Friday, August 10, 2012

SPORT

OURA ALETA KIZAIZAI KWENYE SOKO LA USAJILI - AS ROMA WASEMA DE ROSSI ANAUZWA KWA ZAIDI YA €100 MILLION, SANTOS WASEMA NEYMAR NDIO HAGUSIKI KABISA



Siku moja baada ya mchezaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea Sao Paolo Lucas Moura kusajiliwa kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekdi kwenye soko la usajili nchini Brazil kwenda Paris Saint Germain, marais wa vilabu vingine duniani wameanza kutoa kauli ambazo zitaleta gumzosana kwenye soko la usajili duniani.

PSG wametumia kiasi cha £150 millioni katika kipindi cha mwezi mmoja kufanya manunuzi ya kuwasajili Lucas Moura, Zlatan Ibrahimovic  na Thiago Silva.

Matumizi ya namna hii yameanza kuwatia vichaa baadhi ya viongozi wa vilabu vingine, Kwa upande wa AS Roma ambao mchezaji wao Daniele de Rossi amekuwa akitakiwa na Manchester City nao wameingia tamaa.


Akiongea mkurugenzi wa Roma Walter Sabatini mara laipoulizwa juu ya thamani ya Rossi, akaanza kwanza kuzungumzia mchezaji wa Fiorentina Stevan Jovetic ambaye aliwekwa kwenye thamani ya €30 million na klabu yake, na Napoli nao ambao walisema mchezaji wao Edinson Cavani  alikuwa na thamani ya €100 million kwa timu ambazo zilikuwa zinamtolea macho.

"Gharama ya De Rossi ni juu zaidi ya majina yote uliyoyataja hapo juu, kwani maana hiyo Rossi ana gharama zaidi €100 miilion na zaidi." -Sabatini

Ikiwa na kiungo huyo mwenye miaka 29 atakuwa na gharama hiyo , unadhani mchezaji ambaye anatajwa kuja kuwa na kiwango kikubwa kuliko wote, Neymar atakuwa thamani ya fedha ngapi?

Kwa mujibu wa raisi wa Santos Luis Alvaro, amesema baada ya Lucas Moura kuuzwa kwa bei ya €45 million huku alilipwa mshahara wa £250,000 kwa wiki, basi bei ya Neymar haielezeki - yaani anaweza hata asiuzike.

Neymar kwenye mkataba wake ana kipengele kinachomruhsu kuuzwa endapo klabu inayomtaka itatoa £57 million.

Lakini baada ya Moura kuuzwa kwa bei chafu bei  hiyo ya Neymar inaweza ikapanda maradufu.

ANDIKA CHOCHOTE KUTOKANA NA HIZI PICHA ZA MBWANA SAMATTA.


HIKI NDICHO ALICHOKISEMA MSEMAJI WA SIMBA EZEKIEL KAMWAGA.


Salaam ! Kwa waliosoma gazeti la Super Star la leo, watakuwa wameona stori yenye kichwa cha habari; "Sinema Mpya Ngassa, Twite." Ndani yake kuna maelezo kwamba Ngassa na Mbuyi Twite wanakwenda Yanga. Kuwa eti Azam wameamua kumpeleka Yanga kwa vile wamekasirishwa na hatua ya Simba kumsajili Redondo. Chanzo cha habari, hakitajwi. Wamezungumza na mimi nimesema hakuna kitu kama hicho. Wamezungumza na Msemaji wa Azam kawaambia hakuna kitu kama hicho. Lakini wameandika hiyo stori kwa kutumia "VYANZO VYAO." Hivi mwandishi kama huyu nikigoma kumpa ushirikiano nitakuwa nimekosea? Chini yake kuna stori ya Okwi. Uongo mtupu. Sote tunajua Okwi amekwenda kuitumikia timu yake ya taifa na atarejea baada ya hapo. Lakini mwandishi, kwa sababu zake, ameamua kufanya hilo lionekane ni tatizo!!!!!! Kwamba sasa Okwi bye bye Simba...Inauma sana lakini waandishi hawa ni rafiki zangu, wanataaluma wenzangu nk.... Tutafanyaje kazi zetu katika mazingira haya ambapo mtu anatunga stori ili auze gazeti????? Naomba mfahamu kwamba kuna watu wanaumia sana kwa habari za namna hii. Hawali wakashiba na wanakaa na wahka siku nzima. Tuthamini hisia za wenzetu

No comments:

Post a Comment