Kenyatta atamba matokeo ya awali uchaguzi nchini Kenya
Uhuru Kenyatta, mgombea urais wa muungano wa Jubilee
Wakati wakenya wakiendelea kusubiri kutangazwa kwa matokeo ya
jumla ya uchaguzi mkuu nchini humo mara baada ya zoezi la kupiga kura
kukamilika hapo jana,matokeo ya awali ya uchaguzi huo yanaonesha kuwa
mgombea urais kwa tiketi ya muungano wa Jubilee, Uhuru Kenyatta
anaongoza kwa asilimia 54.60% akifuatiwa na Raila Odinga wa muungano wa
Cord mwenye asilimia 40.30% matokeo ambayo hata hivyo yanabadilika
kadiri muda unavyozidi kusonga.
Usiku kucha matokeo ya uchaguzi huo yameendelea kukusanywa
kutoka katika vituo vya kupigia kura huku karibu theluthi ya vituo vya
kupigia kura vikituma matokeo majira ya asubuhi leo Jumanne.
Wapiga kura hiyo jana walisimama katika mistari kadhaa yenye umbali wa mamia ya mita wakiendelea kungoja kwa amani nje ya vituo vya kupigia kura kukamilisha zoezi hilo katika uchaguzi unaodaiwa kuwa na utata kuliko chaguzi zilizowahi kutokea nchini Kenya.
Aidha kabla ya zoezi la kupiga kura vurugu za umwagaji damu zilitokea katika eneo la Pwani mjini Mombasa ambapo polisi sita na washambuliaji sita waliuawa katika mashambulizi mawili tofauti, huku mabomu kadhaa yakilipuliwa na kumjeruhi mtu mmoja huko Mandera mpakani na Somalia.

No comments:
Post a Comment