhamiaji
4.
Sarafu na Benki Kuu
5.
Mambo ya Nje
6.
Usajili wa Vyama vya Siasa
7.
Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya Kodi yatokanayo na
Mambo ya Muungano.
·
BENKI KUU
Kwa kuwa Tume
imependekeza Muungano wa Shirikisho kutokana na uzito wa maoni ya wananchi.
Hivyokutakuwa na Benki Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakayokuwa na wajibu
wa kusimamia masuala ya Sarafu na Fedha za Kigeni na Benki za Washirika wa
Muungano.
·
BENKI ZA SERIKALI ZA WASHIRIKA
Kutokana na pendekezo
la kuwepo kwa Serikali ya Shirikisho la Nchi tatu, inapendekezwa kuwepo kwa
Benki zitakazokuwa na jukumu la kutunza akaunti ya fedha za Serikali za kila
Mshirika wa Muungano na kuzisimamia benki za biashara katika mamlaka zao.
·
BAADHI YA MAMBO AMBAYO HAYAMO KWENYE RASIMU YA KATIBA
o
Serikali ya Majimbo
Ndugu
Wananchi,
Tume ilipokea maoni kuhusu mambo mengine muhimu ambayo hayamo katika rasimu
hii. Moja ya mambo hayo ni Serikali za Majimbo. Tume ilichambua maoni na
sababu za wananchi kupendekeza Serikali za Majimbo lakini Tume ilibaini
changamoto nyingi na ikaamua kutopendekeza muundo huu.
Kwanza, baada ya kuamua kupendekeza Muundo wa Muungano wa Serikali Tatu,
ilionekana ni dhahiri kuongeza ngazi nyingine ya Serikali ingeleta gharama
kubwa. Serikali nyingine kumi zingekuwa na Wakuu wa Majimbo, Mabaraza ya
Mawaziri na Mabunge na gharama yake ingekuwa kubwa.
Pili, katika kutembelea nchi Tume ilishuhudia dalili za wazi za mivutano ya
Udini, ukanda,malalamiko ya upendeleo wa baadhi ya maeneo na ukabila.
Dalili zilikuwa wazi kwamba utawala wa majimbo ungeirudisha nchi kwenye
utawala utakaoigawa nchi kwa misingi ya ukabila, udini na ukanda na kuzigawa
rasilimali za taifa kikanda na hivyo kuleta tofauti kubwa ya kimaendeleo katika
nchi.
·
Mahakama ya Kadhi
Ndugu
wananchi,
Jambo la pili ni mahakama ya kadhi. Tume ilipokea maoni mengi kuhusu suala
hili. Baadhi ya wananchi walitaka mahakama ya kadhi iingizwe kwenye Katiba na
wengine walipinga. Baada ya kuamua kuwa Muundo wa Muungano uwe wa Serikali
Tatu, Tume iliona kuwa Mahakama ya Kadhi siyo suala la Muungano na
imeliacha ili lishughulikiwe na Washirika wa Muungano.
Hata hivyo ilionekana kuwa suala siyo kuwapo au kutokuwapo kwa mahakama
ya kadhi. Mahakama hizo zinaweza kuwapo bila ya kuwa katika Katiba. Zanzibar
kuna mahakama ya kadhi bila kuingizwa kwenye Katiba ya Zanzibar. Kwa kutumia
uzoefu huo hata Tanzania Bara inaweza kupata ufumbuzi wa suala hili.
·
Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya
Jambo
la Tatu ni Kuwepo au kutokuwepo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya. Baadhi ya Wananchi
walitaka Wakuu wa Mikoa na Wilaya wasiwepo, wengine walitaka Wakuu wa Mikoa na
Wilaya waendelee kuwepo lakini wachaguliwe na wananchi na waengine wakasema
wawepo na waendelee kuteuliwa na Rais kama ilivyo sasa. Tume ilitafakari kuhusu
suala hili na kuamua kwamba siyo suala la Muungano na kwa kuwa Muundo wa
Muungano imependekezwa uwe wa Serikali Tatu, Tume iliona suala la uwepo au
kutokuwepo na namna ya upatikanaji wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya lishughulikiwe
na Washirika wa Muungano.
·
Serikali za Mitaa
Kuhusu
Serikali za Mitaa,
Tume ilipokea maoni kutoka kwa wananchi kuhusu kuziimarisha Mamlaka za Serikali
za Mitaa kwa kuzipatia uhuru kamili wa kujiamulia mambo yao bila kuingiliwa na
Serikali Kuu. Tume ilitafakari suala hili na kuamua kwamba siyo jambo la
Muungano na hivyo, litashughulikiwa kwenye Katiba za Washirika wa Muungano.
·
Uraia wa Nchi mbili
Ndugu
Wananchi,
Jambo la tatu ni Uraia wa Nchi mbili. Tume ilipokea maoni kutoka kwa wananchi
mbalimbali kuhusu kuwekwa kwenye Katiba suala la Uraia wa nchi mbili. Baada ya
kufanya uchambuzi kwa kutengenisha mambo yapi ni ya Kikatiba na yapi yanaweza
kutekelezwa bila kuingizwa kwenye Katiba bali kwenye Sheria inayohusu jambo
husika, Tume imependekeza kuwa suala la Uraia wa nchi mbili linaweza kuwekwa
kwenye Sheria badala ya kuwekwa kwenye Katiba. hii ni kwa sababu kutokana
na utafiti uliofanywa na Tume, suala hilo linaweza kubadilika wakati wowote na
hivyo likiwa kwenye Katiba linaweza kuifanya Katiba kubadilishwa mara kwa mara.
MWISHO
Naomba nichukue fursa
hii kwa niaba ya Tume kuwashukuru Watanzania wote kwa kushiriki kikamilifu
katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba, kuanzia hatua ya kutoa maoni na
kuwachagua wawakilishi wenu watakaopata fursa ya kuipitia, kuijadili na
kuitolea maoni Rasimu ya Katiba. Ushirikiano huu ulikuwa muhimu sana kwa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba hasa ukizingatia kuwa lengo ni kupata Katiba Mpya
ambayo itaakisi ndoto na matakwa ya Wananchi wa Tanzania.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, inatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar:
1.
Kwa
kuipatia vifaa afisi na mahitaji ya lazima
2.
Kwa
kuiwezesha Tume kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu,
3.
Kwa
kutokuingilia Uhuru wa Tume wakati wa Utekelezaji wa Majukumu yake na
4.
Kutoa
Wataalam wenye Weledi, Mahiri, Makini na Waadilifu ambao wameunda
Sekretarieti ya Tume.
Ndugu
Wananchi,
Shukrani za pekee ziwaendee:
1.
Wakuu
wa Mikoa,
2.
Wakuu
wa Wilaya,
3.
Wakurugenzi
/ Makatibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa,
4.
Makamanda
wa Polisi wa Mikoa na Wilaya,
5.
Watendaji
wa Kata, Vijiji, Mitaa na Masheha.
Kwa kuisaidia Tume
kutekeleza Majukumu yake kwa ufanisi. Aidha, tunazishukuru Asasi za Kiraia,
Taasisi, Jumuiya za Kidini, Vyama vya Siasa na Makundi mbalimbali kwa namna
walivyoshiriki katika kuhamasisha wananchi kushiriki katika kutoa maoni.
Mwisho ingawa siyo kwa umuhimu, Tunawashukuru Wanahabari wote kwa kazi nzuri
waliyoifanya ya kuisaidia Tume kufikisha taarifa mbalimbali za Tume kwa Wananchi
na katika kuhamasisha Wananchi kushiriki katika mchakato wa Mabadiliko ya
Katiba.
Nachukua nafasi hii kuwaomba Wananchi kupitia Mabaraza ya Katiba ya Wilaya,
Mabaraza ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye Malengo
yanyofanana kushiriki vyema, kwa umakini, utulivu na kwa amani katika hatua hii
ya kuipitia, kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba.
Tume imekuwa ikithamini na itandelea kuthamini mawazo na maoni kutoka kwa
Watanzania wote.
Rasimu ya Katiba itapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya www.katiba.go.tz
SASA NAKUOMBA MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS UIZINDUE RASMI RASIMU YA KATIBA
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
TOA MAONI TUPATE KATIBA MPYA
· RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa
HIVI SASA, Ni matangazo ya moja kwa moja (live) kutoka
ukumbi wa mikutano wa karimjee yakirushwa na TBC1. mgeni rasmi ni rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JAKAYA MRISHO KIKWETE... KATIBA MPYA KWA
TANZANIA YENYE NEEMA
TUFUATILIE
HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA
MABADILIKO YA KATIBA, JAJI JOSEPH S. WARIOBA, KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI WA
HABARI KUHUSU UZINDUZI WA RASIMU YA KATIBA TAREHE 03 JUNI, 2013 KWENYE VIWANJA
VYA UKUMBI WA KARIMJEE,
DAR ES SALAAM.
·
Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilali – Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano,
·
Mhe. Mizengo K. P. Pinda (Mb.) - Waziri Mkuu,
·
Mhe. Seif Sharif Hamad – Makamu wa Kwanza wa Rais – Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar,
·
Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (Mb.) - Makamo wa Pili wa Rais -
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
·
Mhe. Mathias Chikawe – Waziri wa Katiba na Sheria,
·
Mhe. Abubakar Khamis Bakary - Waziri wa Katiba na Sheria wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
·
Mhe. Jaji Frederick M Werema - Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,
·
Mhe. Othman Masoud Othuman - Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,
·
Viongozi wa Vyama vya Siasa,
·
Waheshimiwa Wajumbe wa Tume na Wajumbe wa Sekretarieti ya
Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
·
Ndugu Wananchi,
·
Wageni Waalikwa
·
Waandishi wa Habari Mabibi na Mabwana.
1.
UTANGULIZI
Ndugu
Wananchi,
Awali ya yote namshukuru mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kufikia hatua hii ya
leo ya kuzindua Rasimu ya Katiba. pia, niwashukuru ninyi nyote mliohudhuria
halfa hii ikiwa ni mwendelezo wa mchakato muhimu wa Mabadiliko ya Katiba ya
nchi yetu.
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilipitishwa Bungeni Novemba, 2011 na kufanyiwa
mabadiliko Februari, 2012. Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliundwa kwa mujibu wa
Kifungu 6(1) cha sheria hiyo (Cap.83). Wajumbe 34 wa Tume waliteuliwa na
kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,
mwezi Aprili, 2012. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Tume imepewa
miezi kumi na minane kukamilisha kazi yake kuanzia siku ilipoanza kazi rasmi
ambayo ilikuwa Mei 2, 2012.
Tume iliandaa ratiba ya utekelezaji wa majukumu yake. Kufuatana na ratiba hiyo
Tume ilijipanga kukusanya maoni ya wananchi katika kipindi cha miezi mitano
kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba, 2012. Kazi hiyo ilifanywa kama tulivyopanga.
Tume ilijigawa katika makundi na ilitembelea mkoa yote thelathini.
Tume ilifanya mikutano 1,942 ambayo ilihudhuriwa na wananchi wapatao
1,365,337 ambao kati ya hao wananchi 333,537 walitoa maoni ama kwa
mazungumzo ya ana kwa ana au kwa maandishi. Tume pia ilipata maoni ya wananchi
wengi, wa ndani na nje ya nchi kwa njia mbali mbali kama vile; Mikutano ya
hadhara, Fomu maalum za Tume, barua kupitia Masanduku ya Barua ya Tume,
Mitandao ya Kijamii ya barua pepe; facebook ya Tume, Tovuti ya Tume; Makala
mbalimbali kutoka kwenye magazeti na ujumbe mfupi wa simu.
Tume ilitumia mwezi Januari, 2013 kukusanya maoni ya makundi mbali mbali katika
jamii, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa, taasisi za Serikali, taasisi za
dini, wakulima, wafugaji, wafanyakazi, asasi za kiraia na kadhalika. Makundi
zaidi ya 160 yalikutana na Tume na kutoa maoni. Tume pia ilipata maoni ya
viongozi wa juu wa Serikali walioko madarakani na waliostaafu. Kwa jumla
viongozi 43walitoa maoni.
Tume ilipanga kutumia miezi mitatu ya Februari, Machi na Aprili kuchambua maoni
ya wananchi na kuandaa Rasimu ya Katiba. Lakini tuligundua kwamba maoni
tuliyopata yalikuwa mengi sana, na pamoja na matumizi ya teknolojia ya kisasa,
tulitambua umuhimu wa kuongeza muda hadi mwisho wa mwezi Mei, Maoni ya wananchi
yaligusa mambo yote yanayohusu Katiba na mengi ya maoni hayo yalikinzana.
Aidha, baadhi ya maoni yaligusia masuala ya Kisera, Kisheria na Kiutendaji.
Tulifanya uchambuzi makini na wa ndani wa maoni hayo na kazi hiyo
tumeikamilisha na rasimu imeandaliwa na Tume na leo tupo hapa kwa ajili ya
kuizindua, ambapo Wananchi watapata nafasi ya kuisoma. Kwa leo, kwa niaba ya
Tume, napenda kutaja maeneo machache tu ambayo tunayapendekeza.
·
IBARA ZINAZOPENDEKEZWA KWENYE RASIMU YA KATIBA
Ndugu
Wananchi,
Katiba yetu ya sasa ina ibara 152. Tume ilifanya jitihada kubwa sana
kuandaa rasimu ambayo siyo ndefu. Lakini katika hali halisi haikuwezekana. Rasimu
ya Katiba tunayopendekeza ina ibara 240.
·
MISINGI MIKUU YA TAIFA
Utangulizi wa Katiba
ya sasa ndio unaobeba misingi mikuu ya Taifa ambayo ni Uhuru, Haki, Udugu na
Amani. Tume inaamini kwamba misingi hii ni mizito na inastahili kubaki
kwenye Katiba mpya. Hata hivyo, Tume imeona ni busara kuongeza misingi mingine
mitatu ya Usawa, Umoja na Mshikamano. Hivyo, Tume imependekeza Katiba iwe na
Misingi Mikuu saba ya Taifa;yaani; Uhuru, Haki, Udugu, Usawa, Umoja, Amani
na Mshikamano.
·
TUNU ZA TAIFA
Katiba yetu ya sasa
haina sehemu inayoelezea tunu za Taifa (National Values). Wananchi wengi
walitoa maoni kwamba Katiba itaje Tunu za Taifa. Tume imependekeza Tunu
zifuatazo zitajwe ndani ya Katiba. Tunu hizo ni;- Utu, Uzalendo, Uadilifu,
Umoja, Uwazi, Uwajibikaji na Lugha yetu ya taifa ya Kiswahili.
·
MALENGO YA TAIFA
Tume ilipozunguka
nchi nzima wananchi walizungumzia sana kuhusu malengo ya taifa. Walitaka Katiba
ionyeshe dira ya taifa. Wananchi wanayo ndoto yao ya Tanzania ya kesho na kesho
kutwa. Kwa kuzingatia maoni ya wananchi, kuna sura nzima inayohusu Malengo
mahsusi na ya msingi ya mwelekeo wa shughuli za Kiserikali na Sera za Kitaifa.
Rasimu ya Katiba inaeleza kuwa Malengo ya Kitaifa yaliyoainishwa ndani ya
Rasimu yatakuwa ni Mwongozo kwa Serikali, Bunge, Mahakama, Vyama vya Siasa,
Taasisi na Mamlaka nyingine, na kwa kila mwananchi katika matumizi au kutafsiri
Masharti ya Katiba au Sheria nyingine za Nchi.
Kwa msingi huo, Tume imependekeza malengo makuu ya taifa yapanuliwe kwa
mpangilio wa kuonesha malengo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni,
kimazingira na sera ya mambo ya nje. Malengo hayo yameingizwa kwenye Rasimu
ya Katiba.
·
VYOMBO VYA KIKATIBA
Wananchi
walizungumzia suala la kubainishwa kwa vyombo vya Kikatiba na kuingizwa kwenye Katiba
ili viwe na nguvu ya Kikatiba katika utekelezaji wa majukumu yao. Tume
imependekeza baadhi ya vyombo vifuatavyo viwe vya Kikatiba; Tume ya Uhusiano na
Uratibu wa Serikali, Baraza la Mawaziri, Kamati Maalum ya Makatibu Wakuu na
Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri; Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa, Tume
Huru ya Uchaguzi, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Tume ya Utumishi wa Umma, Tume
ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
·
MAADILI YA VIONGOZI NA MIIKO YA UONGOZI
Wananchi wengi pia
walizungumzia kwa upana sana kuhusu maadili na miiko ya Viongozi, kwa
kuzingatia maoni ya wananchi Tume inapendekeza maadili ya viongozi wa umma,
pamoja na miiko ya uongozi yawekwe kwenye Katiba. Tume pia imependekeza
kuwa Sekretariati ya Maadili ibadilishwe kuwa Tume yenye mamlaka makubwa ya
kusimamia maadili ya viongozi wanaovunja miiko ya uongozi.
·
HAKI ZA BINADAMU
Kuhusu haki za
binadamu wananchi walitaka haki hizi ziimarishwe na kusiwe na vikwazo visivyo
vya lazima. Tume imependekeza mabadiliko katika baadhi ya haki za binadamu kwa
madhumuni ya kuziimarisha. Moja ya mabadiliko hayo ni kuhusu uhuru wa
mwananchi kushiriki shughuli za umma. Tume inapendekeza kwamba vikwazo
vilivyowekwa kuzuia mgombea huru viondolewe. Kwa maana nyingine Tume
inapendekeza mgombea binafsi aruhusiwe.
Tume pia, inapendekeza haki mpya ziingizwe kwenye Katiba ikiwa ni pamoja
na haki ya wafanyakazi, , haki ya mtoto, haki za Watu wenye Ulemavu, Haki za
Wanawake, Haki za Wazee, Haki za Makundi Madogo katika Jamii, Haki ya Elimu na
Kujifunza, Haki ya kupata habari, Haki na uhuru wa habari na vyombo vya habari
na kadhalika.
·
URAIA
Wananchi wengi
walipendekeza kuwa suala la Uraia libainishwe wazi kwenye Katiba. Tume
imependekeza kwa kutaja Raia wa Jamhuri ya Muungano na haki zake.
·
MIKOPO NA DENI LA TAIFA
Ndugu
Wananchi,
Wananchi walizungumzia suala la uwepo wa Ukomo wa nchi kukopa na uwepo wa
utaratibu wa kulipa Deni la Taifa ili kuilinda Nchi isiwe na deni kubwa. Kwa
kuzingatia maoni ya Wananchi, Tume imependekeza kuwa, Serikali itawajibika
kutoa taarifa Bungeni kuhusu Mikopo kwa kuainisha kiasi cha deni lililopo, riba
yake na matumizi ya fedha za Mikopo na utaratibu wa kulipa Madeni ya Taifa.
·
MFUMO WA UTAWALA
Kuhusu utawala, Tume
inapendekeza Tanzania iendelee na mfumo wa Jamhuri kwa maana ya nchi
inayoongozwa na Rais Mtendaji ambaye ni Mkuu wa nchi, Kiongozi wa Serikali na
Amiri Jeshi Mkuu.
·
UCHAGUZI WA RAIS
o
Umri wa kugombea Urais
Tume ilipokea maoni
yanayokinzana kuhusu umri wa mwananchi kugombea Urais. Baadhi walipendekeza mtu
akishakuwa na sifa ya kupiga kura awe pia na sifa ya kugombea Urais. Umri wa
mtu kuruhusiwa kupiga kura ni miaka 18. Wengine walipendekeza umri uliopo
kwenye Katiba wa mtu kugombea Urais, yaani kuanzia miaka 40 na kuendelea,
uendelee kubaki kama ulivyo.
Wengine walisema Umri wa mtu kuruhusiwa kugombea Urais uwe miaka 35 au miaka 50
na kuendelea.
Tume imeyachambua maoni yote hayo, ikafanya utafiti kwa kupitia Katiba za Nchi
zingine na uhalisia wa watu wanaogombea na kuchaguliwa kuwa Marais katika Nchi
mbalimbali Duniani ambazo zingine zimeruhusu wagombea wa nafasi ya Urais kuwa
na umri chini ya miaka 40.
Wengi walioomba kugombea nafasi hiyo walikuwa na umri wa miaka 40 au zaidi.
Kwa kuzingatia maoni ya wananchi, utafiti na hali halisi, Tume inapendekeza
Rais aendelea kuchaguliwa na wananchi na pamoja na sifa nyingine, mtu anayeomba
urais asiwe chini ya miaka 40.
Uchaguzi wa Rais itakuwa kama ilivyo sasa, yaani mgombea Urais atakuwa na
mgombea mwenza kwa utaratibu kama ilivyo sasa. Isipokuwa, Tume imependekeza Mgombea
Urais anaweza kupendekezwa na Chama cha Siasa au kuwa Mgombea Huru.
Mgombea wa nafasi ya Rais atatangazwa kuwa mshindi iwapo atakuwa amepata
kura zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote zilizopigwa.
Hata hivyo, matokeo ya uchaguzi wa Rais yanaweza kulalamikiwa Mahakamani,
lakini siyo kila mtu anaweza kufungua kesi. Wanaoweza kufungua kesi ni wagombea
Urais. Aidha, ni Mahakama ya Juu pekee ndiyo itakuwa na Mamlaka na uwezo wa
kusikiliza malalamiko kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais na shauri lazima
liamuliwe ndani ya mwezi mmoja, yaani siku therathini.
Rais aliyeshinda ataapishwa siku thelathini tangu alipotangazwa kuwa mshindi
au kuthibitishwa na Mahakama.
·
MADARAKA YA RAIS
Ndugu
Wananchi,
Tume inapendekeza kwamba, Rais abaki na madaraka ya uteuzi wa viongozi wa ngazi
za juu. Hata hivyo inapendekezwa Rais ashirikiane na taasisi na vyombo vingine
katika uteuzi. Kwa mfano:
Uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri, Rais atateua na Bunge
litathibitisha.
Kuhusu Jaji Mkuu na Naibu Jaji Mkuu Rais atawateua kutokana na majina ya
watu waliopendekezwa na Tume ya Uutumishi wa Mahakama na baada ya hapo Bunge
litathibitisha.
Kuhusu Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama inapendekezwa kianzishwe
chombo kipya kitakachoitwa Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa, ambalo kati ya
majukumu yake itakuwa ni kumshauri Rais kuhusu uteuzi wa Wakuu wa vyombo vya
ulinzi na usalama.
Kuhusu Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu watateuliwa na Rais
kutokana na mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma.
·
KINGA YA RAIS
Tume baada ya kupitia
maoni ya Wananchi, inapendekeza Rais abaki na kinga kama ilivyo sasa na anaweza
kushitakiwa na Bunge kama ilivyo Katiba ya sasa.
·
IDADI YA MAWAZIRI
Inapendekezwa Rais
aunde Serikali ndogo iliyo na Mawaziri wasiozidi kumi na tano na
mawaziri hao wasiwe wabunge. Mawaziri hawatahudhuria vikao vya Bunge isipokuwa
kama watahitajika kutoa ufafanuzi kwenye kamati za Bunge.
·
BUNGE
Ndugu
Wananchi,
Kuhusu Bunge kutakuwa na wabunge wa aina mbili. Kutakuwa na Wabunge wa
kuchaguliwa na wabunge watano wa kuteuliwa na Rais kuwakilisha Watu
wenye Ulemavu.
Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili mmoja mwanamke na mwingine
mwanamume.
Tume inapendekeza kwamba, Mbunge akifukuzwa na Chama cha Siasa abaki kuwa
Mbunge lakini akihama Chama atapoteza Ubunge wake.
Inapendekezwa ukomo wa Ubunge uwe vipindi vitatu vya miaka mitano mitano. Hata
hivyo, wananchi wanaweza kumwondoa mbunge wao kabla ya mwisho wa kipindi
chake.
Inapendekezwa pia kusiwepo na uchaguzi mdogo isipokuwa kama nafasi
inayokuwa wazi inatokana na Mbunge huru ndipo utafanyika uchaguzi mdogo kujaza
nafasi hiyo, lakini kama nafasi ikiwa wazi kutokana na Mbunge wa Chama cha Siasa
basi nafasi hiyo, ijazwe na mtu kutoka Chama hicho.
Inapendekezwa Spika na Naibu Spika wasitokane na Wabunge na wasiwe Viongozi
wa vyama vya Siasa.
·
TUME YA UCHAGUZI
Tume imefanya
uchambuzi wa maoni ya wananchi kuhusu Tume ya Uchaguzi. Tume inapendekeza jina
la tume liwe Tume Huru ya Uchaguzi. Tume pia inapendekeza sifa za
wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ziwekwe kwenye Katiba. Wajumbe wa Tume Huru ya
Uchaguzi watapatikana kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizoainishwa ndani
ya Katiba kwa kuomba. Majina ya waombaji yatachambuliwa na Kamati ya Uteuzi
ambayo Mwenyekiti wake atakuwa Jaji Mkuu na wajumbe wengine sita ambao ni
Majaji Wakuu wa nchi Washirika, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Maspika
wa Mabunge wa nchi Washirika na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu.
Kamati ya uteuzi itapendekeza majina ya watu wanaofaa kwa Rais ambaye atateua
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wengine. Bunge litathibitisha uteuzi
wao. Wabunge na viongozi wa aina hiyo hawatakuwa na sifa za kuwa wajumbe wa
tume ya uchaguzi.
Inapendekezwa Tume huru ya Uchaguzi isimamie masuala ya uchaguzi, kura ya
maoni na Usajili wa Vyama vya Siasa.
·
MAHAKAMA
Kuhusu Mahakama
inapendekezwa kuanzishwa kwa Mahakama ya Juu (Supreme Court) Majaji wa Mahakama
ya Juu na Mahakama ya Rufani watateuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume
ya Utumishi wa Mahakama.
·
MUUNDO WA MUUNGANO
Ndugu
Wananchi,
Suala la muundo wa Muungano ndilo lililokuwa gumu kuliko masuala yote.
Tume ilitumia muda mwingi kuchambua maoni ya wananchi. Pamoja na kwamba hadidu
za rejea zilielekeza Tume kuzingatia uwepo wa Muungano, baadhi ya wananchi
walitoa maoni kwamba Muungano uvunjwe na Tume iliyapokea maoni hayo. Licha ya
kwamba waliotaka kuvunjwa muungano walikuwa wachache sana, Tume ilichambua
sababu walizotoa na kuridhika kwamba hazikuwa na uzito.
Wananchi walio wengi walitaka Muungano uendelee. Kati yao wapo waliopendekeza
Muungano wa Serikali moja, Serikali mbili, Serikali tatu, Serikali nne na
muungano wa mkataba. Sababu za wale waliopendekeza Serikali nne hazikuwa na
uzito, kwa hiyo Tume ikaamua kutopendekeza muundo huo.
Wananchi waliopendekeza Serikali moja walikuwa wachache lakini sababu zao
zilkuwa na uzito. Hata hivyo, Tume kwa kuzingatia hali halisi iliona ni
changamoto kubwa kuwa na Muungano wa Serikali Moja.
Wananchi waliopendekeza Muungano wa Mkataba walikuwa wengi (hasa wananchi wa
Zanzibar) na sababu zao zilikuwa na uzito. Lakini uchambuzi wa Tume ilionekana
wazi kwamba ili kupata mkataba lazima kwanza kuwe na nchi mbili huru kabisa
lakini hakukuwa na mazingira ya uhakika ya kupata mkataba wa muungano. Tume
iliona kuna changamoto ya muungano kuvunjika ingawa waliotoa maoni walisisitiza
muungano ubaki. Hivyo, Tume iliamua kutopendekeza muundo huo.
Wananchi waliopendekeza Tanzania iendelee na Muundo wa sasa wa Serikali mbili
walikuwa wengi na sababu zao zilikuwa nzito. Hata hivyo, wananchi katika kundi
hili walipendekeza mabadiliko mengi na makubwa. Tathmini ya Tume ilionyesha
kwamba isingewezekana kufanya mabadiliko yote yaliyopendekezwa.
Wananchi waliopendekeza muundo wa Serikali tatu walikuwa wengi kuliko makundi
yote. Sababu zao zilikuwa nzito lakini pia kulikuwa na changamoto nyingi na
nzito. Pamoja na maoni ya wananchi Tume ilirejea sababu za kupendekeza muundo
huu zilizotolewa na Tume zilizopita na Tafiti zilizofanywa na Tume kuhusu aina
mbalimbali za Muungano. Baada ya yote hayo Tume ilifikia uamuzi wa kupendekeza mfumo
wa Serikali tatu. Yaani Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanzania
Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
·
ORODHA YA MAMBO YA MUUNGANO
Ndugu
Wananchi,
Tume imependekeza katika Rasimu ya Katiba kuwa orodha ya Mambo ya Muungano yawe
7 badala ya 22 yaliyopo sasa.
Mambo ya muungano yanayopendekwa ni:
1.
Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2.
Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
3.
Uraia na Uhamiaji
4.
Sarafu na Benki Kuu
5.
Mambo ya Nje
6.
Usajili wa Vyama vya Siasa
7.
Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya Kodi yatokanayo na
Mambo ya Muungano.
·
BENKI KUU
Kwa kuwa Tume
imependekeza Muungano wa Shirikisho kutokana na uzito wa maoni ya wananchi.
Hivyokutakuwa na Benki Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakayokuwa na wajibu
wa kusimamia masuala ya Sarafu na Fedha za Kigeni na Benki za Washirika wa
Muungano.
·
BENKI ZA SERIKALI ZA WASHIRIKA
Kutokana na pendekezo
la kuwepo kwa Serikali ya Shirikisho la Nchi tatu, inapendekezwa kuwepo kwa
Benki zitakazokuwa na jukumu la kutunza akaunti ya fedha za Serikali za kila
Mshirika wa Muungano na kuzisimamia benki za biashara katika mamlaka zao.
·
BAADHI YA MAMBO AMBAYO HAYAMO KWENYE RASIMU YA KATIBA
o
Serikali ya Majimbo
Ndugu
Wananchi,
Tume ilipokea maoni kuhusu mambo mengine muhimu ambayo hayamo katika rasimu
hii. Moja ya mambo hayo ni Serikali za Majimbo. Tume ilichambua maoni na
sababu za wananchi kupendekeza Serikali za Majimbo lakini Tume ilibaini
changamoto nyingi na ikaamua kutopendekeza muundo huu.
Kwanza, baada ya kuamua kupendekeza Muundo wa Muungano wa Serikali Tatu,
ilionekana ni dhahiri kuongeza ngazi nyingine ya Serikali ingeleta gharama
kubwa. Serikali nyingine kumi zingekuwa na Wakuu wa Majimbo, Mabaraza ya
Mawaziri na Mabunge na gharama yake ingekuwa kubwa.
Pili, katika kutembelea nchi Tume ilishuhudia dalili za wazi za mivutano ya
Udini, ukanda,malalamiko ya upendeleo wa baadhi ya maeneo na ukabila.
Dalili zilikuwa wazi kwamba utawala wa majimbo ungeirudisha nchi kwenye
utawala utakaoigawa nchi kwa misingi ya ukabila, udini na ukanda na kuzigawa
rasilimali za taifa kikanda na hivyo kuleta tofauti kubwa ya kimaendeleo katika
nchi.
·
Mahakama ya Kadhi
Ndugu
wananchi,
Jambo la pili ni mahakama ya kadhi. Tume ilipokea maoni mengi kuhusu suala
hili. Baadhi ya wananchi walitaka mahakama ya kadhi iingizwe kwenye Katiba na
wengine walipinga. Baada ya kuamua kuwa Muundo wa Muungano uwe wa Serikali
Tatu, Tume iliona kuwa Mahakama ya Kadhi siyo suala la Muungano na
imeliacha ili lishughulikiwe na Washirika wa Muungano.
Hata hivyo ilionekana kuwa suala siyo kuwapo au kutokuwapo kwa mahakama
ya kadhi. Mahakama hizo zinaweza kuwapo bila ya kuwa katika Katiba.
Zanzibar kuna mahakama ya kadhi bila kuingizwa kwenye Katiba ya Zanzibar. Kwa
kutumia uzoefu huo hata Tanzania Bara inaweza kupata ufumbuzi wa suala hili.
·
Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya
Jambo
la Tatu ni Kuwepo au kutokuwepo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya. Baadhi ya Wananchi
walitaka Wakuu wa Mikoa na Wilaya wasiwepo, wengine walitaka Wakuu wa Mikoa na
Wilaya waendelee kuwepo lakini wachaguliwe na wananchi na waengine wakasema
wawepo na waendelee kuteuliwa na Rais kama ilivyo sasa. Tume ilitafakari kuhusu
suala hili na kuamua kwamba siyo suala la Muungano na kwa kuwa Muundo wa
Muungano imependekezwa uwe wa Serikali Tatu, Tume iliona suala la uwepo au
kutokuwepo na namna ya upatikanaji wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya lishughulikiwe
na Washirika wa Muungano.
·
Serikali za Mitaa
Kuhusu
Serikali za Mitaa,
Tume ilipokea maoni kutoka kwa wananchi kuhusu kuziimarisha Mamlaka za Serikali
za Mitaa kwa kuzipatia uhuru kamili wa kujiamulia mambo yao bila kuingiliwa na
Serikali Kuu. Tume ilitafakari suala hili na kuamua kwamba siyo jambo la
Muungano na hivyo, litashughulikiwa kwenye Katiba za Washirika wa Muungano.
·
Uraia wa Nchi mbili
Ndugu
Wananchi,
Jambo la tatu ni Uraia wa Nchi mbili. Tume ilipokea maoni kutoka kwa wananchi
mbalimbali kuhusu kuwekwa kwenye Katiba suala la Uraia wa nchi mbili. Baada ya
kufanya uchambuzi kwa kutengenisha mambo yapi ni ya Kikatiba na yapi yanaweza
kutekelezwa bila kuingizwa kwenye Katiba bali kwenye Sheria inayohusu jambo husika,
Tume imependekeza kuwa suala la Uraia wa nchi mbili linaweza kuwekwa kwenye
Sheria badala ya kuwekwa kwenye Katiba. hii ni kwa sababu kutokana na
utafiti uliofanywa na Tume, suala hilo linaweza kubadilika wakati wowote na
hivyo likiwa kwenye Katiba linaweza kuifanya Katiba kubadilishwa mara kwa mara.
MWISHO
Naomba nichukue fursa
hii kwa niaba ya Tume kuwashukuru Watanzania wote kwa kushiriki kikamilifu
katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba, kuanzia hatua ya kutoa maoni na
kuwachagua wawakilishi wenu watakaopata fursa ya kuipitia, kuijadili na
kuitolea maoni Rasimu ya Katiba. Ushirikiano huu ulikuwa muhimu sana kwa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba hasa ukizingatia kuwa lengo ni kupata Katiba Mpya
ambayo itaakisi ndoto na matakwa ya Wananchi wa Tanzania.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, inatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar:
1.
Kwa
kuipatia vifaa afisi na mahitaji ya lazima
2.
Kwa
kuiwezesha Tume kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu,
3.
Kwa
kutokuingilia Uhuru wa Tume wakati wa Utekelezaji wa Majukumu yake na
4.
Kutoa
Wataalam wenye Weledi, Mahiri, Makini na Waadilifu ambao wameunda
Sekretarieti ya Tume.
Ndugu
Wananchi,
Shukrani za pekee ziwaendee:
1.
Wakuu
wa Mikoa,
2.
Wakuu
wa Wilaya,
3.
Wakurugenzi
/ Makatibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa,
4.
Makamanda
wa Polisi wa Mikoa na Wilaya,
5.
Watendaji
wa Kata, Vijiji, Mitaa na Masheha.
Kwa kuisaidia Tume
kutekeleza Majukumu yake kwa ufanisi. Aidha, tunazishukuru Asasi za Kiraia,
Taasisi, Jumuiya za Kidini, Vyama vya Siasa na Makundi mbalimbali kwa namna
walivyoshiriki katika kuhamasisha wananchi kushiriki katika kutoa maoni.
Mwisho ingawa siyo kwa umuhimu, Tunawashukuru Wanahabari wote kwa kazi nzuri
waliyoifanya ya kuisaidia Tume kufikisha taarifa mbalimbali za Tume kwa
Wananchi na katika kuhamasisha Wananchi kushiriki katika mchakato wa Mabadiliko
ya Katiba.
Nachukua nafasi hii kuwaomba Wananchi kupitia Mabaraza ya Katiba ya Wilaya,
Mabaraza ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye Malengo yanyofanana
kushiriki vyema, kwa umakini, utulivu na kwa amani katika hatua hii ya
kuipitia, kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba.

TOA MAONI YAKO