Monday, November 12, 2012

TAZAMA MATUKIO YOTE HAPA KATIKA PICHA MECHI KATI YA SIMBA NA TOTO AFRICA.

Kipa Wilbert Mweta wa Simba akijaribu kuokoa mpira kwa mguu bila mafanikio katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Toto Africans ya Mwanza, iliyoshinda 1-0.  

Mpira upo nyavuni
Mfungaji wa bao la Toto akipongezwa na wewnzake



Kocha wa Simba, Milovan Cirkovick akiangalia saa yake dakika zikiyoyoma timu yake imelala

Wachezaji wa Toto wakinywa maji

Hatari kwenye lango la Toto

Komabil Keita wa Simba akionyesha ubabe na Suleiman Kibuta wa Toto. walitaka kupigana

Okwi anateleza

Cheki jamaa alivyomkaba Sunzu

Kiemba anateleza

Okwi katika mishe

Ulinzi mkali

Jonas Mkude anatoa pasi

Hoi, kocha Milovan kushoto na wachezaji wake kulia Mkude na Shomary Kapombe

Hatari kwenye lango la Toto

Sunzu akishughulika

Mussa Said Kimbu akichuana na Kiemba anayeelekea kuangukia mpira

Okwi alipangua safu yote ya ulinzi ya Toto, lakini akashindwa kufunga

Okwi anawatoka mabeki wa Toto

Mwinyi Kazimoto anaambaaa

keita anamiliki mpira kulia

Emmanuel Swita anaosha

Refa Judith Gamba akimuinua mchezaji wa Toto 

Sunzu anataka kuingia yeye nyavuni baada ya kipa wa Toto kudaka mpira

Haruna Chanongo na Mohamed Hussein wa Toto

Chanongo akidhibitiwa

Kikosi cha Toto leo

Kikosi cha Simba leo

Kipa wa Toto, Erick Ngwengwe akidaka mpira mbele ya Okwi na Sunzu

Ngwengwe akidaka mpira mbele ya Sunzu

Ngwengwe akidaka mpira mbele ya Okwi..

HUYU NDIE ANASEMA SIASA ZA WAZIRI MEMBE NI ZA KINAFIKI, ANAFANYA MCHEZO WA KIHUNI NA ANAHUSIKA KUMCHAFUA RAIS KIKWETE

Posted: 11th November 2012 by Ajuaye Mcha 

0
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi CCM, HUSSEIN BASHE
Mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa wa CCM Hussein Bashe amefikia hatua hiyo ya kumtaja Benarnd Membe kutokana na vipeperushi vinavyodaiwa kusambazwa Dodoma kwamba Bashe na kundi lake limepanga kuwashawishi wajumbe wa mkutano mkuu kupiga kura za maruhani ili Rais Kikwete asiwe na uongozi wa kofia mbili ikiwemo ile ya Uenyekiti wa Taifa wa CCM.
BASHE amesema kwa mfumo wa kiuongozi ndani ya CCM ni mwendawazimu pekee anayewaza kwamba suala hilo linawezekana na kwamba kauli iliyotolewa na mmoja wa kada wa chama hicho AGUSTINO MATEFU juu ya kumpunguzia kura rais ni mkakati uliopangwa ili kumdhalilisha Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Ili kuondoa utata wa juu ya anayehusika kuwatuma vijana wanaoeneza chuki na makundi ndani ya CCM, Bashe amemtaja mmoja wa Mawaziri wa awamu ya hii kwamba anaendesha mchezo mchafu ili kujisafishia njia ya Urais 2015.
Wakati hayo yakitokea tayari maandalizi ya shughuli za ufunguzi wa mkutano mkuu zimekamilika na wajumbe wameshawasili Dodoma tayari kuwachagua viongozi mbalimbali katika Ukumbi wa mikutano wa Kizota.
Namkariri Bashe akisema “anaewatumia hawa vijana ni Benard Membe ndio anaefanya huu mchezo wa kihuni ambao amekua akiufanya kwa muda mrefu ndani ya chama chetu, nilisema aache michezo hii… ameweza kubakia kwenye siasa za CCM kwa muda mrefu kwa kugawa watu, huu ni sehemu ya mpango wake amekua akitumia vijana hawa, kama mlikuepo hapa Dodoma wakati tunafanya uchaguzi wa vijana alikuja mpambe wake mkubwa kabisa ndugu Nyalandu kutuletea vurugu katika ukumbi wa uchaguzi
Kwenye line ya pili Bashe amesema “nataka kutumia fursa hii kumwambia Membe kwamba sina mpango wa kumnyima kura rais Jakaya bali nina mpango wa kumnyima yeye kura, kura yangu hatopata, kura ya wale wote wanaoweza kunielewa hatopata na kama atashinda NEC atashinda kwa kura za watu wengine na sio kura ya Hussein Bashe, kwa muda mrefu Membe amekua akisurvive kwa siasa za unafiki na uongo ndani ya chama chetu na bahati mbaya viongozi wanafamu, ni mwendawazimu tu anaeweza kufikiri ndani ya chama chetu tunaweza kufikiria tumuweke mwenyekiti mwingine na rais mwingine, huyo atakua aidha ana matatizo ya akili ama sio mwanachama wa CCM”
Kuhusu kipeperushi, Bashe amesema “kwanza kipeperushi hicho hata kukiona sijakiona, hakuna mpango huo na sijawahi kufikiri kuendesha hujuma/mkakati dhidi ya rais Jakaya Mrisho Kikwete”

PICHA ZA FAINALI YA BONGO STAR SEARCH 2012.


Posted: 11th November 2012 by AJUAYE MCHA
0
Walter.
.
Hii ndio ilikua Top 5.
.
Linah na Amini waliperform pia.
Walter na mc Sizza na Vanessa Mdee.
.
Top 3
.
Zawadi kwa mshindi wa kwanza.
Baada ya Walter kutangazwa mshindi.

DIAMOND NA OMMY DIMPOZ WAPATA AJALI!!


gari la Diamond baada ya ajali
Jumamosi wiki iliyopita, msanii Diamond alipata ajali barabara ya chole alipokua akitokea Sleepway  kushoot video ya pini lake jipya lenye zengwe hatari tangu litoke (nataka kulewa).
"mida kama ya saa tatu tatu hivi kasoro,nikiwa narudi home, napita mitaa ya arabela mbele kuna Rav 4 mkono wa kulia kuna pikipiki nilikua nataka ku overtake pikipiki, nikataka niikwepe pikipiki kwapembeni kulikua na shimo, nikajaribu kurudi kwenye lami ndio nikaenda kugongana na Rav4..lakini hakuna mtu alieumia,"
"unajua mwisho wa mwaka tena huu, watu wanatoa kafara zao bahati mbaya zinatukuta watu kidogo manguli hazituumizi sana, wepesi wepesi wangeondoka mzima mzima kabisa wangebaki story tu alikufa na ajali, sababu hata ukitazama wanaopata ajali ni wale wanao hit, zinafeli hahhaaaaa i was just kidding." ameema  Diamond
Na gari la Ommy Dimpoz amepata ajali sasa hivi na limebebwa na Break Down" alisema jamaa."
nikaona kuthibitisha hili, Ommy mwenyewe atafunguka na baada ya kuvutiwa waya akafunguka
 
"nikweli nimepata ajali maeneo ya Millenium Tower nikiwa naelekea  kwa P Funk nilikua nna session kidogo , ghafla aliekuwa mbele yangu akafunga break na nikaingia kwa nyuma

SEAN PAUL APAGAWISHA KAMPALA...UGANDA!!


Sean Paul akiimba kwa hisia kali

Sean Paul akiwaimbia mashabiki
Sean Paul akiwa stejini
Umati wa mashabiki wakimshangilia Sean Paul Stejini

Flowers wa jiji la Kampala wakishow love kwa Sean Paul

Sean Paul katika mitaa ya jiji la kampala

Sean Paul akiwasili Kampala 

  Mwanamuziki kutoka Jamaica Sean Paul, weekend iliyopita, katika Viwanja vya Cricket Lugogo jijini Kampala nchini Uganda, ameacha burudani ya Historia kama wengi walivyotarajia.
Sean Paul amekua kipenzi cha mashabiki wa muziki nchini Uganda.
Mashabiki wa Sean Paul, walichukua muda wa saa tano kumsubiri Mwanamuziki huyo katika show iliyodhaminiwa na Club Beer.
Baadhi ya wanamuziki waliopanda stejini ni pamoja na Michael Ross, Young Mulo, Navio, Peter Miles, Menshan, Radio na Weasel.
Kulikuwepo na tatizo na mitambo kabla ya Sean Paul kupanda jukwaani, ingawa hapo baadaye mambo yalienda sawa.
Mara tu baada ya Sean Pauil kupanda jukwaani, zilisikika shangwe za mashabiki, nyingi zikitoka kwa wadada wa Kampala.
Mamia wamepongeza maandalizi ya Show hiyo, iliyoandaliwa na kampuni ya  Talent Africa, yake Ali Alibhai kwa ushirikiano na Kibo Media na kudhaminiwa na Club Beer.
Kibao “Always on my mind”  ndicho kilicho wapagawisha wapenzi wa nyota huyo wa muziki wa Dancehall.
Vibao vingine vilivyopigwa ni pamoja na Give it to you, watch them roll, back it up,