LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA KUSHIKA KASI
Ligi kuu ya soka ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa
kuendelea kutimua vumbi katika viwanja
mbalimbali baada ya kushuhudia mwishoni mwa wiki kutokana na baadhi ya vilabu kujipatia
ushindi katika viwanja mbalimbali.
Ligi hiyo itaendelea tena Jumatano tarehe 25 mwezi huu katika
uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga
ambapo wenyeji Coast union watawakaribisha Kagera sugar na katika uweanja wa Jamhuri
mmjini morogoro Polisi morogoro watawakaribisha
Toto Africa ya mwanza.
Pia ligi hiyo itaendelea tena tarehe 28 mwezi huu katika
uwanja wa Chamazi pale timu ya soka ya Azam itakapoikaribisha timu ya Jkt Ruvu kutoka Mkoani Pwani
Mabinngwa watetezi wa ligi hiyo Simba wanatarajiwa kushuka
katika uwanjawa taifa mnamo tarehe 29 mwezi huu kucheza na wajelajela
Prisons kutoka Mbeya wakati katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid wenyeji Jkt
Oljoro watawakaribisha Mgambo kutoka mjini Tanga.
Ligi hiyoitaendelea tarehe 30 wakati mabingwa wa kombe la
Africa Mashariki na kati (KAGAME) Yanga watakapowakaribisha African Lyon katika
uwanja mkuu wa Taifa huku mechi za wiki hii zikikamilishwa na mechi kati ya Ruvu shooting
watakaowakaribisha Mtibwa sugar katika uwanja wa Chamazi.
Wakati ligi hiyo
ikiendelea kushika kasi vilabu
vinavyoshiriki ligi hiyo bado havijakabidhiwa fedha za kujikimu na mdhamini wa
ligi hiyo kampuni ya Vodacom kutokana na mdhamini kutakaka kukutana kwanza
vilabu hivyo ili kufikia mwafaka.
Mwafaka wanaoutaka
vilabu hivyo ni kuongezewa fedha za kujikimu pamoja kuruhusiwa kwa kipengele
kinachoziruhusu klabu kuwa ni mdhamini mbadala lli iwe chachu kwao katika kuleta
ushindani kwenye ligi hiyo.