Langa ambaye aliingia rasmi kwenye muziki baada ya kuwa mmoja ya washindi Coca Cola Pop Star, ambapo aliunda kundi la WAKILISHA kwa pamoja na Shaa pamoja na Witness. Walifanikiwa kutoa nyimbo kadhaa ambazo zilitamba sana kwenye vituo vya Radio na Television.
Thursday, June 13, 2013
MSANII WA HIP HOP LANGA AFARIKI DUNIA
Langa ambaye aliingia rasmi kwenye muziki baada ya kuwa mmoja ya washindi Coca Cola Pop Star, ambapo aliunda kundi la WAKILISHA kwa pamoja na Shaa pamoja na Witness. Walifanikiwa kutoa nyimbo kadhaa ambazo zilitamba sana kwenye vituo vya Radio na Television.
HOTUBA YA MATUMIZI YA BAJETI YA SERIKALI YA ZANZIBAR MWAKA 2013-2014
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf
Mzee akielekea katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya
kuwasilisha Hotuba ya matumizi ya Bajeti ya Serikali ya mwaka wa Fedha
2013-2014.mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
Baadhi ya
Makatibu wa kuu wa wizara za Serikali wakiwa katika Ukumbi wa Baraza la
Wawakilishi wakifuatilia hotuba ya matumizi ya Bajeti ya Serikali ya
mwaka wa Fedha 2013-2014.iliowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee mbweni nje ya Mji
wa Zanzibar.
Baadhi ya
Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali wakifuatilia hotuba ya
matumizi ya Bajeti ya Serikali ya mwaka wa Fedha
2013-2014.iliowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na
Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee mbweni nje ya Mji wa Zanzibar
Tuesday, June 11, 2013
Hali ya Mandela inasemekana kuwa tete
"mzee Mandela yuko hospitalini na hali yake bado haijabadilika.''
Maombi yakekuwa yakifanywa makanisani kote nchini Afrika Kusini kumuombea Mandela ambaye anatibiwa kwa ugonjwa wa mapafu.
Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 94, alipelekwa hospitalini mapema Jumamosi , ikiwa ni mara ya tatu kulazwa hospitalini mwaka huu.
Kwa mujibu wa duru za urais, Mandela amekuwa akiugua kwa muda mjini Johannesburg baada ya kukumbwa tena na ugonjwa wa mapafu.
Alilazwa hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi mnamo Jumamosi.
Kwa mujibu wa taarifa za urais, Rais President Jacob Zuma, amerejelea wito wake kwa watu nchini Afrika Kusini kumuombea Madiba wakati huu anapougua.
Lakini mwandishi wa BBC mjini Pretoria, Karen Allen, anasema kuwa kuna matumaini amdogo kuwa Mandela aliyeongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, huenda kupona.
Anasema kuwa wengi walipata matumani baada ya bintiye Mandela Zindzi, kusema kuwa babake yuko salama na kuwa anaendelea kupata nafuu.
Mkewe Mandela Graca Machel, alifutilia mbali, ziara yake mjini London Jumamosi ili kuwa kando ya mumewe.
Mandela alikuwa Rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 hadi 1999.
Alifungwa jela miaka 27 na anaaminika kuwahi kuugua ugonjwa wa mapafu alipokuwa akifanyishwa kazi ngumu katika machimbo ya mawe akiwa jela
Lwakatare aachiwa kwa dhamana Kisutu
Mkurugenzi wa Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Wilfred Lwakatare
Posted Jumanne,Juni11 2013 saa 11:10 AM
Kwa ufupi
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es
Salaam imekubali kumwachia Mkurugenzi wa Usalama wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Wilfred Lwakatare kwa dhamana ya
Sh10Milioni.
Kwa habari zaidi ungana nami baadaye
Kwa habari zaidi ungana nami baadaye
Monday, June 10, 2013
"Ningekuwa Ruge, Ningemwomba Radhi Jaydee"Asema Sebo
Monday, June 10, MARA BAADA YA TAIFA STARS KUREJEA-POULSEN ANENA NA KUSEMA WANGEKUWA WANGECHEZA 11 UWANJANI WASINGEFUNGWA NA,MOROCCO
Kocha wa Timu bali matokeo ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amesema refa wa mechi ya Taifa Stars na Morocco iliyopigwa Marrakech Jumamosi kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia Brazil mwakani aliuwa mchezo kwa kutoa kadi nyekundu kwa mchezaji Aggrey Morris.
Akitoa maoni ya mchezo huo, Poulsen alisema alisikitishwa na jinsi refa huyo alitoa adhabu kali ambayo haiendani na kanuni za FIFA.
Aggrey Morris alioneshwa kadi nyekundu baada ya kugongana na Abderazak Hemed Allah ambaye aliifungia Morocco bao la kwanza katika dakika ya 37.
“Hakuwa na sababu ya kumuonesha Morris kadi nyekundu kwani tayari alishawapa Morocco penalti, alisema Poulsen huku akiongeza, “FIFA imeshawaonya marefa mara kadhaa dhidi ya kuua mchezo kwa namna hii ya kutoa adhabu kali kupita kiasi.”
Poulsen alisifu wachezaji wake na kusema licha ya kucheza pungufu walipambana uwanjani na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa Amri Kiemba. Morocco walishinda kwa 2-1.
“Kama tungecheza kumi na moja hadi mwisho nina uhakika tungeshinda mechi hii lakini refa aliiua mechi na huwezi kufanya hivi katika mechi ngumu kama hii,” alisema Poulsen.
Kocha huyo alisema kupata goli la ugenini unapochez na timu ngumu kama Morocco ni jambo la kujivunia hasa mnapokuwa pungufu uwanjani.
Alisisitiza kuwa sasa wanaelekeza nguvu zote katika mechi shidi ya Ivory Coast Jumapili ijayo. “Mambo ya Morocco yamekwisha sasa tunafikiria namna ya kushinda mechi ya Jumapili.
Tanzania iko katika kundi C inayoongozwa na Ivory Coast yenye pointi 10, Tanzania 6, Morocco 5 na Gambia 1.
Taifa Stars imerejea Jumatatu alfajiri kutokea Marrakech Morocco na itaendelea na kambi ya wiki moja ili kujiandaa na mechi dhidi ya Ivory Coast.
Nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja alisema wachezaji walicheza kwa ari kubwa na walifurahishwa na jinsi watanzania walijitokeza kwa wingi.
“Tulipata faraja kubwa sana kuwaona watanzania wengi uwanjani…mambo ya Morocco yameisha sasa tuangalie Ivory Coast,” alisema.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe ambaye bia yake inadhamini Taifa Stars, alisema wacezaji walijitahidi hasa ikizingatiwa walicheza pungufu na hata wakafanikiwa kufunga bao moja.
“Katika hali kawaida, wachezaji wengine wangekata tamaa lakini bao hili moja linaonesha kuwa wachezaji walikuwa na ari ya kupata ushindi,” alisema Bw Kavishe.
Alisema wao kama wadhamini wana imani kubwa na Taifa Stars na kwamba wanaamini hii ni safari ya mafanikio ambayo ilianza mwaka mmoja uliopita tangu Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ianze udhamini huo.
Chadema yakubali Serikali tatu
Mbeya/Dar. Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman ameweka bayana kuwa wanaunga mkono Rasimu ya Katiba na hasa
suala la Muungano wa Tanzania kuundwa na Serikali tatu kama
ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Amesema mambo mengi yaliyopendekezwa na
chama chake yamefanyiwa kazi na Tume ya Mabadiliko na kuishangaa CCM
akidai kwamba inapinga rasimu hiyo hususan suala la Serikali tatu wakati
kimsingi watu wa Tanzania Bara wamekuwa wakipunjika kwenye muundo wa
sasa wa Muungano.
Akihutubia mkutano wa kampeni ya
kuwania udiwani wa Kata ya Iyela katika Uwanja wa Bongonela, Mbeya jana
jioni, Mbowe alisema chama chake kinataka kuona Serikali ya Tanganyika
ikifufuliwa. Alikuwa akimnadi mgombea wa Chadema, Charles Mkela.
Alisema Chadema kinataka kuona
Wazanzibari wakiwa na Serikali yao ili wajiamulie mambo yao na pia
Watanganyika wawe na uongozi wao lakini waunganishwe na Serikali ya
Muungano.
Alisema muundo wa sasa wa Muungano una
matatizo. Kwa mfano, mbunge wa Zanzibar anawakilisha watu wachache zaidi
ukilinganisha na mbunge wa Bara. Wananchi mtashangaa sote tunalipwa
sawa.”
“Ila zikija Serikali tatu ina maana
kuwa kila upande wa Muungano utatumia rasilimali zake. Haya mambo
kulipana fedha nyingi kwa kazi kidogo yatakoma.”
Subscribe to:
Posts (Atom)


