Monday, September 24, 2012

HABARI YA MICHEZO


                                     LIGI  KUU YA VODACOM KUENDELEA KUSHIKA  KASI
Ligi kuu ya soka ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi  katika viwanja mbalimbali baada ya kushuhudia mwishoni mwa wiki kutokana na baadhi ya vilabu kujipatia ushindi katika viwanja mbalimbali.
Ligi hiyo itaendelea tena  Jumatano tarehe 25 mwezi huu   katika  uwanja wa Mkwakwani  mjini Tanga ambapo  wenyeji Coast union watawakaribisha  Kagera sugar na katika uweanja wa Jamhuri mmjini morogoro Polisi morogoro watawakaribisha  Toto Africa  ya mwanza.
Pia ligi hiyo itaendelea tena tarehe 28 mwezi huu katika uwanja wa Chamazi pale timu ya soka ya Azam itakapoikaribisha  timu ya Jkt Ruvu kutoka Mkoani Pwani  
Mabinngwa watetezi wa ligi hiyo Simba wanatarajiwa kushuka katika  uwanjawa taifa mnamo  tarehe 29 mwezi huu kucheza na wajelajela Prisons kutoka Mbeya wakati katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid wenyeji Jkt Oljoro watawakaribisha Mgambo kutoka mjini Tanga.
Ligi hiyoitaendelea tarehe 30 wakati mabingwa wa kombe la Africa Mashariki na kati (KAGAME) Yanga watakapowakaribisha African Lyon katika uwanja mkuu wa Taifa huku mechi za wiki hii zikikamilishwa  na mechi kati ya Ruvu shooting watakaowakaribisha Mtibwa sugar katika uwanja wa Chamazi.
 Wakati ligi hiyo ikiendelea  kushika kasi vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo bado havijakabidhiwa fedha za kujikimu na mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom kutokana na mdhamini kutakaka kukutana kwanza vilabu hivyo ili kufikia mwafaka.
Mwafaka  wanaoutaka vilabu hivyo ni kuongezewa fedha za kujikimu pamoja kuruhusiwa kwa kipengele kinachoziruhusu klabu kuwa ni mdhamini mbadala lli iwe chachu kwao katika kuleta ushindani kwenye ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment