Wednesday, March 6, 2013

YANGA

Kikosi cha Young Africans Sports Club

YANGA KUIVAA TOTO AFRICAN JUMAMOSI

Baada ya kuichapa timu ya Kagera Sugar kwa bao 1-0 katika mchezo uliopita mwishoni wa wiki, timu ya Young Africans Sports Club itashuka dimbani siku ya jumamosi kucheza na timu ya Toto Africans ya kutoka jijini Mwanza, mchezo utakaofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia majira ya saa 10 jioni.
Read more...
 
Kikosi cha Young Africans kilipokuwa kambini nchini Uturuki

YANGA YAENDELEA KUJIFUA

Kikosi cha timu ya Young Africans leo kimeendelea na mazoezi asubuhi katika uwanja wa mabatini Kijitonyama kujiandaa na mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi ya Vodacom dhidi ya timu ya Toto African siku ya jumamosi  Machi 09 ,2013 katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Read more...
Kikosi cha Young Africans kilipokuwa katika kambi ya mafunzo nchini Uturuki

YANGA YAENDELEA NA MAZOEZI

Kikosi cha timu ya Young Africans leo kimeendelea na mazoezi katika katika uwanja wa mabatini Kijitonyama kujiandaa na mchezo namba 135 wa mzunguko wa pili wa Ligi ya Vodacom dhidi ya timu ya Toto African siku ya jumamosi  Machi 09 ,2013 katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Read more...
Haruna Niyonzima (wa pili kutoka kushoto) mfungaji wa bao la ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Kagera Suagr

YANGA YAZIDI KUJIKITA KILELENI , YAICHAPA KAGERA SUGAR 1-0


Bao lililofungwa na kiungo wa kimataifa raia wa Rwanda Haruna Niyonzima dakika ya 66 ya mchezo, limeifanya timu ya Young Africans kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom nchini Tanzania bada ya kuichapa timu ya Kagera Sugar kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Read more...


















No comments:

Post a Comment