Monday, August 13, 2012

usajili


MOURA ATUA PSG.
WAKATI hekeheke za usajili zikiendelea kupamba moto barani Ulaya klabu ya Psg imeizidi ujanja Manchester United kwa kumsajili kinda wa Kibrazil Lukas Moura.
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19  ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani na kipaji chake kinafananishwa na nyota  wenzake wa Brasil kama Ronaldo De’lima na Ronaldinho Gaucho.
Kinda huyo anayechezea klabu ya soka ya Sao Paulo alikuwa akiwaniwa kwa udi na uvumba  na klabu hiyo kwa nia ya kukiimarisha kikosi hicho kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya uingereza.
Mtandao wa klabu ya soka ya Sao Paulo uliripoti kuwa Manchester United ilishindwa kufikia dau lililotangazwa  la paundi mil 45 kitendo kilichowafanya kumuuza kwa Psg waliofikia dau hilo.
Hata hivyo kinda huyo ataanza kuitumikia klub hiyo kuanzia januari mwakani kutokan na makubaliano yaliyofikiwa kati ya klabu yake ya Sao Paulo na Psg.
Kinda huyo ameonyesha uwezo mkubwa katika michezo ya olimpiki iliyokuwa ikifanyika jijini London alipokuwa akiwakilisha nchi yake ya Brasil kitendo kilicho washawishi viongozi wa Psg kumsajili.
Baada timu ya Mancherster United kumkosa kinda huyo imehamishia nguvu zake kwa kiungo wa Atletic Madrid Ika munian ambaye ataigalimu kiasi cha paund million 30.

No comments:

Post a Comment