Friday, July 5, 2013

Sumaye azindua ziara Dsj



 Posted on 5jully 2013
Waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Fredrick Sumaye amezindua safari ya kuelekea nchini Kenya ya wanafunziwa chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam (DSJ).na kuwataka kutumia fursa hiyo kuitangaza zaidi Tanzania

Sumaye amezindua safari hiyo chuoni hapo na kuwataka wanafunzi kwenda kujifunza utalii na jinsi ya kumudu maisha pasipo kutegemea kuajiriwa na serikali bali kujiajiri wenyewe kwa elimu waliyoipata.

Pia aliwataka wanafunzi hao kujifunza mazingira ya Kenya jinsi yalivyo tofauti na ya hapa kwetu Tanzania na hata watalii wengi huvutiwa   kutembelea  nchi hiyo na  kuwaongezea pato lao la taifa.

Alisema kuwa nchi ya Kenya iko juu kiuchumi tofauti na Tanzania  hivyo  basi    mnavyokwenda ni vizuri mkajijifunze kutoka kwa wenzetu na kuja kuyafanyia kazi kwa ufasaha zaidi ili kuleta maendeleo  kwa taifa Letu.

Sumaye aliendelea kusema wafanyakazi wa Kenya ni wafanyakazi waamifu  na wachapa kazi sana tofauti na Tanzania hivyo basi nasi  tukajifunze vitu hivyo katika ziara hii ili tuweze kulijenga taifa letu.

Kwa upande wa biashara alisema Kenya wanauwezo mkubwa wa kufanya biashara za nje tofauti na Tanzania hivyo nasi tukaifunze mbinu hizo za kibiashara kutoka kwao ili tuje kuwa mabalozi hapa nchini..

Ziara hiyo inatarajiwa kuwa ya siku tano kuanzia taehe 9 mwezi wa saba hadi tarehe 14 ambapo malengo ya ziara hiyo ni kujifunza utamadunui wa nje pamoja na kujifunza elimu yao ilivyo tofauti na Tanzania.

Tuesday, July 2, 2013

Simba yamuacha Kaseja

Suala hapa sio kuachwa kwa Kaseja bali Simba walipaswa kuendelea kumuamini  kwani bado ana mchango kwa simba na Taifa stars kutokana na mchango wake ambao amekuwa akiutoa ndani na nje ya uwanja


Kimsingi mchezaji akimaliza mkataba wake huwa anakuwa huru kutafuta klabu yoyote endapo klabu yake haitokuwa na nia ya kumwongezea mkataba mpya

Ikumbukwe kua Kaseja ameidakia Simba kwa miaka kumi yenye mafanikio makubwa  na kuiwezesha kubeba mataji mengi ya ligi kuu bara pamoja na kuiwakilisha vizuri katika michuano ya vilabu barani Afrika

Kwani mnamo mwaka 2003 alifanikiwa kuingoza simba kuwandoa mabingwa wa vilabu barani Afrika kwa wakati huo Zamalek ya Misri na bado aliendelea kuiongoza vizuri Simba na Taifa Stars  hali iliyopelekea kuendelea kuwa kipa namba moja hadi hivi leo

Hata hivyo sababu ambazo zimekuwa zikitolewa na  viongozi ni kuwa kiwango cha mchezaji huyo kimeshuka kitendo ambacho kimekuwa kikipingwa vikali na mashabiki wa soka ambao wanadai Kaseja hajachuja kwa kiasi hicho bali kutakuwa kuna chuki kati yake na baadhi ya viongozi

Nao baadhi ya wadau wameliambia gazeti la upendo kuwa Simba watakuja kumjutia kaseja kwani ana mchango mkubwa na hawajamuona golikipa yoyote Tanzania mwenye uwezo zaidi ya yake hivyo basi Simba walipaswa kufikiria kabla ya kufanya maamuzi ya kumuacha.

Emmanuel Bayo mkazi wa Kinondoni amesema Keseja ni golikipa mzuri sana kwa Tanzania kwani licha ya kuisadia Simba kwa muda mrefu amekuwa pia golikipa chaguo la kwanza kwa Taifa Stara hivyo sina shaka naye akiendelea kuidakia Simba.

‘Pia sababu zinazosemwa kuwa amechuja mimi sikubaliani nazo hivyo Simba wanabidi kuendelea kuwa naye na ataendelea kuwasaidia zaidi kutokana na kiwango anachokionyesha uwanjani pindi anapoiwakilisha Simba au Taifa stars’ alisema Bayo

Abubakar Rasul mkazi wa Buguruni alisema alidhani Simba wangeendelea kumuamini Kaeja kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa klabuni hapo hata kama angekuwa amechuja wangepaswa kuwa nae au kumpeleka kozi ya ukocha ili aje awe kocha wa makipa kutokana na mapenzi aliyo nayo juu ya Simba

‘Hali hii itawavunja moyo hata wachezaji wengine wenye mapenzi makubwa na Simba watacheza huku wakijua hata muda wao utakapoisha watatupwa bila kuthaminiwa mchango wao walioutoa kwa Simba’ alisema Rasul

Hivyo basi viongozi wa Simba hasa hawapaswi kuyapuuza maoni wanabidi wayafanyie kazi ili kuweza kuiboresha Simba ili hiƩndele kuwika Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Thursday, June 27, 2013

TRA:Kodi ya magari kulipwa kwa kwa njia ya mtandao kuanzia 1'Julai



Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Benki kuu ya Tanzania (BOT) wamefanya maboresho katika ulipaji kodi kwa njia ya mtandao.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Fedha wa TRA Salehe Mshoro alisema kuanzia Julai mosi TRA na BOT  wataanzisha mfumo wa ukusanyaji kodi utakao unganisha na mifumo ya benki.kuu na benki za biashara.

Alisema kuwa mtu akienda kulipa kodi zile fedha zitakwenda BOT  na papo kwa hapo atapata taarifa kwa njia ya barua pepe  na taarifa zitakwenda kwa haraka TRA zitakazoonyesha kuwa kodi imelipwa.

Alidai kuwa mfumo huu utaondoa migongano ya mara kwa mara na pia watakuwa wamefanya  makubaliano kati ya TRA na wananchi ambao ndio walipa kodi.na pia mfumo huu wamejufanyia majaribu toka mwezi januari.

Aidha alisema mfumo huu utaanza kutumika kwa walipa kodi wakubwa wa malipo yanayoanzia millioni tano(5) ambao hao watakuwa mabalozi kwa wengine wadogo na alisema kumbukumbu zitaingizwa kwenye mamlaka na watapata taarifa.

Mlipa kodi atatakiwa kujisajili kwenye mtandao wa TRA ambao ni www.tra.go.tz akiingia kwenye wwbsite ya TRA anaweza kupata taarifa zake muhimu za usajili na namba za utambulisho na benki yake.


Naye Murugenzi wa mradi Ramadhani Sangeti alisema wamejiunga na mkongo mkubwa wa taifa  na endapo mkongo mkubwa hautapatikana ile mingine itasaidia,

Mategemeo ya TRA ni kuwa utaongeza urahisi wa ulipaji kodi na utaondoa kero za wananchi pia itapunguza muda na kumpunguzia mteja gharama, kwani ni mfumo salama wenye kutoa taarifa kwa wakati.

Mwisho aliwataka walipa kodi pindi watakapopata matatizo yoyote wapige namba za huduma ambazo ni bure  kwa upande wa TTCL na Vodacom ni 08001126 au Tigo ambazo n i 0713800333 na Airtel 0786800000

Saturday, June 22, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

22/06/2013
Na: Simon Mmbando

CUF KUANDAMANA 29 JUNI HADI IKULU,PROF.LIPUMBA KUONGOZA,MAANDAMANO KUPOKELEWA NA RAIS KIKWETE.

Waheshimiwa waandishi wa habari, kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya uongozi wote wa kitaifa wa Chama chetu, naomba kuchukua fursa hii kuwakaribisha Ofisi Kuu ya chama ili tupate fursa ya kuzungumza nanyi na kwa maana hiyo kuzungumza na watanzania kupia kwenu ili ujumbe uliokusudiwa na chama uweze kuwafikia wananchi popote pale walipo.
Tumewaita leo tarehe 22 Juni 2013 tukiwa na agenda moja kuu nayo ni kuwaeleza kwamba Chama cha Wananchi CUF kimeandaa Maandamano ya Amani siku ya tarehe 29 Juni 2013 maandamano ambayo yataanzia eneo la Buguruni kituo cha Mafuta saa nne kamili asubuhi, kupitia barabara ya Uhuru, Mnazimmoja, Bibi Titi, Posta mpya , Aridhi hadi Ikulu.
Maandamano hayo ambayo yataongozwa na Mwenyekiti wa Chama taifa Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, yanatarajiwa kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au mwakilishi wake, na kwamba yanalengo la kufikisha malalamiko ya wananchi kutokana na vitendo vya ukatili vinavyofanywa na jeshi la polisi na jeshi la wananchi ambalo kimsingi taifa letu linaelekea mahali pabaya.
Waheshimiwa waandishi wabari, mtakumbuka tarehe 15 Juni 2013 wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakihitimisha mkutano wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata nne za Arusha, palitokea mlipuko wa bomu uliopoteza maisha ya wananchi wane kwa mujibu wa taarifa za polisi na wengine wengi kujeruiwa vibaya.
Kwa kuwa jambo hili lipo katika hatua za uchunguzi, Chama cha CUF hakikusudii kuingilia uchunguzi unaoendelea lakini tunataka kufikisha ujumbe kwa rais kwamba hii si mara ya kwanza kuundwa kwa tume mbalimbali za uchunguzi hapa nchini. Kinachotusikitisha ni kuwa hata mara baada ya uchunguzi huo, hakuna ripoti inayotolewa hadharani kuonyesha chanzo cha tukio, wahusika na hatua zilizo au zinazotarajiwa kuchukuiliwa.
Tutamtaka Mheshimiwa rais kuhakikisha ripoti ya uchunguzi itokanayo na maafa yaliyotokea Arusha iwekwe wazi na serikali iwachukulie hatua stahiki wale wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo ili iwe funzo kwa wengine au wale wenye kuwa na malengo yanayofanana na hayo kwa kuwa Tanzania ni yetu sote na haitowezekana watu wachache wayachezee maisha ya watu kwa sababu ya kukidhi matakwa binafsi ambayo hayana tija kwa jamii.
Maandamano pia yanalenga kuishinikiza serikali kukomesha vitendo vya kinyama, vitendo vya kijangili vinavyofanywa na Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kuwakamata, kuwatesa, na kubaka wananchi wasio na hatia wa Mkoa wa Mtwara na hasa wanaoishi katika wilaya za Mtwara Mjini, MtwaraVijijini, na Newala huku baadhi yao wakichomewa nyumba zao moto na wengine wakiporwa mali zao.
Waheshimiwa waandishi wa habari, mtakumbuka hivi karibuni pamekuwa na fukuto la suala la gesi katika Mkoa wa Mtwara ambapo baadhi ya maafisa wa Serikali wamekuwa wakipotosha madai ya wananchi ikidaiwa kwamba wananchi wa mkoa huo wamesema hawako tayari kuona gesi yao inatumiwa na wananchi wengine kinyume na wale wa mikoa ya Lindi na Mtwara jambo ambalo si kweli lakini wanayafanya haya ili kuwajengea chuki dhidi ya watanzania wengine ionekane kwamba wananchi wa Mtwara na Lindi ni wabinafsi na wasioitakia mema nchi yetu.
Madai ya wananchi wa Mtwara yanatokana na uzoefu waliokuwa nao katika maeneo yote ambapo pana miradi ya kimaenedeleo itokanayo na maliasili ya nchi, maeneo hayo yamekuwa masikini na watu wachache wamekuwa wanatajirika, walichotaka kufahamu wananchi watanufaikaje na uwepo wa gesi katika maeneo yao kabla ya kuinufaisha nchi mzima kwa kuwa wao ndiyo watakuwa wa kwanza kuathirika ikiwa patatokea hitilafu yoyote itokanayo na uchimbwaji wa gesi hiyo.
Leo tunaweza kujifunza kutokana na uchimbaji wa Dhahabu Geita (GGM), uchimbaji wa Almasi Mwadui Shinyanga, Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Nyamongo na maeneo mengine mengi, nini hali ya maisha ya wananchi wa maeneo hayo.
Pamoja na upotoshwaji wa makusudi uliofanywa na unaoendelea kufanywa na watendaji wa serikali juu ya suala la gesi ya Mtwara, inashangaza hata Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambalo lilionekana awali kutenda haki kwa wananchi wa Mtwara baada ya wananchi kukosa imani dhidi ya Polisi kutokana na wizi na uporaji wa mali za wananchi huku wakichoma moto baadhi ya maduka kwa lengo la kuhalalisha vitendo vya hujuma pamoja na kuchoma moto soko la Nkana Read, Jeshi lililojijengea heshima kwa jamii nalo limeanza kuingia mkumbo wa kuwatesa raia bila makosa.
Mwanzoni mwa wiki hii Mkurugenzi wetu wa siasa wa wilaya ya Mtwara Mjini Mhe. Saibogi ambaye pia ni mwenyekiti wetu wa serikali ya Mtaa alitekwa na wanajeshi na kumpeleka katika Kambi yao iliyopo barabara ya kwenda Nanyamba ambapo walimvua nguo na kumpiga mijeredi usiku kucha bila hatia na kumuachia asubuhi yake huku wakiahidi kuwakamata viongozi wengine wa CUF ili kutoa funzo kwa wale wanaopigania haki za wananchi.
Matukio ya namna hii si ya kuyafumbia macho na yanatengeneza serikali yenye kiburi isiyotokana na maamuzi ya raia. Maisha ya namna hii hayawezi kuendeshwa katika nchi inayojiita huru kama yakwetu na badala yake mambo haya yanatukumbusha enzi za utawala wa kikoloni ambpo CUF kamwe hatupo tayari kuruhusu vitendo vya kishenzi kuona vinafanyika nchini petu.
Tulikianzisha Chama hiki kwa madhumuni ya kuwaunganisha watanzania wote popote walipo, bila kujali itikadi zao, waweze kukataa aina yoyote ya uonevu, ukandamizaji, unyanyasaji, ubaguzi na udhalilishaji wa kisiasa au kiuchumi.
Aidha tuna dhamira ya kulinda, kutekeleza na kuzienzi haki za Binadamu pamoja na kuinua uchumi wa nchi kwa siasa zitumikie uchumi badala ya uchumi kutumikia siasa kama inavyofanyika hivi sasa. CUF tunaamini katika siasa za ustaharabu ambazo zitatuwezesha kuwa na jamii salama yenye mshikamano na ushirikiano katika kuijenga nchi yetu, lakini wenzetu wanatumia upole wetu na ustaharabu wetu kutufanyia vitendo vinavyokiuka utu wa mtu na hatimaye kila aliyepewa mamlaka ya kuongoza sehemu ya nchi yetu anageuka kuwa mfalme na kuamrisha kamata Yule, mpe kesi Yule na mwache Yule. Uvumilivu wetu usiwe mtaji kwa CCM na serikali yake kutufanya watakalo, nasi ni binadamu.
Waheshimiwa waandishi wa habari, maandamano yetu yanalenga pia kuitaka serikali kuwasikiliza wananchi wa Mtwara kwa kukaa nao chini, kujua hoja zao na kutoa ufafanuzi pale patakapobidi, sisi tunaamini wanazo hoja za msingi na wakisikilizwa serikali itaona namna ya kuzifanyia kazi hoja hizo badala ya kukurupuka na kutoa kauli za kibabe eti hawa wanachochewa na vyama vya siasa au pana watu wasioitakia mema nchi ndiyo wanachochea, kauli hizi zinajenga chuki na zanakosa uzalendo wa taifa. Haiwezekani hao wanaojiita ndiyo wazalendo halisi wawe wanaifidi nchi alafu tuendelee kukaa kimya kama vile wananchi wa kusini ni watu wasioweza kufikiri na kupambanua baya na zuri.
Wakati wananchi hawa walipopeleka maombi yao kupitia kwa Mhe. Mohamedi Habibu Mnyaa Mbunge wa Mkanyageni, ilikuwa nafasi nzuri kwa serikali kuweza kusikiliza maombi yao na kutoa maamuzi, badala yake siasa zikatumika, maombi yakakataliwa leo Bunge linaunda kamati ya uchunguzi iende mtwara wakachunguze nini ikiwa tayari hoja zao zilikataliwa?
Ieleweke kuwa nchi yetu itajengwa na watanzania wenyewe kwa kushirikiana na kusikilizana. Amani ya kweli itapatikana ikiwa haki itaonekana kutendeka kwa jamii yote. Waheshimiwa waandishi wa habari, haya ni sehemu tu ya mambo ambayo tunakusidia kumfikishia rais wetu ili aweze kuyafanyia kazi.
Mungu Ibariki CUF, Mungu ibarika Tanzania.
Imetolewa na
Shaweji Mketo,
Naibu Mkurugenzi wa Mipango, Uchaguzi na Siasa,
tarehe 22 Juni 2013

Friday, June 21, 2013

Matusi yachangia Stars kufungwa:Gadi



Simon Mmbando.
Askofu Charles Gadi wa kanisa la Good News for all Minister  amesema kuwa lugha ya udhalilishaji na matusi vilichangia kufungwa kwa timu ya Taifa Stars.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo alisema ziposababu nyingi zilizo sababisha Taifa Stara kupoteza mchezo wake dhidi ya Ivory coast uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Askofu Gadi alisema sababu kubwa iliyopelekea Taifa Stara kupoteza mchezo wake ni Mizaha mingi ya washangiliaji na matusi yaliyokithiri ambayo mbele za Mungu huonekana kama sio maombi.

Unapo tukana Mungu husika kama vile akusikiapo unavyo omba hvyo sisi sote kama Watanzania tulimwamini Mungu na tukiamini tutapata ushindi. Ni jambo la ajabu kuona watu wanaomba msaada wa Mungu na wengine wanatukana matusi.

Hali hiyo hukinzana na Mungu na mwisho wake kushindwa kama hali hiyo ya matusi ikipitiliza ushindi kwetu itakuwa ni ndoto.

Aliendelea kusema kuwa goli la kwanza lilifungwa kwa maombi ya Watanzania waliokuwa pale na walio kuwa majumbani kwao wakiomba, lakini matusi yalio endelea ya kutukana maumbile ya siri ya Mama zetu,Wake zetu, Wakwe zetu, Dada zetu na Watoto wetu wa kike yalitukwamisha.

Matusi hayo yalikwamisha ushindi kwa Taifa Stara kwani unapo tukana maumbile ya akina mama ni sawa na kuchafua na kukejeli uumbaji wa Mungu kwa akina mama na hali hiyo hupelekea laana na hali ya kushindwa.

Alisema cha ajaba hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na imefikia wakati tuziombe mamlaka usika hasaBunge na Wabunge na akina mama wasiyafumbie macho mambo hayo bali watunge sheria zenye kutoa adhabu kali kwa watu wenye mazoea ya kutamka matusi.

Kama zilivyo nchi nyingine kutema bigijii unaweza kufungwa miezi mitatu kwanini nch yetu unalifumbia macho kosa matusi Mabaya kama hayo au yanaonekana ni situ cha kawaida, utadhani Uwanjani pale palikuwa na kiwanda cha kuzalisha matusi.

Hali hiyo ya matusi inachafua sura nzima ya tasnia ya michezo  na itatufanya tuwe wasindikizaji kwani mambo haya yana athari sana katika ulimwengu wa roho na yasipo tiliwa mkazo kuna uwezekano wakuwa poteza maajenti ambao huja nchini kutafut wachezaji na kuwauza nje ya nchi.

Kuhusu usalama kwa watazamaji alisema uwanja ulijaa kwa kiwango ambacho ni tatizo kama kukitokea jambo la hatari kwani watu walijazana hadi njia za lupita watu, wanaishauri serikali iweke screen kubwa nje ya uwanja ili kwa watakaochelewa
Kuingia uwanjani waangalie mpira lupita nje ya uwanja.

Taifa Star ilicheza mchezo huo dhidi ya Ivory coast Juni,16 mwaka huu na  kupoteza kwa kufungwa magoli 4-2 na kupoteza nafasi yakushiriki kombe la dunia litakalofanyika  nchini Brazil Juni, mwakani.


Mwisho alitoa pongezi kwa Wachezaji, Serikali,Wananchi, TFF na kamati (Saidia Taifa Star Ishinde) kwajitahada walizofanya katika maandalizi ya timu yetu, pia wakazi wote wa Dar es Salaam na wote waliofika uwanjani kwani walionyesha uzalendo wa kuipenda nchi yao.

Thursday, June 13, 2013

SIMBA YAPANGA KUMUUZA AMRI KIEMBA WYDAD CASABLANCA YA MOROCCO BAADA YA KUMSAINISHA MKATABA MPYA


 
               Siku moja baada ya Simba kumwongezea mkataba Amri Kiemba, klabu hiyo ya Msimbazi inatarajia kumpiga bei kiungo huyo mwenye kiwango kilichosimama kwenye mstari kwa timu ya Wydad Ac Casablanca ya Morocco.

Mpango wa kumuuza Kiemba umekuja baada ya mashushushu wa timu hiyo ya Morocco kuridhishwa na kiwango alichoonyesha wakati akiichezea Taifa Stars dhidi ya Morocco katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwakani.
Katika mchezo huo, Stars ilifungwa mabao 2-1, huku Kiemba akifunga bao nzuri la kufutia machozi kwa kiki ya mwendo mrefu nje ya boksi la hatari.
Zakaria Hanspope, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, amelithibitishia gazeti la Mwananchi jana kuwa, mazungumzo ya awali ya kuuzwa kwa kiungo huyo aliyewahi kucheza Yanga yako hatua za mwisho kukamilika.
“Ni kweli, mazungumzo ya awali yameshafanyika kati ya Simba na uongozi wa Wydad Ac Casablanca, leo tunamalizia tulipofikia,” alisema Hanspope.
“Niko Morocco kufanya mazungumzo ya mwisho na uongozi wa Wydad Casablanca, natumaini tutafikia mahala pazuri Mungu akijalia,” alisema Hanspope.
Mmoja wa vigogo wa Kundi la Friends of Simba ndiyo aliyeushtua uongozi juu ya mpango huo, ambao nao waliharakisha kumsainisha mkataba mpya kabla ya kumuuza. Juzi, Simba ilimsainisha Kiemba mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh35 mil.