Posted: 11th November 2012 by Ajuaye Mcha
BASHE amesema kwa mfumo wa kiuongozi ndani ya CCM ni mwendawazimu pekee anayewaza kwamba suala hilo linawezekana na kwamba kauli iliyotolewa na mmoja wa kada wa chama hicho AGUSTINO MATEFU juu ya kumpunguzia kura rais ni mkakati uliopangwa ili kumdhalilisha Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Ili kuondoa utata wa juu ya anayehusika kuwatuma vijana wanaoeneza chuki na makundi ndani ya CCM, Bashe amemtaja mmoja wa Mawaziri wa awamu ya hii kwamba anaendesha mchezo mchafu ili kujisafishia njia ya Urais 2015.
Wakati hayo yakitokea tayari maandalizi ya shughuli za ufunguzi wa mkutano mkuu zimekamilika na wajumbe wameshawasili Dodoma tayari kuwachagua viongozi mbalimbali katika Ukumbi wa mikutano wa Kizota.
Namkariri Bashe akisema “anaewatumia hawa vijana ni Benard Membe ndio anaefanya huu mchezo wa kihuni ambao amekua akiufanya kwa muda mrefu ndani ya chama chetu, nilisema aache michezo hii… ameweza kubakia kwenye siasa za CCM kwa muda mrefu kwa kugawa watu, huu ni sehemu ya mpango wake amekua akitumia vijana hawa, kama mlikuepo hapa Dodoma wakati tunafanya uchaguzi wa vijana alikuja mpambe wake mkubwa kabisa ndugu Nyalandu kutuletea vurugu katika ukumbi wa uchaguzi”
Kwenye line ya pili Bashe amesema “nataka kutumia fursa hii kumwambia Membe kwamba sina mpango wa kumnyima kura rais Jakaya bali nina mpango wa kumnyima yeye kura, kura yangu hatopata, kura ya wale wote wanaoweza kunielewa hatopata na kama atashinda NEC atashinda kwa kura za watu wengine na sio kura ya Hussein Bashe, kwa muda mrefu Membe amekua akisurvive kwa siasa za unafiki na uongo ndani ya chama chetu na bahati mbaya viongozi wanafamu, ni mwendawazimu tu anaeweza kufikiri ndani ya chama chetu tunaweza kufikiria tumuweke mwenyekiti mwingine na rais mwingine, huyo atakua aidha ana matatizo ya akili ama sio mwanachama wa CCM”
Kuhusu kipeperushi, Bashe amesema “kwanza kipeperushi hicho hata kukiona sijakiona, hakuna mpango huo na sijawahi kufikiri kuendesha hujuma/mkakati dhidi ya rais Jakaya Mrisho Kikwete”
No comments:
Post a Comment