Friday, June 21, 2013

Matusi yachangia Stars kufungwa:Gadi



Simon Mmbando.
Askofu Charles Gadi wa kanisa la Good News for all Minister  amesema kuwa lugha ya udhalilishaji na matusi vilichangia kufungwa kwa timu ya Taifa Stars.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo alisema ziposababu nyingi zilizo sababisha Taifa Stara kupoteza mchezo wake dhidi ya Ivory coast uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Askofu Gadi alisema sababu kubwa iliyopelekea Taifa Stara kupoteza mchezo wake ni Mizaha mingi ya washangiliaji na matusi yaliyokithiri ambayo mbele za Mungu huonekana kama sio maombi.

Unapo tukana Mungu husika kama vile akusikiapo unavyo omba hvyo sisi sote kama Watanzania tulimwamini Mungu na tukiamini tutapata ushindi. Ni jambo la ajabu kuona watu wanaomba msaada wa Mungu na wengine wanatukana matusi.

Hali hiyo hukinzana na Mungu na mwisho wake kushindwa kama hali hiyo ya matusi ikipitiliza ushindi kwetu itakuwa ni ndoto.

Aliendelea kusema kuwa goli la kwanza lilifungwa kwa maombi ya Watanzania waliokuwa pale na walio kuwa majumbani kwao wakiomba, lakini matusi yalio endelea ya kutukana maumbile ya siri ya Mama zetu,Wake zetu, Wakwe zetu, Dada zetu na Watoto wetu wa kike yalitukwamisha.

Matusi hayo yalikwamisha ushindi kwa Taifa Stara kwani unapo tukana maumbile ya akina mama ni sawa na kuchafua na kukejeli uumbaji wa Mungu kwa akina mama na hali hiyo hupelekea laana na hali ya kushindwa.

Alisema cha ajaba hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na imefikia wakati tuziombe mamlaka usika hasaBunge na Wabunge na akina mama wasiyafumbie macho mambo hayo bali watunge sheria zenye kutoa adhabu kali kwa watu wenye mazoea ya kutamka matusi.

Kama zilivyo nchi nyingine kutema bigijii unaweza kufungwa miezi mitatu kwanini nch yetu unalifumbia macho kosa matusi Mabaya kama hayo au yanaonekana ni situ cha kawaida, utadhani Uwanjani pale palikuwa na kiwanda cha kuzalisha matusi.

Hali hiyo ya matusi inachafua sura nzima ya tasnia ya michezo  na itatufanya tuwe wasindikizaji kwani mambo haya yana athari sana katika ulimwengu wa roho na yasipo tiliwa mkazo kuna uwezekano wakuwa poteza maajenti ambao huja nchini kutafut wachezaji na kuwauza nje ya nchi.

Kuhusu usalama kwa watazamaji alisema uwanja ulijaa kwa kiwango ambacho ni tatizo kama kukitokea jambo la hatari kwani watu walijazana hadi njia za lupita watu, wanaishauri serikali iweke screen kubwa nje ya uwanja ili kwa watakaochelewa
Kuingia uwanjani waangalie mpira lupita nje ya uwanja.

Taifa Star ilicheza mchezo huo dhidi ya Ivory coast Juni,16 mwaka huu na  kupoteza kwa kufungwa magoli 4-2 na kupoteza nafasi yakushiriki kombe la dunia litakalofanyika  nchini Brazil Juni, mwakani.


Mwisho alitoa pongezi kwa Wachezaji, Serikali,Wananchi, TFF na kamati (Saidia Taifa Star Ishinde) kwajitahada walizofanya katika maandalizi ya timu yetu, pia wakazi wote wa Dar es Salaam na wote waliofika uwanjani kwani walionyesha uzalendo wa kuipenda nchi yao.

Thursday, June 13, 2013

SIMBA YAPANGA KUMUUZA AMRI KIEMBA WYDAD CASABLANCA YA MOROCCO BAADA YA KUMSAINISHA MKATABA MPYA


 
               Siku moja baada ya Simba kumwongezea mkataba Amri Kiemba, klabu hiyo ya Msimbazi inatarajia kumpiga bei kiungo huyo mwenye kiwango kilichosimama kwenye mstari kwa timu ya Wydad Ac Casablanca ya Morocco.

Mpango wa kumuuza Kiemba umekuja baada ya mashushushu wa timu hiyo ya Morocco kuridhishwa na kiwango alichoonyesha wakati akiichezea Taifa Stars dhidi ya Morocco katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia mwakani.
Katika mchezo huo, Stars ilifungwa mabao 2-1, huku Kiemba akifunga bao nzuri la kufutia machozi kwa kiki ya mwendo mrefu nje ya boksi la hatari.
Zakaria Hanspope, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, amelithibitishia gazeti la Mwananchi jana kuwa, mazungumzo ya awali ya kuuzwa kwa kiungo huyo aliyewahi kucheza Yanga yako hatua za mwisho kukamilika.
“Ni kweli, mazungumzo ya awali yameshafanyika kati ya Simba na uongozi wa Wydad Ac Casablanca, leo tunamalizia tulipofikia,” alisema Hanspope.
“Niko Morocco kufanya mazungumzo ya mwisho na uongozi wa Wydad Casablanca, natumaini tutafikia mahala pazuri Mungu akijalia,” alisema Hanspope.
Mmoja wa vigogo wa Kundi la Friends of Simba ndiyo aliyeushtua uongozi juu ya mpango huo, ambao nao waliharakisha kumsainisha mkataba mpya kabla ya kumuuza. Juzi, Simba ilimsainisha Kiemba mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh35 mil.

MSANII WA HIP HOP LANGA AFARIKI DUNIA

Msanii wa muziki wa kizazi Langa Kileo amefariki dunia jioni ya leo katika hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua ugonjwa wa Malaria.

Langa ambaye aliingia rasmi kwenye muziki baada ya kuwa mmoja ya washindi Coca Cola Pop Star, ambapo aliunda kundi la WAKILISHA kwa pamoja na Shaa pamoja na Witness. Walifanikiwa kutoa nyimbo kadhaa ambazo zilitamba sana kwenye vituo vya Radio na Television.

HOTUBA YA MATUMIZI YA BAJETI YA SERIKALI YA ZANZIBAR MWAKA 2013-2014

  • Written by  Ajuaye Mcha

untitled 58b01

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee akielekea katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kuwasilisha Hotuba ya matumizi ya Bajeti ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2013-2014.mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.

untitled2 e5db1
Baadhi ya Makatibu wa kuu wa wizara za Serikali wakiwa katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia hotuba ya matumizi ya Bajeti ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2013-2014.iliowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
untitled3 500ce
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali wakifuatilia hotuba ya matumizi ya Bajeti ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2013-2014.iliowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee mbweni nje ya Mji wa Zanzibar

Tuesday, June 11, 2013

Hali ya Mandela inasemekana kuwa tete


Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, angali katika hali mbaya ingawa imeweza kudhibitiwa. Mandela amelazwa katika hospitali moja mjini Pretoria.
"mzee Mandela yuko hospitalini na hali yake bado haijabadilika.''
Maombi yakekuwa yakifanywa makanisani kote nchini Afrika Kusini kumuombea Mandela ambaye anatibiwa kwa ugonjwa wa mapafu.
Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 94, alipelekwa hospitalini mapema Jumamosi , ikiwa ni mara ya tatu kulazwa hospitalini mwaka huu.
Kwa mujibu wa duru za urais, Mandela amekuwa akiugua kwa muda mjini Johannesburg baada ya kukumbwa tena na ugonjwa wa mapafu.
Alilazwa hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi mnamo Jumamosi.
Kwa mujibu wa taarifa za urais, Rais President Jacob Zuma, amerejelea wito wake kwa watu nchini Afrika Kusini kumuombea Madiba wakati huu anapougua.
Lakini mwandishi wa BBC mjini Pretoria, Karen Allen, anasema kuwa kuna matumaini amdogo kuwa Mandela aliyeongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, huenda kupona.
Anasema kuwa wengi walipata matumani baada ya bintiye Mandela Zindzi, kusema kuwa babake yuko salama na kuwa anaendelea kupata nafuu.
Mkewe Mandela Graca Machel, alifutilia mbali, ziara yake mjini London Jumamosi ili kuwa kando ya mumewe.
Mandela alikuwa Rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 hadi 1999.
Alifungwa jela miaka 27 na anaaminika kuwahi kuugua ugonjwa wa mapafu alipokuwa akifanyishwa kazi ngumu katika machimbo ya mawe akiwa jela

Lwakatare aachiwa kwa dhamana Kisutu


Mkurugenzi wa Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema),  Wilfred Lwakatare 


Posted  Jumanne,Juni11  2013  saa 11:10 AM
Kwa ufupi
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam  imekubali kumwachia Mkurugenzi wa Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema),  Wilfred Lwakatare kwa dhamana ya Sh10Milioni.
Kwa habari zaidi ungana nami baadaye

Monday, June 10, 2013

"Ningekuwa Ruge, Ningemwomba Radhi Jaydee"Asema Sebo


Mtangazaji wa kipindi cha Sun Downer cha Magic FM, Sebo amesema kwamba shangwe zilizolipuka mara baada ya Jaydee kutajwa kuwa miongoni mwa wanaowania tuzo ya msanii bora wa kike ktk tuzo za KTMA, ni ishara ya mwanadada huyo kukubalika ktk jamii. Mtangazaji huyo amesema kwamba Jaydee ni mwanamke mwenye uthubutu ktk harakati za kuyasaka maisha na kwamba yeyote mwenye nia ya kukwamisha jitihada zake aibu na iwe juu yake. Ameongeza kuwa kukubalika kwa mwanadada huyu pia kulidhihirika pale ambapo watazamaji ktk tukio hilo walipomshinikiza Meneja wa msanii huyo (Gadna) kutaja kiingilio na tarehe ya maadhimisho ya miaka 13 ya Jaydee ktk uga wa muziki. Hivyo, Sebo anaona ni vyema Ruge akajishusha na kumaliza tofauti zake dhidi ya Jaydee.