Posted on 5jully 2013
Waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Fredrick Sumaye amezindua safari ya kuelekea nchini Kenya
ya wanafunziwa chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam (DSJ).na kuwataka kutumia
fursa hiyo kuitangaza zaidi Tanzania
Sumaye amezindua safari hiyo chuoni hapo na kuwataka wanafunzi
kwenda kujifunza utalii na jinsi ya kumudu maisha pasipo kutegemea kuajiriwa na
serikali bali kujiajiri wenyewe kwa elimu waliyoipata.
Pia aliwataka wanafunzi hao kujifunza mazingira ya Kenya jinsi yalivyo tofauti na ya hapa kwetu Tanzania
na hata watalii wengi huvutiwa
kutembelea nchi hiyo na kuwaongezea pato lao la taifa.
Alisema kuwa nchi ya Kenya iko juu kiuchumi tofauti na
Tanzania hivyo basi mnavyokwenda ni vizuri mkajijifunze kutoka
kwa wenzetu na kuja kuyafanyia kazi kwa ufasaha zaidi ili kuleta maendeleo kwa taifa Letu.
Sumaye aliendelea kusema wafanyakazi wa Kenya ni wafanyakazi waamifu na wachapa kazi sana
tofauti na Tanzania
hivyo basi nasi tukajifunze vitu hivyo
katika ziara hii ili tuweze kulijenga taifa letu.
Kwa upande wa biashara alisema Kenya
wanauwezo mkubwa wa kufanya biashara za nje tofauti na Tanzania hivyo nasi tukaifunze
mbinu hizo za kibiashara kutoka kwao ili tuje kuwa mabalozi hapa nchini..